IMEANDIKWA NA ZUHURA
JUMA, PEMBA@@@@
WAZEE wa
shehia ya Majenzi Wilaya ya Micheweni Pemba wamesema, iwapo wazazi wa watoto
wanaozaliwa miaka ya sasa wanafuata utaratibu wao waliokuwa wakuwapikia vyakula vya lishe, wangekuwa na nguvu pamoja na afya bora.
Walisema kuwa, mambo mengi ya zamani yameachwa kutekezwa hali
ambayo inasababisha madhara kwao, hivyo ni vyema wakafuata utaratibu waliokuwa
wakitumia wao zamani kwa lengo la kujenga afya bora ya mtoto.
Walisema kuwa, utamaduni wao wa malezi ya watoto wachanga
waliokuwa wakiufuata uliwajenga sana watoto wao kwa kupata nguvu sambamba na
kuepukana na husda pamoja vijicho.
‘’Maisha ya sasa kila kitu watu hawakitaki, utasikia mtoto
mchanga ana gesi, mbona sisi zamani walikuwa watoto wetu hawaumwi ovyo na
walikuwa na nguvu’’, awalisema wazee hao.
Hamad Mbwana Shaame mkaazi wa shehia hiyo alisema kuwa,
kutokana na utamaduni wao wa Micheweni, mtoto anapofikia siku saba tu alikuwa
anapikiwa kibwabwa au papai na kurambishwa, ili kukua vizuri, kupata nguvu na
afya bora.
‘’Anaanza kwa kurambishwa na kila akikuwa inakuja hatua
nyengine ya kulishwa, hivyo kipindi hicho watoto walikuwa hawapati maradhi kiholela’’,
alifahamisha.
Alisema kuwa, kibwabwa hicho kinapikwa kwa unga wa mchele na
sukari na unakuwa ni laini sana, huku anasubiriwa mtoto kukua na kupikiwa uji
wa mtama na uwele, jambo ambalo kwa wazazi wa sasa hawaliendelezi.
Kwa upande wake Saada Said Kombo alisema, utamaduni wao
ilikuwa wanatafuta chochoni na kuzitengeneza vizuri na badala yake wanaanika na
kuzitwanga kwa ajili ya kupata unga, hivyo mtoto anapofika siku saba baada ya
kuzaliwa, unachanganywa na sukari kidogo na kurambishwa mara tatu.
‘’Unga wa chochoni ni mzuri kwa sababu ni dawa, kwani mtoto
ilikuwa sio rahisi kupata kijicho ama husda na pia ilikuwa hapati magonjwa ya mara
kwa mara kama watoto wa sasa ikiwemo gesi’’, alisema bibi huyo.
Alisema kuwa, wazazi wa sasa wanasema chochoni zina sumu na
ndio hawawapi watoto wao, jambo ambalo sio kweli kwa sababu wao walikuwa
wanautengeneza vizuri na kuwapa watoto wao na wala hakuna aliekufa.
‘’Tulikuwa tunaziroweka siku tatu na kila siku tunamwaga maji
na tunaingiza mengine, sasa faida ya chochoni kwanza inajenga mwili, kitu cha
pili ni fungo la mwili kwani mtoto hapatwi na ubaya’’, alieleza.
Nae Sharifu Massoud Hamad alisema kuwa, watoto wengi wanaozaliwa
miaka ya sasa wengi wao wanakumbwa na magonjwa mbali mbali kutokana na
kuwalisha watoto vyakula ambavyo havistahiki kupewa.
Sheha wa Shehia hiyo Faki Kombo Hamad alisema kuwa, vyakula
hivyo walipikiwa wao na wazazi wao walipokuwa wachanga, ingawa kwa sasa wanaambiwa
kuwa mtoto hatakiwi kupuewa kitu chochote mpaka afikie miezi sita.
MWISHO.
Comments
Post a Comment