WANANCHI laki 118,760 wakiwemo wanawake 60,203, wanaume 39,641 na watoto 18, 232 wamenufaika na elimu, msaada na ushauri wa kisheria kwa muda wa miaka 30 na kati ya hao, laki 108, 860 wameshinda kesi na kupata haki zao mbali mbali.
Aidha kati
ya hao 11, 8760 ni wananchi 9, 216 pekee ndio ambao licha ya kupata elimu na
msaada huo wa kisheria, walishindwa katika kesi zao.
Akizungumza
kwenye kongamano la maadhimisho ya siku ya haki za binaadamu duniani, leo Disemba
10, 2022 lililofanyika Kijangwani mjini Unguja, na kuandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar 'ZLSC' kwa kushirikiana na Tume ya Haki za Binaadamu 'CHRAGG' kwa ufadhili wa Umoja wa Mataifa, Ofisi ya Haki za Binaadamu 'UN-OHCHR' Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo
hicho Harusi Miraji Mpatani, amesema wastan kwa mwaka waliopatiwa msaada ni wananchi 3, 936.
Ameeleza pia
Kituo kiliwasaidia watoto na masuala ya kisheria 18,232, ambapo pia kwa upande
mwengine, Kituo hicho kiliwapa elimu wananchi katika mikutano ya wazi,
makongamano na semina wapatao 574, 808.
Amesema,
licha ya changamoto ambazo kituo kimepitia wanajivunia kuona wapo wananchi,
waliopata msaada wa kisheria na wengi wao kupata haki zao hivyo.
Hivyo Mkurugenzi
huyo, ameitaka jamii kuendelea kukiunga mkono kituo hicho, ili kutimiza malengo
yake, hasa ya kuwapatia elimu, ushauri na msaada wa kisheria bila ya malipo.
‘’Ni jambo
la kujivuania kwetu na wananchi, kuona kituo kimeaminiwa na wananchi wastani wa
laki 6 kuja kupata ushauri na msaada wa kisheria,’’alieleza.
Akizungumzia
kuhusu kilele cha siku ya kimataifa ya haki za binaadamu, alisema kila mmoja
akiheshimu haki za mwenzake, haki ya binaadamu wote kuwa ni sawa, italeta
maana.
Kwa upande Mkurugenzi wa Kituo hicho Zanzibar, ameipongeza na kuishuru kwa dhati Umoja wa Mataifa, Ofisi ya Haki za Binaadamu 'UN-OHCHR' kwa ufadhili wao ambao umefanikisha shughuli hii.
Akifungua
kongamano la maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar Mgeni Jailan
Jecha, alisema Zanzibar, ilikuwa ya mwanzo kuziweka kwenye katiba yake ya mwaka
1984.
‘’Ipo sura
nzima ambayo lengo ni kuja kuzilinda haki hizo, hivyo ni wajibu wa wananchi,
kuona kila mmoja anailinda haki ya mwenzake,’alieleza.
Aidha
Mkurugenzi huyo alisema haki ya kuishi ndio hasa msingi mkuu wa haki za
binaadamu, hivyo ni wajibu wa jamii na vyombo vya ulinzi na usalama, kulitilia
maanani hilo.
Katika hatua
nyingine, aliupongeza uongozi wa ZLSC kwa kufikisha miaka 30 ya utendaji wao wa
kazi, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao.
Mapema
Mwenyekiti wa Bodi wa ‘ZLSC’ Jaji wa mahakama kuu Zanzibar Mshibe Ali Bakari,
alisema suala la haki za binadamu ni jambo pana.
‘’Hakuna
anayeweza kutoa tafsiri halisi ya maana ya haki za binadamu, hivyo maneno
yaliomo kwenye katiba, kuwa binaadamu wote ni sawa, inatosha,’’aliafanua.
Katika hatu nyingine Mwenyekiti huyo wa ZLSC amesifu juhudi za ufadhili wa kufanikisha shughuli zote za siku mbili kupitia Umoja wa Mataifa, Ofisi ya Haki za Binaadamu 'UN-OHCHR' na kuwaomba waendelee kushirikiana.
''Kwa niaba ya wajumbe wa Bodi wa ZLSC tunawashukuru sana wenzetu wa UN-OHCHR kwa ufadhili wao mkubwa na dio uliofanikisha shughuli hiii, kwa hili hingereni sana,''alifafanua Jaji Mshibe.
Kwa upande
wake, Katibu wa Tume ya Kurekebisha sheria Zanzibar Mussa Kombo, alisema lazima
suala la haki za binaadamu liangaliwe na utamaduni wa nchi husika.
‘’Kwa mfano
Tanzania hatukubaliani na uwepo wa mapenzi ya za jinsia moja, hata kama ziko
nchi zinakubaliana na kuona ni sehemu ya haki za binaadamu,’’alisema Katibu
huyo.
Awali
Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba Safia Saleh
Sultan, alisema changamoto walizokumbana nazo walizigeuza na kua fursa ya
kusonga mbele.
Akiwasilisha
mada ya hali halisi ya haki za binadamu Zanzibar na upatikanaji wake, Naibu
Katibu wa Tume ya Haki za binadamu na Utawala Bora Zanzibar, Juma Msafiri
Karibona, alisema serikali imekuwa mlinzi mkuu wa haki hizo.
Alieleza
kuwa, zipo mamlaka zimekuwa ndizo zilizopewa jukumu ikiwa ni pamoja na Jeshi la
Polisi, tume ya haki za binadamu, katiba na sheria mbali mbali.
‘’Kila mmoja
akitimiza wajibu wake kwa kutii na kuheshimu haki ya mwengine, sio rahisi
kusikia kuwa, kuna mmoja amevunjiwa haki zake,’’alieleza.
Afisa sheria
kutoka vyuo vya Mafunzo Zanzibar Seif Maabad Makungu, alisema kwa sasa haki za
binaadamu, kwa wanafunzi wa vyuo vya mafunzo, iko vizuri, ikiwemo kupata uhuru
wa kuabudu.
Alieleza
kuwa, hata mwaka huu 2022 wanafunzi watatu wameruhusiwa kufanya mitihani yao ya
taifa, sambamba na kuwepo kwa milo mitatu, kupata habari kupitia tv na usomaji
wa magazeti.
Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo,
wamesema elimu bado inahitajika kwa jamii, ili kujua thamani na hadhi ya haki
za binadamu.
Walisema,
Jeshi la Polisi sio wa mwanzo kulinda haki hizo, bali kila mmoja na kwa nafasi
yake, ananojukumu hilo.
Haya ni maadhimisho ya 12 ya haki za binadamu ulimwenguni kufanywa na Kituo cha Huduma za sheria Zanzibar ‘ZLSC’, ili kuwaleta pamoja wadau wa haki za binadamu, kujadili changamoto za uvunjifu wa amani, ambapo kwa mwaka huu yamefadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Ofisi ya Haki za Binaadamu 'UN-OHCHR'
Mwisho
Comments
Post a Comment