Na Nusra Shaaban, Unguja;
Viongozi
hao kutoka vyama
vinne vya siasa Zanzibar kama
vile Chama cha mapinduzi CCM, Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA, ACT
Wazalendo pamoja na Chama cha wananchi CUF wamejumuika kwa pamoja huko katika chuo cha
utawala wa umma (IPA) kilichopo Tunguu Wilaya ya kati Unguja.
Awali Ikumbukwe kwamba mwaka
wa 2022 viongozi hao walipatiwa
mafunzo na Jumuiya ya
Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) kwa kushirikiana na Konrad
Adenauer Stiftung (KAS) katika utekelezaji wa mradi wa “amani yetu
mshikamano wetu” unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU).
Lengo la kujumuika kwa viongozi hao ni
kuendelea kuhubiri amani ya nchi kwa kutoa mafunzo ya kudumisha amani kwa
wanafunzi hao hasa ikizingatiwa kwamba wao ndio viongozi wa kesho.
Akizungumza
wakati akitoa mafunzo hayo Mjumbe kikosi
kazi cha ng’ome ya wanawake Taifa ACT Wazalendo bi Halima Ibrahim alisema
wanafunzi hao ndio viongozi watarajiwa hivyo wanapaswa kutambua namna
watakavyoendelea kuidumisha amani kwa kutumia elimu yao.
Katibu Mkoa
wa Mjini magharibi kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA bi Huzaima
Ali Hamdan alizungumzia umuhimu wa
kutatua migogoro ikiwa ni njia moja wapo ya kuendelea kudumisha amani ya nchini.
Nae Mjumbe
wa Chama cha mapinduzi CCM Nahla Adul
Halim alisema bila ya amani hakuna
maendeleo hivyo wanafunzi hao wanakila sababu ya kuhakikisha kwamba amani ya nchi inaendelea kudumu.
Hasina Ali Matar, Mkurugenzi wa mipango na uchaguzi kutoka chama
cha wananchi CUF alisema wanafunzi hao
wana nafasi ya kusaidia usuluhishi kwa kuwa wazalendo wa kuipenda nchi yao na kuamini katika mashirikiano ya ujenzi wa
Taifa moja .
Wanafunzi
mbalimbali waliopatiwa mafunzo hayo akiwemo Rais kutoka serikali ya
wanafunzi ndugu Nassir Mussa wametoa
shukrani zao kwa kuwapongeza viongozi hao kwa kuwapatia
mafunzo ya kudumisha amani na kuahidi kuwa mstari wa mbele katika kujenga
amani ya nchi kwa kuanzia na utatuzi wa migogoro katika ngazi ya
Uongzozi wa serikali ya wanafunzi.
Comments
Post a Comment