NA JUMA SEIF, PEMBA;
Wazaidiz wa sheria wametakiwa kuhakikisha wanaisaidia na kuilekeza jamii katika kutekeleza sheria za nchi.
Akizungumza katika mkutano wa jumuiya ya Wasaaidizi wa sheria ya Wilaya ya Chake chake CHAPO uliofanyika Febuari 4, 2023 mjumbe wa bodi wa jumuiya hiyo Kassim Ali Omar amesema wasaidizi wa sheria wanawajibu wa kuiyelekeza jamii katika kuzifahamu na kujuwa namna bora ya kuzitekeleza.
Amesema sheria inagusa kila pahala katika maisha ya watu kwani sheria hizo zina lengo la kuleta ustawi na usawa katika maisha ya watu.
Mjumbe huyo amesema wasaidizi washeria wanawajibu mkubwa wa kuisadia jamii hasa wakati anapokuwa na tatizo kwqni ndani ya jamii kuna watu wengi wanapokumbwa na tatizo hajui wapi namna ya kuzipata haki zake.
"Ni lazima sisi wasaisizi wa sheria tuwape wananchi njia ya kujua haki zao kipinsi wanapokuwa na tatizo, kwani mtu hadi anagika mahakamani anakuwa hajui chochote kuhusu sheria ya kosa lake".
Pia Adam Abdalla Fakih ambaye ni mjumbe wa CHAPO amesema katika kutekeleza majukumu yao vizuri ni vyema kwa wasaidizi wa sheria kuwajibika na kufanya kazi kwa mashirikiano katika kutekeleza majukumu ya taasisi ili kuweza kupata wepesi wa kuisaidia jamii.
Aidha amewakumbusha wasidizi wa sheria wilaya ya Chake chake wakuiwezesha jamii kuepuka vitendo vya udhalilishaji kwa kuipa elimu ambayo itawaondoa kwenye rushwa muhali jambo ambalo linakwamisha upatikanaji wa haki, kuongezeka vitendo vya udhalilishaji na kuwaumiza wathirika ikiwemo watoto wenye umri chini ya miaka kumi na tano.
Kwa upande wake mkurugenzi jumuiya ya wasaidizi sheria wilaya ya Chake chake Nassor Bilali Ali aliwataka wasaidizi wa sheria kuhakikisha wanajisali ilikupata uhalali wa kuisaidia jamii kwani wasipo fanya hivyo ni kukwamisha utekelezaji wa majukumu yao ya kuwasaudia jamii kama idara inavyoelekeza.
Wasaidizi wa sheria wao wamesema ipo haja kwa mamlaka husika kuwawekea mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu wakati wanapofikwa na tatizo la kisheria na kuwasaidia zaid kwani hawa huwa wanapata tabu wakati anapokabiliwa na changamoto ya kesi kwani huwa wanateseka hadi kupata haki zao.
Mratibu wa jumuiya hiyo Mohamed Hassan Abdalla amesma katika kufanikisha majukumu ya wasaidizi wa sheria ni lazima tufanye kazi kwa vikundi ikiwemo zile shehia za karibu, kwani majukumu ya mtu mmoja mmoja inaleta ugumu katika kutekeleza majukumu ya wasaidizi wa sheria kwa haraka.
ReplyForward |
Comments
Post a Comment