NA HAJI NASSOR, UNGUJA::::
KITUO cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ kwa kushirikiana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa, ofisi ya haki za binadamu (UN-OHCHR) asubuhi ya leo Disemba 10, 2022 wanatarajia kufanya kongamano maalum la maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki za binadamu ulimwenguni.
Akitoa taarifa kwa
waandishi wa habari ofisini kwake Kijangwani mjini Unguja, Disemba 9, 2022 Mkurugenzi Mtendaji
wa Kituo hicho Harusi Miraji Mpatani, alisema Mkurugenzi wa Mashataka Zanzibar
Jailan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Alieleza kuwa, kongamano
hilo linatarajiwa kufanyika ofisini kwao Kijangwani mjini hapa, na maandalizi
yote yameshakamilika kwa asilimia 100.
Alisema katika kongamani
hilo la kuadhimisha siku ya kimataifa ya haki za binadamu, wameshirikiana kwa
karibu na ofisi ya Umoja wa Mataifa, ofisi ya haki za binadamu (UN-OHCHR)
Alisema, tayari waalikwa
wote wakiwemo, wanasheria, mawakilisi wa serikali, Polisi, wasaidizi wa sheria,
wanaharakati kutoka Unguja na Pemba, na wananchi wa kawaida wameshaalikwa.
Mkurugenzi huyo alisema, kwa
vile ujumbe wa mwaka huu ni ‘UTU, UHURU NA HESHIMA KWA WOTE’ ni
dhahiri kuwa, unakwenda sambamba na shughuli zao, wanazozifanya kila siku.
Alifahamisha kuwa,
matarajio yao ni kuona waalikwa watajadili kwa uwazi, hali haki za binadamu
hasa kwa upande wa Zanzibar na anaamini kuwa, maadhimisho hayo yatakuja na
maazimio ambayo yataweza kuibua mikakati ya ulinzi wa haki za binadamu kwa watu
wote na kila pmoja kuheshimu matakwa ya sheria na ulinzi huo.
Aidha Mkurugenzi huyo
mtendaji wa ZLSC, alisema pamoja na shughuli hizo, kongamano hilo, litakuwa
sehem ya maadhimishao ya miaka 30 ya Kituo hicho tokea kuasisiwa kwake mwaka
1992.
Katika hatua nyingine,
Afisa Mipango wa ‘ZLSC’ Thabiti Abdalla Juma, alisema kituo kimeshawafikia
wananchi kadhaa wa Unguja na Pemba, kuwapa elimu, ushauri na msaada wa kisheria
bila ya malipo.
Nae Mratibu wa Kituo cha
Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba, Safia Saleh Sultan, aliwaomba
waaalikwa kufika ukumbini kwa wakati.
Awali Mwenyekiti wa Bodi
ya wakurugenzi wa kituo hicho Jaji wa mahakama kuu Zanzibar, Mshibe Ali Bakari,
amesema wakati umefika kila mmoja, kutekeleze wajibu wake ipasavyo.
Mwisho
Comments
Post a Comment