NA HAJI NASSOR, PEMBA:
email: hajipembatoday@gmail.com:
JAMII kisiwani Pemba, imetakiwa kujitenga
mbali na baadhi ya watu wanaotumia vibaya nafasi zao, kwa kushawishi kujiingiza
kwenye migogoro isiyokuwa na tija, kwani amani itakapochafuka, gharama ya
kuirejesha ni kubwa.
Hayo
yalielezwa na mtoa mada, ya utatuzi wa migogoro kisiwani humo, Ali Abdalla Juma,
wakati akielezea njia za kujinga na migogoro, kwenye mafunzo ya siku mbili ya
utatuzi wa migogoro, yalioandaliwa na Jumuiya mwemvuli ya asasi za kiraia
kisiwani Pemba PACSO, na kufanyika Chake chake.
Alisema,
inawezekana mtu kwa sababu ya cheo chake au umaarufu wake katika jamii,
akalikusanya kundi mfano kama la vijana, na kuwashawishi kuvunja amani, akijua
matokeo yake ni kujipatia maslahi yake binafsi.
Mtoa mada
huyo alieleza kuwa, jamii lazima ione umuhimu wa kuwepo kwa amani na utulivu,
na vivyo hivyo wawe mashuhuda wazuri, kwa nchi zilizotumbikia kwenye migogoro,
namna ambavyo maisha yanakuwa magumu.
‘’Sisi jamii, lazima kama kuna mtu kwa sababu ya cheo chake anataka kututumia vibaya, tujitenge nae, maana migogoro inapokuwa kuwa mikubwa, huzaliwa vurugu na mauwaji,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine, amewataka washiriki hao, wanapopokea migogoro kutoka katika jamii
zao, lazima waangalie chanzo, wahusika, athari na kisha waanze kutoa elimu ya upatanishi.
Akifungua mafunzo
hayo, Mwenyekiti wa ‘PACSO’ Mohamed Ali Khamis, alisema suala la ndoa kuwa ni
chanzo cha migogoro, sio dhana sahihi, bali wanandoa kwa tabia zao mbaya, ndio
inayopelekea migogoro.
Alieleza kuwa,
suala la ndoa hata la wake wanne, kwa imani ya dini ya kiislamu, halina shida,
bali ikiwa wanandoa watakosa kuaminiana, wao ndio huwa chanzo cha migogoro.
‘’Hata
nafasi ya usheha, uhakim, majaji mahakamani, ndoa, ofisi ya Mufti kama vilivyo
na asili yake, huwa havina shida, bali watumishi wa tasisi hizo, kama sio
waamifu wanaweza kuzalisha migogoro,’’alieleza.
Mapema
Katibu Mkuu wa PACSO Sifuni Ali Haji, alisema wapo wanaoshika nafasi za usheha,
mahakimu na majaji, wamekuwa chanzo cha migogoro, kutokana na kukosa uaminifu
katika utekelezaji wa majukumu yao.
Wakichangia mada
kwenye mafunzo hayo, washiriki hao walisema, bado wanandoa, wamiliki wa ardhi
kinyume na sheria, wamekuwa wakisababisha migogoro kwa jamii.
Walisema,
kama wenye mamlaka katika uongozi, wakishindwa kutenda haki na wakaendeleza
ubaguzi miongoni mwa jamii, hapo huwa rasihi, kuzaliwa kwa migogoro.
Mchungaji
Benjamen Kissanga, alisema haki ndio tunda la amani, ambalo kisha huzaa upendo
na wananchi kuishi kwa amani.
‘’Ikikosekana
haki kwa jamii, na uvumilivu ukifikia mwisho, huwa rahisi kuzaliwa na migogoro
ambayo mwisho wake, ni vurugu na visasi vya muda mrefu,’’alieleza.
Nae Mwenyekiti
wa Jumuiya ya wasioona Pemba ‘ZANAB’ Suleiman Mansour Suleiman, alisema
wanasiasa kwa kule kutotosheka na madaraka, wamekuwa wakiwagonganisha vichwa
wananchi na kuzaliwa kwa migogoro.
Nae Khadija
Ahmed, alisema kukosekana kwa uvumilivu na kutoheshimiana kwa wanandoa, hupelekea
migogoro ambayo mwishowake, huvunjika kwa ndoa.
Sheha wa
shehia ya Wara Massoud Mohamed Khamis na mshiriki Hamad Faki Rashid, walisema
elimu ya uraia, utaifa na uzalendo unahitajika kwa jamii, ili kuzuia migogoro.
Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyotayarishwa na PACSO kwa kushirikiana na the foundation for Civil Society na Search for Common Ground, na yamefadhiliwa na Umoja wa nchi za Ulaya EU.
Comments
Post a Comment