NA OMAR HASSAN, ZANZIBAR@@@
Kamishna wa Polisi Zanzibar CP HAMAD KHAMIS HAMAD amewataka watendaji wa Baraza la Sanaa Sensa ya Filamu na Utamaduni kufuata sheria katika kutekeleza majukumu yao na wasitoe vibali vya kupiga muziki kwa watu wasiokuwa na sifa ili kuondoa kero kwa wananchi zinazosababishwa na wapiga muziki.
Akizungumza na Viongozi wa Baraza hilo ambao wameteuliwa hivi karibuni, waliofika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kujitambulisha, CP HAMAD amewataka kuwachukulia hatua bila ya kuwaonea muhali wanaokiuka sheria ili wananchi waendelee kuwa na Imani na Serikali yao kakika kuwaondolea kero.
Nae Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Sensa ya Filamu na Utamaduni JUMA CHOUM JUMA ameliomba Jeshi la Polisi kuendelea kushirikiana nao ili kufanikisha kazi za Baraza hilo.
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi Jamii Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP JONAS MAHANGA amelihimiza Baraza la Sanaa kuwasimamia wasanii kutoa maudhui yenye maadili na kuhamasisha Uzalendo.
MWISHO
Comments
Post a Comment