ZANZIBAR nayo, imebarikiwa kuwa na utamaduni wake
unaofuatwa.
Inajumuisha imani ya dini ya kiislamu, mila, desturi na
maadili mema, yatokanayo na asili na watu wa ukanda wa pwani.
Kuna mambo ambayo hujitokeza ikiwemo wigo na
kusababisha kupotea kwa utamaduni husika, hatimae kuleta mabadiliko kwa vizazi.
Utandawazi ni miongoni mwa mambo yanayosababisha kupotea
kwa utamaduni huo, na kupelekea mmong'onyoko wa maadili na kuzaliwa chungu ya
majanga.
Miongoni mwa wigo huo ni suala la kufanya tendo la
kuingiliwa kinyume na maumbile, ambalo huathiri afya ya uzazi kwa jamii.
Ingawa baadhi ya wanajamii, huona ni jambo la kawaida
bila kuzingatia athari, huku wakiyatupilia mbali makatazo ya imani ya dini na
hata sheria za nchi.
"Wake zenu ni mashamba yenu, basi waendeeni
mashambani kwenu mnavyopenda'' surat Al- Baqara (2:223) aya hii
inawaruhusu wanaume kuwaendea wake zao kwa namna wanavyopenda.
Ingawa ndani ya mipaka ya mashamba yao yaani
sehemu ya mbele ya mwanamke, amabayo ni ya uzazi na sio nyuma kama wingine
wanavyotafsiri.
Kipengele cha 154 cha 'penal code Cap. 16 (2022)
"unnatural offences" cha sheria ya Tanzania Bara kinafafanua kuwa,
yeyote anaefanya tendo la kinyume na maumbile, akitiwa hatiani adhabu ya juu ya
kifungo cha maisha au angalau miezi 30 ya kifungo.
Kwa Zanzibar kipengele cha 150 inaeleza kuwa tendo
la ngono, kinyume na maumbile (anal intercourse) ni kosa na linaadhibiwa hadi
miaka 14 ya kifungo.
Utafiti uliofanywa na Nyblade et al (2017) nchini
Tanzania unaonesha kuwa, tendo hilo hufanywa na watu wa rika tofauti, ambapo
mwanamke mmoja kati ya wanne, wanashiriki tendo la kinyume na maumbile.
Mratibu wa Tume ya Ukimwi Pemba Ali Mbarouk Omar
anasema, kibaolojia maumbile ya njia ya haja kubwa haijaumbwa kufanya tendo la
kujamiana.
Ndio maana, kunatokezea madhara ikiwemo michubuko
na kusababisha hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na magonjwa
mengine ya kujamiana.
"Njia ya haja kubwa (rectum), zimeumbwa kutoa
kinyesi na sio kuingiza jambo lolote, kama wanavyofanya baadhi ya watu kuingiza
uume, hali ambayo ni kuharibu afya ya uzazi," anasema.
Katika ufafanuzi wake anasema, mbegu za mwanaume
zinapoingia kwenye njia ya haja kubwa, husabisha muingiliano wa
homoni ambazo mara nyingi, hupelekea ulegevu wa viungo,
Jingine ni kuwa na sauti nyembama na tabia ambazo
zinazopelekea kuwa na muonekano tofauti, hivyo ikiwa ni mwanamme huwa na tabia
za kike.
Kwa kawaida njia ya tendo la kujamiana ambayo anakuwa
nayo mwanamke, hutoa utelelezi au maji ya matayarisho ya tendo la kujamiana.
Ingawa kwa njia ya haja kubwa haifanyi hivyo, kwani ina
ukavu wakati wa jimai na kuleta michubuko ya lazima.
Anasema njia ya haja kubwa ya mwanaume, hutoka
kinyesi ambacho kina vimelea vya hatari, vinavyoweza kusababisha
uambukizi njia ya mkojo, kwa anaefanya au kusabisha bawasili, kwa anaefanyiwa.
Kumbe kunaweza kusababisha saratani ya njia ya haja
kubwa au matatizo ya muda mrefu ya kutokuwa na uwezo wa kuzuia haja kubwa,
inapotokea
Madhara mingine hasa kwa wanawake ni shida ya
kujifungua, kwani pumzi (nguvu) za kusukuma mtoto zinakosekana.
"Uimara wa njia ya haja kubwa, husaidia
kuzuia pumzi ya uchungu na kusaidia njia ya uzazi ya kawaida, kufanya kazi yake
ya kusukuma mtoto kwa urahisi,"anafafanua.
Mkuu wa vituo vinavyotoa huduma na tiba kwa watu
wanaoishi na virusi vya UKIMWI, kanda ya Pemba dokta Rahila Salim Omar, anasema
kisayansi tendo la ndoa lina sehemu yake sahihi.
Kuingiliwa kinyume na maumbile, mtu hubadilika
uhalisia wake na kupelekea kupoteza uimara na misuli kulegea, hatimae
kuharibu sehemu za uzazi.
Fatma Said Mohamed ni daktari kutoka kitengo cha elimu
ya uzazi hospitali ya Abdalla Mzee, anasema kitendo hicho kinasababisha njia ya
haja kubwa kulegea.
Anaenda mbali zaidi kuwa, kila umri unaposonga, haja
kubwa hutoka bila kizuizi, humsababishia aibu na kumshushia hadhi yake mbele ya
jamii.
Afisa ustawi hospitali ya Abdalla Mzee Nasir Faki Juma,
anatilia mkazo kuwa eneo linalofanyiwa tendo hilo asili yake haliruhusiki,
kuingia kitu kutoka nje kwenda ndani.
MTAZAMO WA JAMII UKOJE
Asha Bakar Juma wa Mkoani anasema, tabia hiyo iwe kwa
mwanamke ama mwanamme haikubaliki katika jamii na huonekana hana utamaduni.
Siti Ali Hamad na Kombo Juma Ali wanasema, jamii
humuangalia vibaya na kumuondolea hadhi mtu mwenye tabia ya kufanya tendo hilo
kinyume na maumbile.
Asma Juma Hamad (sio jina lake halisi) anasema
baadhi ya wasichana hutumia njia hii ya kujamiana kama ni njia ya kulinda
usichana wao (bikira) au hata kukwepa ujauzito.
"Kwa sasa jamii imeona tendo la kujamiana
kinyume na maumbile ni jambo la kawaida, kwani wapo wanandoa wengi
hufanya tendo hili kwa kuridhishana, hata kama wanajua ni kosa,''anasema.
SABABU YA MATENDO HAYO NI IPI?
Ali Mbarouk Mratibu wa Tume ya UKIMWI Pemba
anasema zipo sababu za kimaumbile, kibaologia na za kishetani
zinazosababisha matendo ya kujamiana kinyume na maumbile.
Anasema sababu za kibaologia kwenye nasaba au maumbile
ya kibauologia na mchanganyiko wa homoni na vinasaba, inawezekana
kusababisha mtu kuwa na hisia au maumbile tofauti kidogo na jinsia yake.
Ingawa mienendo ya tabia za jimai inaeleza kwamba, hii
haishawishi mtu kufanya tendo la kujamiana kinyume na maumbile.
Kwa sababu za mabadiliko ama mchanganyiko wa
chembe nasaba ( DNA na vichocheo vya homoni.
Aidha mwanamme anaweza kuwa na tabia za kike sauti,
mwendo, ishara, tabia, hulka na hata maono ama mwanamke anaweza kuwa na mabadiliko,
muonekano, sauti, tabia, ndevu, hulka na silka za kiume.
Hoja hizi zinapingwa ama kuungwa mkono na wanatabia
(behaviorists) kwa kusema, tabia ya kufanya au kufanywa tendo la jimai kinyume
na maumbile, ni tabia ya mtu.
Na aidha ikiwezekana kuchochewa na homoni ama kuchochewa
na tabia za kibinadamu za tamaa, ushawishi, wigo au hisia za kimwili.
DINI INASEMAJE
Sheikh Said Abdalla Nassor kutoka Ofisi ya Mufti Pemba
anasema suala la kufanya tendo kinyume na maumbile, kwa dini ya kiislamu halikubaliki.
Anafahamisha, kutokana na kukatazwa katika dini tendo
hilo linachangia madhara makubwa, ikiwemo kupata adhabu ya Allah,
kukosa barka, kuondoshewa nuru katika maisha ya duniani na ya akhera.
"Mtume Muhammad, amabe ni kiongozi wetu anasema analaaniwa
anaemuendea mwanammke kinyume na maumbile na siku zake za afya,''anasema.
Mchungaji wa kanisa la 'TAG' Makangale na mwangalizi
kwa upande wa Pemba Samwel Elias Maganga, anasema kufanya tendo la kinyume na
maumbile, halikubaliki.
Anaelezea bibilia kitabu cha walawi mlango wa 18 mstari
wa 22 hadi 23 inasema 'usilale na mwanamme mfano wa kulala na mwanamke ni
machukizo wala usilale na mnyama yoyote ili kujitia najisi kwake, wala mwanamke
asisimame mbele ya mnyama ili kulala nae ni uchafu'.
Nyaraka na ripoti mbalimbali zenye uzito wa sharia na
kidini ikiwemo ile ya Islam Q &A ,Islam web zimeelezea wazi kwamba
tendo la jimai kinyume na maumbile kuwa ni haramu.
Akitowa ushuhuda Fatma Kombo Juma (jina sio sahihi)
baada ya mume kumuingilia kinyume na maumbile na hatimae kupata athari athari
wakati wa kujifungua.
Mwingine ambae alikataa jina lakw kupishwa, aliyeolewa
na kuishi na mume wake Dar-es Salaam amepoteza watoto wawili, kwa kukosa pumzi
za kusukuma wakati wa kujifungua.
Mwenyekiti wa jumuiya ya watu wanaoishi na virusi vya
ukimwi VVU ZAPHA+ Wilaya ya Chakechake Maryam Said Abdalla anasema,
sio busara jamii kuendelea kufanya jambo linalowaletea madhara .
Anaitaka jamii kuacha tabia hiyo, kwani inawapa hitilafu
katika mfumo mzima wa uzazi, huku akiwaambia wale ambao wameshakomaa na jambo
hilo, wanaweza kupata ushauri wa taalamu na kucha kabisa.
Wanaharakati wa haki za binadamu, pamoja na
mashirika kama Human Rights Watch , Amnesty International , Human Dignity
Trust na LGBT Voice of Tanzania wanakataa kabisa matumizi ya jimai
isiyo ya kawaida.
Chama cha waaandishi wa habari Tanzania Zanzibar imekuwa
mstari wa mbele katika kutowa elimu juu ya unyanyasaji wa
kijinsia, uzazi, mimba na matumizi ya vyombo vya habari kufikisha ujumbe
kwa umma.
Mkurugenzi wao dk. Mzuri Issa anasema chama hicho
kimekuwa na ushawishi mkubwa katika mawasiliano ya kijamii
kuhusu afya , haki za wanawake na ukatili wa kijinsia.
Mkakati wa wizara ya Afya ni pamoja na kutoa
huduma bora , salama na za heshima kwa watu wote huku
ikihakikisha kuondoa ubaguzi, unyanyasaji na ukandamizaji.
Huku malengo yakiwa ni kuboresha upatikanaji
wa huduma za afya za uzazi ,akili kwa jamii ya LGBTQ kukuza elimu na
uelewa wa haki za binadamu miongoni mwa wafanayakazi wa afya
na jamii .
Mwisho .
Comments
Post a Comment