NA
HAJI NASSOR, PEMBA:
“KESI
ya mtoto wangu mwenye ulemavu wa matamshi, ilifutwa mwaka 2021 mahakamani, kwa
sababu ya siuntafahamu ya eneo alilobakwa ni tofauti na walilolitaja
mashahidi,’’anasema mama wa mtoto huyo.
Mama huyo mkaazi wa Pujini Dodo wilaya ya Mkoani, anasema tokea
asili mtoto wake anaulemavu wa akili na matamshi, sasa kasoro ya kumbu kumbu
yake ndio chanzo cha kukosa haki zake.
Anasema bado watu wenye ulemavu, mara baada ya kubakwa imekuwa
ni shida mpya kuvifikia vyombo vya sheria, kutokana na ulemavu wao wakati
mwengine sheria kuwa na kasoro kwao.
Baada ya mtoto wake kubakwa na mtuhumiwa Abdalla Khatib Abdalla miaka
25, mwanzoni mwa mwaka 2018, kesi hiyo ilichukua tena miezi minane, hadi kufika
mahakamani.
“Nilipofika kituo cha Polisi Chake chake, kwanza sikupata
ushirikiano, na walionipokea wakaniambia kesi yangu inaweza kuwa ngumu
mahakani, kwa sababu hakuna mkalimani,’’anasimulia.
Anasema ingawa askari hao wenyewe kwa wenyewe, walipingana na
kuelezana kuwa, hiyo wao sio kazi yao, na walitakiwa wanichukue maelezo.
Alipelekwa kwenye dawati la jinsia la Polisi la wanawake na
watoto, na kuchukuliwa maelezo, ingawa shida ya kwanza ilikuwa wakati siku
mbili alipotakiwa kumfikisha mtoto wake kwa mahojiano.
Kwa siku hiyo, anasema mtoto wake alieleza kila kitu na kama
alivyofanywa na mtuhumiwa, ikiwa ni pamoja na kumfanyia udhalilishaji kichakani
chini ya Mwembe.
Baada ya kuchukuliwa maelezo hayo, kesi yake alikaa miezi mitatu
bila ya kufikishwa mahakamani na alipoulizwa, aliambiwa asubiri upelelezi
ukamalike.
Ilipofika Disemba 2019, anasema alipata simu kuwa, anatakiwa
kufika mahakama ya Mkoa Chake chake na kwa mara ya kwanza kesi yake ilisomwa.
Mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka huo huo, aliatakiwa kumpeleka
mtoto wake mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi, na akawaeleza kuwa anatabia
ya kupoteza kumbu kumbu.
“Ni kweli siku aliyotoa ushahidi wake, alisema alifanyiwa tendo
hilo ndani ya nyumba, ingawa Polisi alitaja kwenye kichaka,’’anasimmulia mama
huyo.
Kisha kesi hiyo mwishoni mwa mwaka 2020, Mahakama ya Mkoa Chake
chake, ilimuachia huru mthumiwa huyo kwa sababu ya mkanganyiko wa eneo
alilodaiwa kubakwa.
Lakini hata dada wa mtoto wa miaka 16 mwenye ulemavu wa
matamshi, wa Wawi Chake chake, anasema baada ya mdogo wake kutoa taarifa za
kubakwa na kijana Shaaban Mohamed Issa miaka 35, kwanza alichelewa kutafutwa.
“Familia ilikuwa inaniambia mtoto wenu mwenye ulemavu hawezi
kushinda kesi dhidi ya mtoto wangu, kama mnamtafutia muume kwa nguvu sio mtoto
wetu,’’anadai kuelezwa.
Alipofika kituo cha Polisi Juni 12, mwaka 2020 alielezwa kuwa,
wahusika wa kesi hizo hawapo, hivyo alirudi na kwenda siku ya pili.
“Siku ya pili nilifika saa 1:00 asubuhi, lakini huduma niliipata
majira ya saa 8:00 mchana maana wanasema walikuwa kwenye kikao, na siku hiyo
nilichukuliwa maelezo nusu tu,’’anasimulia.
Siku tatu baadae, alipata tena wito wa kutakiwa kufika kituo cha
Polisi akiwa na mdogo wake, na kuchukuliwa maelezo hadi na walipomaliza
walirejea nyumbani.
Alipotaka kujua ikiwa mtuhumiwa wameshamkamatwa walimueleza kuwa
bado, ingawa alipewa namba za simu za Polisi, ikiwa atamuonea apige simu.
“Haya kama nitamuona kama simu yangu ikiwa haina salio
je…nifanye nini,’’aliuliza kituo cha Polisi na kujibiwa kuwa kama anataka haki
ya mdogo wake, simu isikauke salio.
Wiki tatu baada ya kumuona mtuhumiwa akiwa anatembea mitaani,
alifika tena kituo cha Polisi na kuwaeleza, na hapo alitaka kupewa hati ya
kumkamata na kuikataa.
“Kwa uchungu…. wale askari walinataka kunipa hati ya kumkamata
‘warantee’ lakini nikawaambia mimi sina uwezo wa kumkamata mtuhumiwa hiyo ni
kazi yenu,’’alisema.
Alitamani kuachana na kesi hiyo, ingawa alipata msaada kwa
jumuia za watu wenye ulemavu na kutakiwa kuendelea kuitafuta haki ya mdogo
wake.
Mwezi Novemba mwaka jana, baada ya kukaa kwa muda na ukimnya
ukitawala, alifika tena kituo cha Polisi na kuwaeleza kuwa mtuhumiwa yupo
mtaani.
“Mara hii nilambiwa gari haina mafuta, hivyo kama anaweza
kuchangia itakuwa kazi rahisi kumfuatilia mtuhumiwa huyo kijiji cha Wawi,
ingawa alishindwa kutoa fedha hizo,’’analalamika.
Wiki moja baada ya kurudi kituo cha Polisi, alisikia kuwa tayari
mtuhumiwa ameshakamatwa, na alipofuatilia alilithibitisha hilo na kisha
kupelekwa rumande.
“Kpindi cha Corona nasikia yalipata dhamana, lakini katoroka
hadi leo hii, na kesi yangu sijui ilipofika maana sijawahi kuitwa mimi wala
mdogo wangu mwenye ulemavu hadi sasa,’’anasema.
Kadhia kama hii hata mazazi wa mtoto mwenye ulemavu wa viungo,
aliyepewa ujauzito na askari wa chuo cha Mafunzo kambi ya Kengeja wilaya ya
Mkoani, nae analia na vyombo vya sheria.
Mtuhumiwa huyo askari wa chuo cha Mafunzo Suleyom Idd Saleh
miaka 30, alimpata ujauzito mwanamke mwenye ulemavu wa viungo na akili.
Baada ya tukio, wazazi wanadai kuliitishwa vikao vya siri, baina
ya upande mmoja wa familia na wakuu wa kambi ya Kengeja, ili kesi hiyo
isipelekwe kwenye vyombo vya sheria.
Baba wa mtoto huyo, alishafuatwa zaidi ya mara mbili na upande
wa kambi ya Chuo cha mafunzo, kwamba kesi hiyo iishie kwa wao kufunga ndoa.
Ingawa baadae kesi hiyo ilifikishwa mahakamani, miezi mitatu
baada ya kubainika na ujauzito wa miezi sita, kisha alijifungua na mtoto
kupita.
Njama za mtuhumiwa huyo za kutaka kufunga ndoa na mwanamke huyo
mwenye ulemavu wa viungo, ambae pia alikuwa jirani yake, zilifanikiwa na sasa
wanaishi mke na mume.
Mwanasheria kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Pemba Ali
Amour Makame, aliyekuwa akiisimamia kesi hiyo, anasema imeshafutwa mwishoni mwa
mwaka 2019.
KASORO
ZA SHERIA
Kifungu cha 151 (1) cha sheria nambari 7 ya mwaka 2018 Sheria ya
Mwenendo wa Makosa ya Jinai Zanzibar, imeweka wazi yasio na dhamana mahakamani
Kwa mfano kubaka, kuingia kinyume na maumbile, kuingilia
maharimu, kubakwa kwa kundi, kunajisi mtoto wa kiumbe , ingawa kasoro ipo
kwenye kifungu cha 116.
Ambapo kifungu hicho kimekataa dhamana kwa kosa la kunajisi mtu
mwenye ulemavu wa akili, hata kama mtuhumiwa huyo alikuwa anajua kuwa
aliyemnajisi ana ulemavu huo.
MAPENDEKEZO
Ingetungwa sheria moja tu ambayo itajumuisha makossa yote ya
udhalilishaji, badala ya sasa kuwepo kwenye sheria mbali mbali kama vile sheria
ya kuwalinda wari na mtoto wa mazazi mmoja nambari 4 ya mwaka 2005
Au pia kwenye Mtoto nambari 6 ya mwaka 2011, sheria ya Elimu
nambari 6 ya mwaka 1982 hata katikja sheria ya Makosa ya Mwenedo wa Jinai ambary
7 ya mwaka 2018.
WADAU WA HAKI JINAI
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kusini Pemba Richard Tedei
Mchomvu, anasema changamoto kubwa kwa wenye ulemavu baada ya kudhalilishawa, ni
kukosa taaluma ya kuyaripoti matendo hayo.
Hakimu wa mahakama ya watoto Pemba Luciano Makoye Nyengo,
anasema changamoto inayojitokeza hadi kesi za watoto wenye ulemavu, kutofikia
pazuri ni changamoto ya ushahidi.
“Ni kweli kwa hatua za awali, wanapohojiwa kituo cha Polisi huwa
ndugu na jamaa zao wanasaidia kukamilisha maelezo ya mwanzo, lakini kisheria
hawaruhusiwi kufika tena mahakamani,’’anafafanua.
Luciano anabinisha, kuwa sheria haimtambui mkalimani wa awali
aliyesaidia kutoa maelezo kituo cha Polisi, na kisha kufika mahakamani,
ikihofiwa kuegemea upande mmoja.
Hidaya Mjaka Ali, anasema sababu kuu ya watu waliobakwa na
kutovifikia vyombo vya sheria, ni kutawala kwa rushwa kwa baadhi ya vyombo vya
sheria.
Suleiman Mansour, anasema watoto wenye ambao wanabakwa hukumbana
na kuzungurukwa na vikwazo, ikiwa ni pamoja na nenda rudi ya kila siku ya kituo
cha Polisi.
Mratibu wa Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania
TAMWA-Zanzibar ofisi ya Pemba Fat-hya Mussa Said, anasema ndio maana TAMWA
inaendelea kuziibua kasoro za sheria hizo, ili ziangaliwe upya.
‘’Sisi tunashirikiana na waandishi wa habari, ili kuona sasa
kasoro ambazo zinaonekana kudumaza mapambano ya udhalilishaji zinaibuliwa na
kufanyiwa kazi,’’anasema.
Akatolea mfano kuwa kukosekana kwa wakalimani mahakamani ni
kasoro kwa watu wenye ulemavu mara baada ya kudhalilishaji.
WALIOFANIKIWA
KESI ZAO KUFIKA MAHAKAMANI
Mzazi wa Kengeja wilaya ya Mkoani, alisema baada ya mtoto wake
wa miaka 15 kubakwa, alifuatilia kwa muda siku nne kituo cha Polisi Kengeja na
kumfuata kamanda wa Polisi mkoa mara tatu.
“Nilikaa kwa muda mrefu, kesi yangu haijafikishwa mahakamani,
lakini sikukaa tu nilifuatilia kituo cha Polisi na kisha nilipoona
haijafikishwa mahakamani, nilikwenda kwa kamanda wa mkoa,’’anasema.
Hata mzazi wa Wambaa ambae mwaka 2019 mtoto wake alibakwa,
anasema alihamia kituo cha Polisi Mtambile hadi pake mtuhumiwa alipokamatwa.
“Mwaka huu mwanzoni, mshitakiwa ameshafungwa miaka saba, na
alitulipa fidia ya shilingi 200,000 lakini hadi kufanikiwa hilo, nilikumbana na
vikwazo, ikiwa ni pamoja na nenda rudi,’’anasema.
NINI
KIFANYIKE
Asha Said Omar mwenye ulemavu wa viungo wa Mchanga mdogo,
anasema ili kesi za watoto weye ulemavu zifikishwe kwenye vyombo vya sheria, ni
vyema kuanzishwa madawati ya jinsia ngazi ya jimbo.
Omar Mjaka Ali wa Vitongozji anaona lazima kuwe na askari maalum
wanaofuatilia kesi za udhalilishaji za watoto wenye ulemavu, ili kuwapunguzia
vikwazo, wakati wanapofuatilia vyombo vya sheria.
Aliyekuwa Mwanasheria dhamana ofisi ya DPP Ali Rajab Ali,
anasema, haki hutafutwa, hivyo wazazi na walezi waendelee kupambana na
changamoto zilizopo.
SHERIA
YA WATU WENYE N0 6 YA MWAKA 2022 ZANZIBAR
Kifungu cha 30 kinasisitiza wajibu wa kila mtu kulinda, kutetea
haki za watu wenye ulemavu, ikiwemo pale wanapovunjiwa haki zao za msingi
ikiwemo kudhalilishwa.
Na Kifungu cha 31 kikaenda mbali zaidi kikifafanua kuwa, watu
wenye ulemavu hawatobaguliwa au kudhalilishwa kwa namna yote kwa sababu ya
ulemavu wake.
MIKATABA
YA WATU WENYE ULEMAVU
Mkataba wa kimataifa wa haki za watu weye ulemavu, Ibara ya 5
imechambua usawa na kutogaliwa mbele ya sheria, kwamba watu wote wako
wanaulinzia sawa.
Mwisho
Comments
Post a Comment