NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
NAIBU Katibu mkuu wizara ya Nchi, Afisi
ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Omar Haji Gora
amewakumbusha watunza kumbu kumbu wa tasisi za serikali, kuwa, roho ya wizara
ya ni sehemu za masjali.
Naibu Katibu
mkuu huyo, aliyasema hayo, kwa nyakati tofauti wakati akiyafungua mafunzo ya
siku mbili, kwa makatibu muhutasi na watunza kumbu kumbu za serikali, kisiwani
Pemba.
Akizungumza
na watunza kumbu kumbu hao, kwenye mafunzo yaliyofanyika ukumbi wa wizara ya
Fedh Gombani, alisema masjali ndio eneo nyeti pekee, katika kila wizara.
Alieleza
kuwa, ofisi hiyo ndiyo inayotegemewa na wafanyakazi wote, kwa kuhifadhi kumbu
kumbu zao mbali mbali, kama vile barua za ajira.
Naibu Katibu
mkuu huyo, alisema masjali sio sehemu ya kuwekwa ovyo ovyo, na inatakiwa
kuangaliwa kwa macho zaidi ya mawili, kwani ni eneo la kutunzia haki za
wafanyakazi.
‘’Msipokuwa
makini kwenye masjali, mnaweza kumsababishia mfanyakazi, ugonjwa, maradhi na
hatimae kifo, ikiwa mtaipoteza moja ya kumbu kumbu zake muhimu,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine, Naibu Katibu Mkuu huyo, alisema ni kosa kisheria kwa mtumishi wa eneo
la masjala, kutoa siri ya mtumishi mwenzake.
‘’Kwa mfano
kuna barua za uteuzi, kusimamishwa kazi, kuhamishiwa eneo jingine, kuzuiliwa
kwa ruhusa au kuomba mkopo, hapa wapo wanaotoa nje siri hizi,’’alieleza.
Akizungumza
kwenye mafunzo kama hayo, yaliofanyika ukumbi wa Baraza la mji Chake chake kwa
Makatibu muhtasi, Naibu Katibu mkuu huyo, aliwataka kuwa na lugha mzuri.
Alieleza
kuwa, moja ya jambo kubwa ambao waliowengi wanashindwa kulifaulu ni matumizi ya
lugha sahihi, kivazi na utunzaji siri.
‘’Mafunzo
haya na mengine yanayosimamiwa na Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar ‘IPA’ ni
sehemu ya kukumbushana majukumu yetu sisi watumishi wa umma,’’alieleza.
Mapema Afisa
Mdhamini wa wizara hiyo Pemba, Halima Khamis Ali, alisema anatarajia kuona
mabadiliko kwa watunza kumbu kumbu na makatibu muhtasi serikalini.
Alisema
kumekuwa na kilio kikubwa, kuanzia kwa watumishi wa umma na wananchi wanaofuata
huduma, juu ya kutopokelewa vizuri na watumishi wa kada hizo.
‘’Baada ya
mafunzo haya na mengine, tutakuwa tunafuatilia kuona ikiwa kuna mabadiliko,
maana haiwezekani kwa mtumishi wa umma, kuwa na kiburi,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine Afisa Mdhamini huyo, aliwataka watunza kumbu kumbu hao, kuwaeleze
wakuu wao wa tasisi, juu ya mafunzo hayo, katika eneo la mabadiliko ya
kiutendaji.
Kaimu
Mkurugenzi wa Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar ‘IPA’ Bakari Khamis Muhidini,
alisema chuo kitaendelea kuwanao watumishi wa kada zote.
Alieleza
kuwa, mafunzo haya sio ya mwanzo, kwani wapo watumishi wengine wakiwemo
waalimu, wameshapewa kwa mujibu wa majukumu yao.
‘’IPA
imekusudia kuyafanyiakazi, maono ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, la kuwataka wafanyakazi wa serikali kutofanyakazi kwa
mazoea,’’alieleza.
Akiwasilisha
mada ya maadili kwa watunza kumbu kumbu, afisa kutoka ‘IPA’ Hassan Juma Issa,
alisema kanuni ya Utumishi wa umma ya mwaka 2014, inakataza kutoa siri za
serikali.
Alieleza
kuwa, masjala ndio roho ya taasisi, hivyo mtendaji wa eneo hilo, hutakiwa kuwa kioo
kwa watumishi wenzake na jamii kwa ujumla.
Nae mtoa
mada kutoka ‘IPA’ Mzee Juma Haji, alisema mfumo salama wa upangaji majalada,
ndio njia sahihi ya upatikanaji wa taarifa kwa haraka za mtumishi.
‘’Mtendaji
wa masjala kama asipokuwa makini na kutozingatia utaratibu unaotakiwa, anaweza
kuwa msumbufu wakati wa uhitaji wa taarifa husika,’’alifafanua.
Baadhi ya
washiriki wa mafunzo hayo, wamesema hawana shida ya kutunza kumbu kumbu kama
inavyotakiwa, ingawa shida ni baadhi ya wakuu wa tasisi huwalazimisha kupinda
sheria.
Mwisho
Comments
Post a Comment