Skip to main content

UKWELI KUHUSU UWEZO WA UBONGO WA MTOTO MCHANGA HUU HAPA

 



NA HAJI NASSOR, PEMBA: email: hajipembatoday@gmail.com


JAMII imetakiwa kufahamu kuwa, ubongo wa mtoto mchanga unakuwa na ufahamu wa asilimia 25, katika kipindi cha miezi mitatu baada ya kuzaliwa, hivyo ni wakati mzuri kwa familia kumuandaa mtoto huyo watakavyo.

Tafiti zinaeleza kuwa, kama wazazi wanataka kuwa na mtoto mwenye ufahamu wa kujua mambo kadhaa, waanze nae ndani ya miezi mitatu ya mwanzo, kwa kuzungumza nae, kumshirikisha na kumtajia majina ya vitu kama vilivyo.

Mtaalamu wa malezi ya kisayansi ya awali ya watoto ‘SECD’ Rashid Said Nassor, alisema sio sahihi katika kipindi hicho, wazazi kuzungumza na mtoto wao, kwa kuigizia sauti ya kichanga.

‘’Sio vyema kwa wazazi na walezi kuyatumia maneno kama mma, nyamu, chamaki, mbobo, dizi, ledio, chimu, pecha bali kwa wakati huo, wanapowasiliana na watoto wao, wayatamke majina kama yalivyo,’’alieleza.

Aidha mtaalamu huyo alisema, sayansi ikaubali kuwa, mtoto anauwezo mkubwa wa kusikia na kuhifadhi kila kitu kinachozungumza kwenye jamii yake, kupitia ubongo wake.

Alieleza kuwa, ubongo wa mtoto mchanga mara anapozaliwa huwa, mtupu na unatabia ya kuchukua na kugandisha kila kitu, hivyo kama wazazi watatenga muda kumfundisha mtoto, anakuwa rahisi kuyamudu mazingira yake mapema.

Kwa upande wake mtaalamu wa malezi ya kisayansi na makuzi ya awali ya mtoto ‘SECD’ Zanzibar Mohamed Dau, alisema mtoto, akifikia umri wa mwaka mmoja, huwa na uwezo kama wa mtu mzaima kwa asililimia 60.

Alieleza kuwa, anapofikia umri wa miaka kati ya minne na hadi sita, uwezo wa ubongo wa mtoto huyo kufahamu kinachoendelea huwa ni kwa asilimia 90.

‘’Wazazi kama wanataka kuwa na watoto wenye uwelewa na kuyamudu mazingira yao, waanze akiwa na siku moja baada ya kuzaliwa hadi anapofikia miaka minane,’’alieleza.

Nae mkufunzi wa malezi hayo kutoka Tanzania bara Davis Gisuka, alisema umri sahihi kwa wazazi wa kumtayarisha mtoto wao, ni ule kabla ya kuanza elimu ya awali.

‘’Inaonekana kama vile ili umuandae mtoto vyema, ni kumsubiria hadi afikie miaka minene, kwa kumpeleka skuli nzuri na kumlipia fedha nyingi, wakati maandalizi mazuri ni tokea akiwa tumboni,’’alisisitiza.

Kaimu Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii Pemba ambae pia ni mtaalamu wa ‘ECD’ Omar Mohamed Ali, alisema bado wazazi, wanadhani ni kupoteza muda, wanapoelezwa faida ya kuwasiliana na watoto wao wachanga.

‘’Wazazi na walezi, wanaona kama vile uchawi fulani, wanapoambiwa kuwa ubongo wa mtoto mchanga, unapokea na kuhifadhi kila kitu, lakini ni sahihi na tafiti zimeshafanywa,’’alisisitiza.

 Wazazi na walezi kisiwani Pemba walisema, bado elimu ya ‘ECD’ haijasambaa ndani ya jamii, na ndio maana bado imekuwa ni vigumu kwao, kuitekeleza kama ilivyo.




Mkurugenzi Mkaazi wa tasisi ya Children in Crossfire Cragi Ferla alisema nguvu ya pamoja inahitajika, kati ya vyombo vya habari, maafisa ustawi na maendeleo kuifikisha elimu hiyo kwa jamii.

‘’ECD ni njia ya malezi thabiti, ambayo kama wazazi na walezi watayafuata kama ilivyo, wanaweza kuona maajabu ya kiungo cha ubongo kwa mtoto, kadiri anavyokuwa wanakua,’’alieleza.

Mzazi Hassina Haji Iddi ‘mama dula’ wa Gombani Chake chake alisema, ijapokuwa katika siku za hivi karibuni, baadhi ya kliniki wanazokwenda wamekuwa wakielimisha njia hizo.

‘’Zile kliniki ambazo manesi au madaktari wao wamerudi vyuoni katika miaka ya hivi karibuni, wamekuwa wakituelekeza mama wajawazito, lakini sio zahanati zote,’’alieleza.

Hidaya Kassim Khalfan wa Msingini Chake chake, alisema elimu hiyo inahitajika kupatiwa na akinababa pia, ili mtoto apate malezi, makuzi ya pande zote.



‘’Kidogo akina mama wamekuwa wakifanya kwa vitendo malezi ya kisayansi kwa watoto wao wachanga, kwa kule kuchangamana nao, lakini wanaume bado sana,’’alieleza.

Mzazi Issa Hassan Issa miaka 55 wa Mtambile alikiri kuwa, bado elimu hiyo ni mpya, ingawa wamekuwa wakiifanya lakini sio kama maagizo ya wataalamu.

Kwa upande wake sheikh Mohamed Hussein Imamu, alisema maandiko yanakubali mno, suala la malezi ya mtoto tokea akiwa tumboni na muda mfupi baada ya kuzaliwa kwake.

                                Mwisho            

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kutafuta matibabu nje ya nch