NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@
WANANCHI
wa kijiji cha Tundaua shehia ya Kilindi wilaya ya Chake chake, wamesema
hawakatai uwekezaji katika maeneo yao, wanachotaka ni kushirikishwa kila hatua,
kuelekea uwekezaji huo.
Walisema,
kwa sasa wamekuwa wakiona uwekaji wa vikuta ‘bacons’ pembezoni mwa bahari,
ndani ya maeneo wanayolima mihogo, mpunga na mboga mboga, bila ya taarifa yoyote
kutoka serikalini.
Wakizungumza
na waandishi wa habari, kufuatia uwepo wa vikuta hivyo, kwenye eneo
wanaloendesha kilimo, walisema kinachowasikitisha ni kukosa taarifa, juu ya aina ya uwekezaji huo.
Walieleza kuwa,
hawajapata taarifa kutoka kwa sheha wao, wala kiongozi mwingine yoyote, na
kuwaacha njia panda juu ya zoezi ambalo, limeshakamilika la uwekaji wa vikuta.
Mmoja kati
ya wananchi hao Makame Haji Makame, alisema ingawa wao hawajakwenda kulalamikia jambo hilo kwa sheha wao, lakini na yeye hajaita kuwapa taarifa zozote.
Alisema kama
ni suala la uwekazaji, walifikiria kuwa, wengeitwa kwenye kikao maalum, na
kuelezwa kwa kina, juu ya kinachotakwa kufanywa, katika eneo hilo kwa vile wanayo haki hiyo.
‘’Sheha
ametupuuza kwa kutotupa taarifa, sisi tunaona harakati za upimaji na uwekaji wa
vikuta tu, pembezoni mwa bahari na maeneo tunayoendesha kilimo,’’alilalamika.
Nae Mohamed Kassim
Soud, alisema wao hawana shaka na uwekezaji unaotaka kufanyika, ila
kilichowakera ni kutoshirikishwa na kuzarauliwa.
‘’Maeneo
haya kwa zaidi ya miaka 60 sasa, tunaendesha kilimo, sasa tunapoona uwekaji wa
vikuta na sisi kukoseshwa taarifa, huwa hatujisikii vizuri,’’alieleza.
Aidha
mwananchi huyo, alisema kama hiyo ni amri ya Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali
Mwinyi, binafsi amekuwa na utaratibu mzuri wa kukutana na wananchi, kabla ya kuendelea
na jambo jingine lolote,’’alifafanua.
Alifahamisha
kuwa, alitarajia washirikishwe kikamilifu tokea hatua za awali, ili watoe maoni yao juu ya aina ya uwekezaji wenye
tija, hasa kutokana na mila na desturi zao.
‘’Engekuwa
vyema tukashirikishwa na kutoa maoni yetu, ili kujua kunataka kujengwa chuo,
skuli, hospitali au hoteli ili kuwa na ushirikiano na anayekuja,’’alipendekeza.
Kwa upande
wake Mohamed Haji Juma, alisema kinachoendelea hawana taarifa nacho, wanachoshuhudia
ni gari kupita kila siku kijijini hapo, na kuelekea eneo hilo.
Alikri kuwa,
wao hawajamfika sheha wao, juu ya kumuulizia kinachoendelea, ingawa wamejaa na
hofu juu ya aina ya mwekezaji na uwekezaji, unaokuja kijijini kwao.
Mwananchi
Khamis Makame Hamad, alisema ameanza kupatwa na wasisi kwani, eneo hilo kwa
zaidi ya miaka 40 analitumia kwa kilimo cha mpunga.
‘’Nimekuwa
nikilima hata bamia na mboga mboga nyingine, na sasa kufuatia vikuta vilivyowekwa na
watu nisiowafahamu, najihisi nimeshany’ang’wa eneo hilo,’’alilamika.
Nassor Mwadini
Khatib, alisema kuwa pamoja na kwamba eneo hilo ni la serikali, walikabidhiwa wao
kwa ajili ya kulishughulikiwa, ingawa kwa sasa, limevamiwa na mtu wasiemfahamu wala kuwa na taarifa nae.
‘’Sisi ndio
walinzi wa shamba hilo, na tulitarajia kama serikali inalitaka shamba lake, ije
ikutane na sisi na sio kuanza kutiwa vikuta bila ya taarifa, hapa hatukutendewa haki,’’alifafanua.
Khari Bijuma
Makame, alisema hofu yake, pindi eneo hilo la usawa wa bahari litachukuliwa na
mwekezaji, ni kupoteza uhifadhi wa habari, ambao kila miezi mitatu, huvua kwa pamoja.
‘’Eeno hilo ni la hifadhi, wakati ukifikia wa kufunguliwa, kinachopatikana (fedha), hugawa baina ya
mvuvi na jamii, na fedha kuziingiza kwenye ujenzi wa miradi ya jamii kama skuli,’’alieleza.
Tatu Khamis
Hamad, alisema eneo hilo lenye idadi kubwa ya minazi, amekuwa na utaratibu wa
kuokota makuti makavu, na kisha kuyasuka na kuyauza, ili kuendesha maisha yake.
‘’Sasa kama
kwaja uwekezaji, je mzungu ataturhusu kuingia ndani ya eneo hilo na kuokota
makuti, na kuendesha familia zetu,’’alihoji.
Nae Hadia
Makame Ali, alisema hofu yake ni kujengwa hoteli ya kitalii, na kuwa kichochezi
ya uvinjifu wa mila, tamaduni na silka zoa.
Mapema sheha
wa Kilindi Nassor Mohamed Khamis, aliwataka wananchi hao, kuwa watulivu, na
wakati ukifika wataelezwa kila kitu na mwekezaji mwenyewe.
Alisema, kwa
sasa bado ni mapema kujua panataka kujengwa nini, kwani mwekezaji huyo, alikuwa
hajamaliza taratibu za umiliki wa eneo hilo.
Sheha huyo
alieleza kuwa, serikali wala haina nia mbaya na wananchi wake, na haiwezi
kuweka ukezaji ambao utakuwa kinyume na maadili ya wananchi, wa Kilindi na Tundaua yake.
Wakati huo
huo sheha huyo, aliwaahidi wananchi hao kuwa, hakuna hata mmoja, atakaeharibiwa
kipando chake na kukosa kulipwa fidia.
‘’Juzi Novemba
17, wananchi wameanza kuitwa na mwekezaji huyo, ili kuzungumza nao, juu ya
hatma yao katika eneo hilo la serikali, ambalo limeshauzwa kwa mwekezaji,’’alifafanua.
Katika hatua
nyingine sheha huyo, alisema kila mwananchi ambae atakosa eneo la kilimo hapo
baadae, afike ofisini kwake, kwa ajili ya kupewa eneo jingine.
‘’Ardhi ni
mali ya serikali, hivyo ndani ya shehia ya Kilindi hakuna mwananchi anaetaka kuendesha
kilimo akakosa, afike ofisini kwangu, kwa ajili ya kupewa maelekezo,’’alisisitiza.
Eneo hilo la
serikali, kwa sasa linaminazi kadhaa ya serikali, ambapo kwa zaidi ya miaka 60
iliyopita, lipo chini ya wananchi kwa ulinzi na utaratibu na kisha kukodishwa.
Wapo wakulima zaidi ya saba, wanaoendesha
vilimo vya aina mbali mbali, kama vile mpunga, mihogo, mabamia na mboga
nyingine.
Mwisho
Comments
Post a Comment