SIKU YA MTOTO WA AFRIKA, FAMILIA ZIWAPE UHURU WA KUCHEZA WATOTO WENYE ULEMAVU KUWAFUNGIA NI KUDIDIMIZA VIPAJI VYAO
NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
SIKU ya mtoto wa Afrika, ni siku maalum inayoadhimishwa kila
mwaka, kwa lengo la kujenga ufahamu na kuongeza juhudi za kuimarisha hali ya
watoto barani Afrika.
Ambapo kilele cha siku hii, iliadhimishwa Juni 16 ya kila mwaka,
kwa lengo la kuwakutanisha watoto, kujadili mafanikio na changamoto zao.
Siku hii, inaanzia pale mwaka 1991, wakati wa mkutano wa kwanza
wa baraza la mawaziri wa Umoja wa nchi za Afrika (OAU).
Ulifanyika nchini Cairo Misri, ambapo katika mkutano huo, baraza
la mawaziri, lilipendekeza kuanzishwa kwa siku ya maalum ya mtoto wa Afrika.
Ukitaka kuiweka haki na ustawi wa watoto, kwenye ajenda ya
kisiasa, kiutamaduni na kijamii barani Afrika.
Ndipo hapo,
ilipozaliwa Juni16 ya kila mwaka, iwe ni siku ya mtoto wa Afrika, kutokana na
tukio la kusikitisha lililotokea mwaka 1976, Soweto nchini Afrika Kusini.
Siku hiyo, taarifa zinaeleza kuwa, maelfu ya
wanafunzi wa skuli za upili, walijitokeza kuandamana kupinga ubaguzi wa rangi
katika elimu.
Kisha Jeshi la
Polisi nchini humo, liliwakabili kwa ukatili, na maandamano hayo, yalisababisha
vifo vya watoto wengi.
Tukio hilo lilikuwa ni ishara na azma ya
kupigania haki na ustawi wa watoto barani Afrika, na tarehe hiyo ikachukuliwa
kama ishara ya kutambua mapambano yao.
Sasa kupitia siku
ya mtoto wa Afrika, serikali, mashirika ya kijamii, na wadau wingine,
wanajitahidi kuongeza ufahamu juu ya masuala yanayowakabili watoto barani
Afrika.
Zanzibar nayo kama
sehemu ya duniani, kila mwaka tarehe 16 Juni, huugana na nchi nyingine za Afrika,
kuadhimisha siku hiyo.
Ambapo chimbuko la maadhimisho
haya, ni Azimio lililopitishwa na uliokuwa Umoja wa nchi huru za Afrika (OAU)
mwaka 1990.
Kwa lengo la
kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini, waliouawa
tarehe 16 Juni, 1976 kutokana na ubaguzi wa rangi.
Watoto hao,
walikuwa wakidai haki zao za kutobaguliwa, pamoja na haki nyingine za
kibinadamu, ikiwemo haki ya kupata elimu bora.
Leo Zanzibar, tukiadhimisha
siku ya mtoto wa Afrika, ikiwa ni miaka 46 imeshapita, bado kundi kundi la
watoto wa kike hasa wenye ulemavu, wanaendelea kunyima haki zao.
Maana Mkurugenzi wa
Jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Chake chake Pemba ‘CHAPO’ Nassor
Bilali Ali, anasema watoto wa kike wenye ulemavu, wanayohaki ya kupewa uhuru wa
kucheza, michezo waipendayo.
‘’Kwa mfano watoto wa
kike wenye ulemavu, huwaoni wakicheza michezo ambayo wanaweza kuibuliwa vipaji
na kisha kujiajiri, jambo linalokumbusha mateso ya Soweto,’’anasema.
Khalfan Amour Mohamed,
Mratibu wa Jumuiya kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa akili, anasema bado
mateso ya Soweto, yapo ndani ya jamii, kwa kule kuwafungia watoto wenye ulemavu
wa akili ndani.
Wakati Zanzibar,
ikiungana na matifa mingine, katika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika, ni
lazima minyororo iliyofungiwa watoto wa kike wenye ulemavu, ili wasishiriki michezo waipendayo, ikatwe.
‘’Leo watoto wa
kike wenye ulemavu huwaoni kwenye michezo ya riadha, kuogelea, kuendesha baiskeli,
mpira wa kikapu, mikono na wamefungiwa ndani,’’anasema.
Mratibu wa Chama
cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar ofisi ya Pemba Fat-hya
Mussa Said, anasema bado watoto wa kike wenye ulemavu, hawajatekelezewa haki
zao.
‘’Badhi ya nchi
tena za Afrika, unawakuta wanashirikishwa kwenye michezo kama ya mpira wa mikono,
meza, kikapu, riadha na kurusha tufe, lakini hapa kwetu wamefungiwa,’’analalamika.
Anasema pamoja na
ujio wa mradi maalum ambao utawawezesha waandishi kuibua changamoto hizo,
lakini jamii iamke na iwashirikishe watoto wa kile, katika michezo waipendayo.
Mrajisi wa vyama
vya michezo Zanzibar Abubakar Mohamed Lunda, anasema, pamoja na kutokuwepo kwa
mipango thabiti kwa watoto wa kike wenye ulemavu kushiriki michezo, lakini
ndani ya jamii hakuna uwelewa.
‘’Leo
tunasherehekea siku ya mtoto wa Afrika, lakini hatuna miundombinu imara ya
mtoto wa kike mwenye ulemavu kushirikia michezo’,’alinukuliwa akisema.
Afisa Mradi wa kukuza usawa wa kijinsia na ujumuishi
kwenye michezo, Khairat Haji anasema Chama cha Waandishi wa Habari
Wanawake Tanzania-TAMWA- Zanzibar, anasema wameona ipo haja ya kushirikiana na vyombo vya habari, kuibua changamotio za
aina hiyo.
‘’Lengo ni kuondoa mifume dume na yale mawazo mgando ambayo
ni vikwazo dhidi ya wanawake kushiriki katika michezo, kupitia mradi wa michezo
kwa maendeleo unaodhaminiwa na shirika la Ujerumani (GIZ),’’anasema.
WAZAZI
Khadiha Omar Haji
wa Wawi, anakiri kuwa, kutokana na miundombinui kutokuwa rafiki, ni kweli
wanalazimika kuwafungia ndani watoto wa kike kutoshiriki michezo.
‘’Kwanza huoni hata
viwanja kwa ajili yao, vifaa ghali, uwelewa baadhi ya wazazi uko chini, haya yanachangia
kudidimiza vipaji vyao,’’anasema.
Khamis Shehe Khamis
wa Madungu, anasema watoto wa kike na hasa wenye ulemavu, imekuwa ni shida
kuwashirikisha kwenye michezo, kutokana na mazingira.
‘’Kwanza hakuna
viwanja ambavyo ni rafiki kwao, lakini ushajiishaji serikalini haupo wa kutosha,
sasa haya yanachangia waendelee kukaa ndani,’’anasema.
WATOTO WENYEWE
Asma Maulid Khamis
wa Mtoni Chake chake, anasema taasisi za michezo hazijakuwa tayari kuwatoa nje,
kwa ajili ya kushiriki michezo waipendayo.
‘’Mbona kuna ligi
ya mpira wa miguu, kikapo, mikono lakini hakuna hata mchezo mmoja, uliosajiliwa
na kutangaazwa kwa ajili ya wanawake wenye ulemavu,’’anaeleza.
Khadija Rashid Issa
wa Kengeja Mkoani, anasema jamii sio ya kulaumiwa kwa wao kutoshirikishwa
michezo, bali sera na mikakati iliyopo imewatenga.
‘’Kuanzia skuli hadi
vyuo vikuu, lazima ushirikishwaji nzuri kwetu sisi wanawake wenye ulemavu
kushiriki michezo, sasa familia inatumaliza tu,’’anaeleza.
WIZARA HUSIKA YA MICHEZO
Kaimu Mratib wa Idara ya Utamaduni na Michezo Pemba, Khamis
Hamad Juma, anasema haijawahi kutokeza hata mwaka mmoja, kuwepo kwa mashindano
maalum ya mchezo wa aina yoyote kwa watoto wa kike wenye ulemavu.
‘’Hata bonanza la michezo ambalo ni maalum kwa ajili ya
watoto wa kike wenye ulemavu, sijawahi kuliona wala kusikia,’’anafafanua.
Baraza
limevisaidia vyama vitatu (3) vya michezo ya watu wenye ulemavu, katika kuandaa
na kushiriki mashindano kadhaa, yakiwemo taifa ya michezo ya watu wenye ulemavu
wa akili yaliyofanyika mwaka 20202.
Hayo yamefahamika
wakati Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita,
akisoma bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023.
Akasema Zanzibar,
ilifanikiwa kupata medali 20 zikiwemo dhahabu nane, fedha moja, na shaba11,
katika michezo tofauti, kupitia timu za watu wetu wenye ulemavu wa akili.
Waziri Tabia
anasema, kwenye michezo ya watu wenye ulemavu wa mguu na mkono mmoja, wizara
imelisaidia Shirikisho la mchezo huo, na kushiriki mashindano ya kitaifa
yaliyofanyika Arusha.
Lakini pia shirikisho
la michezo ya viziwi Zanzibar (SHIMIVIZA), anasema limesaidiwa kuandaa bonanza
kwa ajili ya shamra shamra ya kuadhimisha siku ya viziwi duniani.
Katika eneo
jingine, moja ya vipaumbele vya mwaka wa fedha wa 2023/2024, ilikuwa ni kuimarisha
na kuendeleza miundombinu ya michezo, kwa kufanya ukarabati mkubwa wa uwanja wa
michezo wa Amaan na Gombani na kujenga viwanja vya michezo vya kisasa kwa kila wilaya.
Mwisho
Comments
Post a Comment