Skip to main content

TAMWA, INTERNEWS NGUVU MOJA KUTAKA SHERIA MPYA YA HABARI ZANZIBAR

 



NA HAJI NASSOR, PEMBA:::


‘’BILA ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi’’.

‘’Tena pia mtu huyo ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati, na rai anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio ya nchini na duniani kote, ambayo ni muhumi kwa maisha yake’’.

Ndivyo Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, inavyoelekeza kifungu cha 18 juu ya upatikanaji na utoaji wa habari kwa raia, tena bila ya kujali mipaka ya nchi.

Mwanasheria wa kujitegemea Khalfan Amour Mohamed, anasema suala la kupata habari, au kutoa ni haki ya kikatiba, ambayo inatofautiana na haki nyingine.

‘’Ukitaka kuzigawa haki hizi, basi zipo haki za kikatiba na haki nyingine zilizotengenezewa sheria yake mbali mbali, mfano haki ya elimu,’’anafafanua.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwajali wananchi wake, haikuishia tu ndani ya Katiba kifungu cha 18 ya upatikanaji wa habari, bali kwa kutambua umuhimu huo, ilianzisha sheria maalum.

Ikumbukwe kuwa, miundombinu ya kupashana habari ni Magazeti, redio na tv, ingawa na kwa sasa kumeibuka mitandao ya kijamii.

Kwa Zanzibar, vyombo vya habari vya magazeti vinasimamiwa na sheria ya Magazeti, Vitabu, na Mawakala wa Habari nambari 5 ya mwaka 1988.



Igawa kwa redio na tv na hata sasa uwepo wa vyombo vya habari mtandaoni, vyenyewe vinasimamiwa na sheria ya Tume ya Utangaazaji Zanzibar nambari 7 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake.

SHERIA YA MAGAZETI, VITABU NA MAWAKALA WA HABARI NO 5, 1988

Sheria hii yenye vifungu 81 na sehem 10, sasa inatimiza miaka 34, tokea kutungwa kwake, na kwa maana nyingine, vipo vifungu zaidi ya 40 ambavyo vyengine vinahitaji kufutwa.

Vyengine vikihitajika kufanyiwa marekebisho na vyengine vilivyobeba maneno makali kama ‘uwezo wa waziri, waandishi kudhibitiwa na kufanya uchochezi’.

Kwenye sheria hii ambayo kwa sasa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar kwa ufadhili wa Shirika la Internews, wanaharakishwa kufutwa, vipo vifungu kadhaa mabavyo vimepitwa na wakati na kuwa na sheria mpya.


VIFUNGU KANDAMIZI KWA UHURU WA HABARI ZANZIBAR

Moja ya kifungu ambacho kwa sasa wadau wanataka kifutwe, ni cha 39 ambapo chenyewe kinaeleza ‘sharti la kukusanya na kutoa habari na vifaa vya habari’.

Kifungu kimeanza vizuri, kuwa hakuna mtu atakayepewa kibali cha maandishi cha kukusanya habari, isipokuwa awe (i) mwandishi wa habari wa ndani au (ii) mwandishi huria wa habari.

Kifungu hicho cha 39 (2), ikaeleza kuwa Mkurugenzi anaweza bila ya kutoa sababu, kukataa kutoa kibali hicho, kukifuta au kukizuia.

Lakini kifungu cha (3) kikatoa haki kwa mkono wa kulia na kupokonya kwa mkono wa kushoto, kwa muathirika wa kibali hicho (mwandishi wa habari) kwamba anaweza kukata rufaa.

‘’Muathirika anweza kukata rufaa ya kuzuialiwa, kukataliwa, kufutwa kwa kibali chake moja kwa moja wa Waziri wa habari ndani ya wakati,’’kinafafanua kifungu.

Kifungu cha (4) ambacho kinapokonya haki hiyo, kinaeleza kuwa ‘kila uamuzi wa waziri kuhusiana na rufaa ya mwandishi wa habari, utakuwa ni wa mwisho na hautafanyiwa mapitio (haukatiwi rufaa) na mhakamani’.

Kwamba iwapo waziri amemkatilia mwandishi wa habari kumkosesha kibali, kukifuta, kukizuia au kukikataa uamuzi wake huo utakuwa wa mwisho.

Lakini hata mazonge mengine ya sheria hii yapo kwenye kifungu cha 40, kinachoelezea uwezo wa waziri wa Habari wa kufuta kibali kilichotolewa na Mkurugenzi.

Kwamba mwandishi wa habari ameshaomba kibali kwa Mkurugenzi, ameshalipa ada itakayopangwa, lakini sheria inampa uwezo Waziri kukifuta kibali hicho.

Waziri anaweza kufuta kibali kilichotolewa na Mkurugenzi ikiwa kwa maoni yake tu, ufutaji huo utakuwa ni kwa maslahi ya umma au ni kwa maslahi ya usalama na utangamano wa taifa’

Kwamba sheria hii, imempa uwezo wa kupitiliza Waziri, na kwamba anaweza, kufuta kibali kwa maoni yake tu, akihisi kukifuta huko, kwa faida kwa taifa.



WADAU WA HABARI WANASEMAJE?

Mdhamini wa Baraza la Habari Tanzania MCT-Zanzibar Shifaa Said Hassan, anasema sheria hiyo imeshapitwa na wakati na moja ya vifungu vibaya ni cha 39 na 40.

‘’Haiwezekani suala la haki ya kikatiba ya kupata na kutoa habari, apewe uwezo wa kupindukia waziri, juu ya kuona nani apewe au asipewe kibali,’’anasema.

Mchambuzi wa sheria za habari Zanzibar Imane Duwe anasema, kwenye nchi ya utawala wa sheria na demokrasia kama ilivyo Zanzibar, sheria hiyo vifungu vyake kadhaa vinapingana na katiba ya nchi.

‘’Iweje kuwe na sharti la kukusanya habari, tena moja ya sharti hilo uwe na kibali ambacho hakitolewi na kamati wala bodi anatoa mtu mmoja,’’anaelezea.

Anasema maajabu mengine ambayo yamo kwenye sheria hiyo ni kifungu cha 40, ambacho kimempa uwezo mkubwa waziri, juu ya kukubali ama kukataa kutoa kibali.

‘’Kinachoonesha udhaifu kuwa, hata mwandishi akikataliwa na waziri kuwa hawezi kuomba kibali, hapo ndio mwisho wa kulalamika,’’anafafanu.

Kwamba uamuzi wa waziri hauwezi kukatiwa rufaa katika mahakama yoyote na hata mwandishi hawezi kumshtaki waziri huyo wa kiongozi wa nchi aliyemteua.

Mwanasheria wa Shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar na mhariri wa habari wa shirika hilo Juma Khamis Juma, anasema ujio wa mapinduzi ya habari ya kidigitali, suala la kibali halipo.

‘’Wanachotakiwa mamlaka ni kufuatilia utendaji wa kazi wa waandishi wa habari na watoa taarifa, lakini sio kuwabana na kuwawekea sheria ngumu,’’anasema.

Mratibu wa Internews Zanzibar Zaina Mzee, anasema vifungu ambavyo vinampa uwezo waziri, ni dhahiri vinapingana na katiba ya nchi.

‘’Muda wa kuwa na sheria unaotaja cheo cha mtu umepita, maana unaweza kuwakosesha wananchi kupata habari, kwa kule waziri, kumchukia mwandishi wa habari tu,’’anasema.



Na ndio maana anasema, Internews imekungana kwa karibu na TAMWA-Zanzibar pamoja na wadu wengine wakiwemo waandishi wa habari, ili kuhakikisha Zanzibar inakuwa na sheria mpya.

‘’Nguvu ya kutaka sheria mpya ya habari, sisi tunavitegemea vyombo vya sheria, na ndio maana tunavishirikisha kila hatua, ili kusaidia kuzieleza mamlaka ubaya wa sheria zinazosimamia habari ulivyo,’’alieleza.

Mhariri mtendaji wa shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar, Ali Haji Mwadini anasema, ukuaji wa maendeleo ya taifa lolote hutegemea mno, uwepo wa waandishi huru wa habari.

‘’Kama bado kuna sheria inaelekeza kuwa waziri anaweza, mkurugenzi akiona, kwa maoni yake au akihisi hiyo sio demokrasia,’’anasema.

WAANDISHI WA HABARI WANASEMAJE?

Abid Juma Suleiman, mwandishi wa habari wa shirika la Magazeti Pemba, anasema sheria hiyo ya Magazeti, Vitabu na Mawakala wa Habari nambari 5 ya mwaka 1988, imekuwa kikwazo kwao.

‘’Ilishawahi kuwakumba waandishi wa habari wa vyombo binasfi kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chambani Mkoani Pemba, kwa kukoseshwa vibali,’’anasema.

Mwandishi wa habari wa kituo cha tv na redio cha Zenj fm Is-haka Mohamed Rubea, anasema sheria hiyo hasa kwenye upatikanaji wa kibali, imekuwa shida.

Mwandishi wa redio Jamii Mkoani Khadina Rashid Nassor, anasema sheria yenye vifungu kandamizi, huwaumizi zaidi waandishi wa vituo binafsi.

Mwandishi wa Gazeti la mtandaoni la Mwanahalisi Jabir Idrissa na mwandishi mwandamizi Salim Said Salim, wanasema suala la kusambaaza na kupata habari ni la kikatiba, halipawi kuweka sharia ngumu.

NINI KIFANYIKE?

Mkurugenzi wa TAMWA-Zanzibar Dk. Mzur Issa Ali, anasema ujio wa sheria mpya ya habari, vifungu vinavyompa uwezo mkubwa waziri vifutwe.

‘’Lakini napendekeza kama habari ni haki ya kikatiba, sharti la kutoa kibali lisiwemo mikononi mwa mtu, bali iwe ni bodi ya ushauri wa habari,’’anapendekeza.

Mchambuzi wa sheria za habari Zanzibar Imane Duwe, anasema maneno kama ‘uwezo wa Mkurugenzi, Waziri, akiona inafaa, akihisi, kwa maoni yake’ kwenye sheria mpya ya habari yasitumike.

‘’Sote tunakubali kuwa kila mmoja anamapungufu yake, sasa kama waziri wa habari, akipewa uwezo mkubwa wa kukubali au kukataa kibali, itafika wakati Zanzibar kusiwe na waandishi wa habari,’’anaeleza.

Mdhamini wa Baraza la Habari Tanzania ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan anasema, wakati umefika Zanzibar kuwa na sheria bora na rafiki.



‘’Ndio maana TAMWA-Zanzibar kwa kushirikiana na wafadhili wetu shirika la Internews, tunaomradi  ambao lengo lake kuu ni kuwawezesha waandishi kusukuma mbele upatikanaji wa sheria mpya habari Zanzibar,’’anasema.

Mwandishi wa kituo cha redio cha Sauti ya Istqama Salim Ali Msellem na mwenzake wa tv ya mtandaoni jicho letu Amina Ahmed, wanasema rufaa ya kukataliwa, kufutiwa kibali isiishie kwa Waziri kama ilivyo sasa.

‘’Suala la habari ni la kikatiba, basi ieleze wazi kuwa waziri akifuta, akikataa kutoa kibali muathirika, sheria ielekezea hadi afike mahakamani,’’anasema.

WANANCHI WA KAWAIDA

Asha Ali Haji mwenye ulemavu wa viungo wa Mtambile, anasema, waandishi wanapowekewe vikwazo kwenye kukusanya, kutafuta na kuandika habari waathirika ni wao wa chini.

Hemed Haji Omar wa Wambaa Mkoani anasema, sheria kandamizi kwa waandishi wa habari ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

                              Mwisho

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...