NA OMAR HASSAN, PEMBA@@@@
KAMISHAN wa Polisi Zanzibar CP. HAMAD KHAMIS HAMAD amewataka Wakaguzi wa Shehia na Watendajiwa Madawati ya Jinsia na Watoto kuweka mikakati itakayoishirikisha jamii kubaini na kuzuwia uhalifu ikiwemo vitendo vya udhalilishaji ili jamii ibaki salama.
Akizungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Mikoa ya Kaskazini na Kusini Pemba huko Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete amesema watendaji wa Polisi wanafanya kazi kubwa ya kutoa elimu kwa jamii lakini bado makosa yanaendelea kufanywa hivyo ametoa rai ya kufanya kwa kufanya tathmini sambamba na kuishawishi jamii kutekeleza wajibu wao wa kushiriki katika kujiwekea ulinzi.
Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP WILLIAM MWAMPAGHALE amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba limejipanga kuweka ulinzi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Skuu ya Idd El Adh-ha.
Comments
Post a Comment