MIAKA 62 YA MAGEUZI MAKUBWA YA SEKTA YA AFYA KUTOKA UHABA, MARADHI NA VIFO VINAVYOZUILIKA HADI HUDUMA ZA KISASA KISIWANI PEMBA.
HABIBA ZARALI, PEMBA@@@@
Mapinduzi ya 12 Januari 1964 ni tukio la kihistoria lililobadili mwelekeo wa
maisha ya Mzanzibari katika nyanja zote za kijamii.
Mapinduzi
ya mwaka 1964 yalikuwa ni Mapinduzi ya uhai yakitambua kuwa bila afya bora,
hakuna maendeleo, hakuna elimu, wala hakuna uchumi.
Miaka
62 ya mapinduzi hayo, sekta ya afya Zanzibar nzima inasimama kama ushahidi
usiopingika kwamba Mapinduzi yamelinda maisha ya wananchi kwa vitendo.
KABLA
YA MAPINDUZI
Kiuhalisia kwa upande wa kisiwa cha Pemba kabla ya Mapinduzi matukufu ya
1964, huduma za afya zilikuwa katika hali ya kusikitisha.
Kwa vile Zanzibar nzima ilikuwa na hospitali kuu moja tu ya Mnazi Mmoja
ni wazi kuwa kwa upande wa Pemba ilikuwa na huduma finyu sana za afya.
Hakukuwa na hospitali kuu badala yake kulikuwa na hospitali 2 ya Chake chake na
Wete, kwa upande wa vituo vya afya vilikuwa ni 14 tu huku vikiwa havina
dawa wala wataalamu wa kutosha.
Madaktari
wazalendo walikuwa 4 ambapo madaktari bingwa hawakuwepo, wauguzi walikuwa
wachache jambo ambalo lilichangia wananchi wengi kupoteza maisha kwa magonjwa
yanayoweza kuzuilika.
Hakukuwa
na huduma za kibingwa, akina mama wengi walijifungulia majumbani bila msaada wa
kitaalamu.
Kutokana
na hali hiyo kabla ya mapinduzi wananchi wanyonge walishindwa kupata huduma za
afya na badala yake walikuwa wagonjwa wengi wasio na tiba.
Kwa
kweli maisha ya wanyonge yalikuwa hatarini kwani hata vifaa vya matibabu
havikuwepo na vilivyokuwepo ni vya watu maalum.
Kabla
ya Mapinduzi upatikanaji wa dawa ulikuwa ni mdogo na zaidi zilikuwa
zinapatikana kwa tabaka tawala.
Kabla
ya Mapinduzi hapakuwa na ghala maalumu la kuhifadhia dawa.
Huduma
za uchunguzi zilikuwa zinapatikana kwa kiwango cha chini na mara nyingi
zilipatikana kwa tabaka tawala pekee.
Hakukuwa
na huduma za uchunguzi kwa njia ya mionzi, ambapo kwa sasa
kuna huduma za uchunguzi kwa njia ya mionzi (X-ray, atrasound, CT scan ,MRI)
Huduma
ya matibabu ya figo haikuwepo(dialysis) , hakukuwa na gari maalum ya kubebea
wagonjwa (Ambulance), wala hakukuwa na
mtambo wa kuzalishia Oxygen kisiwani Pemba
Wakati
huo hakukuwepo na mtambo wa kuchomea taka,taka za hospitali zilikuwa zinachomwa
katika incenarator ndogo za hospitali
Kabla
ya Mapinduzi ya mwaka 64, Wizara ya Afya Pemba ilikuwa na nyumba 10 tu ambazo
zilikuwa zinaishi familia 26, nyumba hizo zilikuwepo Wete Mkoa wa Kaskazini
Pemba.
BAADA YA MAPINDUZI
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeiweka afya kama haki ya msingi ya mwananchi.
Ndani
ya miaka 62, sekta ya afya imepanuka kwa kiwango kikubwa kuanzia
miundombinu ya Afya.
Kisiwa
cha Pemba zipo hospitali 4 za ngazi ya Wilaya ikiwemo ya
Chake - Vitongoji, Hospitali ya wilaya ya Wete - Kinyasini, Hospitali ya
wilaya ya Micheweni na Hospitali ya Wilaya ya Mkoani .
Kwa
upande wa hospitali ya Mkoani hutumika kama hospitali ya rufaa kwa kisiwa cha
Pemba kutokana na huduma zinazotolewa.
Aidha,
kwa sasa Pemba kuna hospitali maalum ya matibabu ya wagonjwa wa afya ya akili
ambayo ipo Pandani na imefunguliwa rasmi tarehe 01/01/2026.
Wizara
ina jumla ya vituo afya 72 vinavyotoa huduma za afya za msingi kisiwani Pemba.
Katika
hivyo kuna dispensari 51 na health Center 21 ambazo Health center hizo zinatoa
huduma za msingi na ziada (zikiwemo za huduma za uzazi, maabara na huduma za
meno).
Aidha,
wizara inaendelea na ujenzi wa health center 6 Konde, Maziwang'ombe, Jadida,
Kiuyu Minungwini, Chonga na Mtambile.
Baada
ya kukamilika vituo hivi vitatoa huduma za matibabu yakiwemo ya wagonjwa wa
nje, wagojwa wa kulazwa.
Na
kila kituo kitakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 25 kwa wakati mmoja.
Huduma
za mama na mtoto, huduma za upasuaji mdogo (minor theater) huduma za maabara,
huduma za ultrasound na huduma za X - ray.
Kwa
upande wa madaktari bingwa (speacialist) wapo 16 ambao wote ni wazawa.
Wizara
ina madaktari MD 70 wazalendo na madaktari 8 tu ndio wakigeni, wauguzi 578
ambao wanafanyakazi katika hospitali na vituo vya afya vyote.
Upatikanaji
wa dawa ni mkubwa kwa sasa umefikia asilimia 80 ya dawa muhimu ambazo
zinatolewa bila malipo kwa wananchi wote.
Aidha
katika uboreshaji wa upatikanaji wa dawa, Wizara imejenga ghala (bohari) la
kuhifadhia dawa Vitongoji ili kuhakikisha wananchi wote wanapata dawa kwa
wakati.
Huduma
za uzazi zimeimarika na zinatolewa bure kwa wananchi wote wa mijini na vijijini
, hali hii imepelekea wananchi walio wengi kujifungulia katika vituo vya afya,
ambavyo vinapatikana katika wilaya na majimbo yote na vinafanyakazi kwa
masaa 24.
Huduma
za uchunguzi wa maabara zimeimarika kwa kiwango kikubwa, zinapatikana katika
kila Wilaya kupitia hospitali na vituo vya afya (health center).
Huduma
za x-ray zinapatikana katika hospitali za wilaya, wakati huduma za ultrasound
zipatikana katika baadhi ya vituo vya afya vinavyotoa huduma za uzazi na
hospitali zote.
Aidha,
huduma za Ct Scan na MRI zinapatikana katika hospitali ya Abdulla Mzee Pemba.
Huduma
za matibabu ya figo inapatikana kwa wakati wote katika hospitali ya Abdulla
Mzee.
Kwa
sasa Pemba ina Amblance 9 ambazo zinafanya kazi ya kubebea wagonjwa kila
wilaya.
Wizara
ya Afya imefunga mtambo wa kuzalishia Oxygen ambao upo Vitongoji kitu ambacho
kwa sasa hakuhitajiki kusafirisha mitungi ya gesi kwenda Unguja kujaza oxgen.
La
kujivunia ni kuwa gesi hiyo imeunganishwa na kitanda cha mgonjwa moja kwa moja
Kwa
sasa kuna mtambo mkubwa wa kuchomea taka zinazozalishwa katika hospitali na
vituo vya Afya vyote vya Serikali na Binafsi.
Kwa
upande wa majengo ya ghorofa yapo 7 ambayo kwa pamoja yana
uwezo wa kuchukuwa familia 120.
Katika
hizo block 4 za familia 76 zipo Abdalla mzee , block 1 ya familia 16 ipo
Kinyasini hospitali, block 1 ya familia 12 ipo hospitali ya wagonjwa wa akili
Pandani.
Wakati
block nyengine 1 ya familia 16 ipo katika hatua za umalizaji wa ujenzi hopitali
ya vitongoji.
Miongoni mwa hospitali muhimu kisiwani Pemba ni ile ya Abdalla Mzee Mkoani
ambayo ni jicho la wananchi kisiwani humo, hospitali ya vitongoji , hospitali
ya Chake, hospitali ya Wete na Micheweni.
Hii inaonesha wazi kuwa Mapinduzi hayakujenga afya mjini pekee, bali Zanzibar
nzima na wananchi wote wanafikiwa na huduma bora za matibabu.
Makamu
wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla anasema
“Mapinduzi hayawezi kuwa kamili bila kulinda uhai wa wananchi.”
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Mngereza Mzee Miraji anasema “Lengo la Mapinduzi lilikuwa kuhakikisha hakuna Mzanzibari anayekosa huduma za afya kwa sababu ya mahali alipo.”
“Kwa kweli tunao wataalamu wa afya mbalimbali wakiwemo wa upasuaji, magonjwa ya
wanawake na watoto, moyo, figo, maabara, mionzi (Radiology), usingizi
(Anesthesia) na magonjwa mengine mengi.”anasema.
Daktari wa upasuaji hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Haji Machano Mussa anasema
leo wanafanya upasuaji ambao zamani ulilazimisha wagonjwa kusafiri nje ya
Pemba.
“Haya
ni matunda ya Mapinduzi vifaa vya kisasa vya matibabu vipo”,anasifia kwa
bashasha,
Mapinduzi
ya Teknolojia ya Afya kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964 hakukuwa na CT Scan,
hakukuwa na ICU za kisasa
Maabara zilikuwa za msingi sana.
Muuguzi
wa hospitali ya Abdallah Mzee Pemba Rabia Mohamed Ussi anasema
“Vifaa vimepunguza vifo na wagonjwa wanapata huduma kwa wakati.”
Afya ya mama na mtoto mafanikio yanayoonekana kupitia sera za Mapinduzi.
Vifo vya akina mama wajawazito vimepungua kwa kiasi kikubwa, huduma za uzazi
zimeimarika,chanjo za watoto zimeenea Zanzibar nzima
SAUTI
ZA WANANCHI
Mwananchi wa Micheweni, Ali Kombo akitowa ushuhuda wa mafanikio anasema “Zamani
tulivuka bahari kwenda Unguja, leo tuna hospitali yetu tunatibiwa hapa hapa
Micheweni liwe kubwa ndo tunapelekwa Abdalla Mzee bado tuko Pemba.”
“Afya imekuwa karibu na wananchi hasa pale wanapopata matibabu katika hospitali
za karibu” anasema Fatuma Vumba wa Mwambe
Anasema
jambo la kujivunia kuona wananchi humalizia hospitali ya Abdalla mzee kwa
matibabu makubwa bila hata kwenda nje ya Unguja ama Tanzania Bara.
Khadija Ali wa Chokocho anasema “Leo tunajifungulia hospitali salama,
zamani ilikuwa hatari sana mapinduzi yameokowa maisha ya watu wengi tena walio
wanyonge.”
Sekta
ya afya imeimarishwa kupitia
Sera ya Afya Zanzibar isemayo afya kwa wote, huduma bora na nafuu, kipaumbele
kwa mama na mtoto.
Sheria ya Afya ya Umma, udhibiti wa ubora wa huduma, usalama wa
wagonjwa,usimamizi wa sekta binafsi.
Mikakati ya Kitaifa, ujenzi na ukarabati wa hospitali mafunzo ya wataalamu
ndani na nje ya nchi, ununuzi wa vifaa tiba, ushirikiano na wadau wa maendeleo.
Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar imeandika historia mpya ya sekta ya afya
kutoka hospitali moja hadi mtandao wa hospitali, vituo vya afya , kutoka
madaktari wachache hadi maelfu ya wataalamu.
Kutoka
vifaa duni hadi teknolojia ya kisasa huu ni ushindi wa Mapinduzi kwa uhai
wa Mzanzibari.
Hii si hadithi ya sifa, bali ni ushahidi wa takwimu kwamba Mapinduzi yameokoa,
yanalinda na yataendelea kulinda maisha ya wananchi wa Zanzibar.
MWISHO
Comments
Post a Comment