NA FATMA HAMAD, PEMBA
‘’KIPINDI cha mvua wanafunzi hulazimika niwafungie wasije madrasani mpaka zitakapo malizika,’’ hayo ni maneno ya Sada Khamis
Hamad mwenye ulemavu wa
viungo ni mwalimu wa madrssa.
Kwake
anasema ulemavu alionao haukua mzigo
kuwa asitimize ndota zake za kuwa
mwalimu wa madrassa.
Hii
ni baada ya kuukosa uwalimu wa skuli kutokana na changamoto za hapa na pale,
ingawa hakukata tamaa.
‘’Nilikuwa
natamani siku moja niwe darasani nafundisha
ila sikubahatika, kusoma skuli hata darasa moja, kwani ilikuwa iko
maeneo ya mbali na siwezi kutembea,’’anakumbuka.
Ukosefu wa kiti mwendo kwa wakati huo, na hasa
kutokana na ukata wa fedha waliokuwa nao wazazi wake, ulimkosesha elimu ya
skuli.
Yote
hayo ni masikitiko ya Mwalimu wa Madrasa ya Qur-aan Sada Khamis Hamad mwenye ulemavu wa viungo
anaeishi katika kijiji cha Shumba Vyamboni Wilaya ya Micheweni Pemba.
Maalim
Sada Khamis Hamad ambae ni mtoto wa sita katika familia yao, anasema suala la kukata
tamaa na yeye lilikuwa mbali mno.
Bada
ya miaka kadhaa, alishindwa hakuweza tena kwenda madrasa kutokana na hali yake
na kwa vile hana usaidizi wa kigari ambacho chengemuwezesha kumsaidia.
Baada
ya kuona anakosa
kusoma, ndipo akamua
anzishe
madrasa yake mwenyewe baada ya kuhitimu kusoma Qur-aan ili aweze kuiendeleza
elimu yake.
‘’Nilisema ijapo kuwa sikuweza
tena kwenda kusoma, lakini isiwe sababu ya
kukaa tu nyumbani, ndipo nikamua
nianzishe madrasa yangu, ili kuwafundisha watoto,’’anaeleza.
Huu
ni mwaka wa nne tangu kuanzisha madrasa hiyo, ambapo alianza na wanafunzi
wanne (4) wawili wa kike na wawili wanaume na sasa
ana wanafunzi 52.
ANA CHANGAMOTO GANI?
Moja anayoiona na kumkosesha usingizi ni
ukosefu wa sehemu salama ya
kusomeshea wanafunzi kutokana na mazingira
yake.
Kwake mazingira hayo, hayako sio rafiki, kwani kwa
sasa anatumia kibaraza cha nyumba yao kuwafundishia wanafunzi
wake.
‘’Nasumbuka
sana
hususan kipindi cha mvua barazani panakuwa hapasomeki inabidi wanafunzi
wasije madarasa mpaka mvua zikate,’’ anasema.
Wanafunzi
wamekuwa wakikimbia na kwenda madrssa nyengine kwa vile kuna sehemu salama za kufundishia.
Akasema
ni wakati kwa wale wanaouguswa na haki ya watoto juu ya elimu, kuona
wanamtembelea na kumpiga tafu, ili kumjengea madrassa ya kisasa.
‘’Si
vyema nguvu zote zikaelekezwa kwenye ujenzi wa miskiti pekee, bali msingi wa
dini ya kiislamu, ni uwepo wa madrassa za kisasa na sio kusomea
barazani,’’anafafanua.
WANAFUNZI WAKE
Asha Khamis na Ali Juma wanafunzi
wanaosoma katika madrsa hiyo, wanasema hawaridhishwi na kitendo
cha kusoma barazani.
‘’Kwakweli hatupendi kusoma mazingira haya, kwani pakiwa na jua hapakaliki, na kukiwa na mvua
tunafungiwa kabisa,’’wanasema.
Wanasema kama kweli kuna nia ya kweli kwa
wadau wa haki za watu wenye ulemavu na watoto kusaka elimu, hakuna budi kujenga
madrassa ya kisasa.
MAMA MZAZI
Hadia
Salim Ameir, anasema mungu amemjaalia kuzaa watoto
wanne
wote wenye ulemavu wa viungo ambapo
mmoja alifariki.
Anasema
mwanzo akiwazaa wanakua ni wazima
wanatembea wenyewe, lakini
kila wakiwa wakubwa ndio wanapata ulemavu.
‘’Nilikua nawazaa ni wazima lakini mwisho wake
wanakua walemavu, na sikuwapeleka Hospital nikajua ni sababu gani ilopelekea hivyo’’,anasema mama huyo.
Aidha
alieleza kuwa anaishi katika mazingira magumu
yeye na watoto wake kwani hata nyumba yao wanayoishi imeshakua mbovu na
haina hata huduma rafiki za vyoo
kwa ajili yao.
“Baba
yao ameshafariki huduma zote
wananitegemea mimi na sina
msaidizi, sina hata kazi ya uhakika ya kufanya maisha yangu ni magumu nahitaji msaada”, alieleza.
Kwa
bahati mbaya wako viongozi wa majimbo kama vile Mbunge au Mwakilishi hajawahi
kupita katika familia yetu ili kuangalia changamoto zilizopo kwenye familia
hii.
Mratibu wa Baraza
la Taifa la
Watu wenye ulemavu Pemba
Mashavu Juma Mabrouk, anasema wamekua
wakiwasaidia watu wenye
ulemavu, ambao wanajishuhulisha na
harakati mbali mbali.
Anasema
wamekua wakifurahika wanapoona
watu wenye ulemavu wakijishuhulisha na
shughuli mbali mbali, hivyo
amewataka wahisani na
wasamaria wema kuelekeza
macho yao kwao.
Hata hivyo amewashauri wazazi wa wanafunzi
wanaosoma katika madrassa hiyo, kuonesha mfano kwa kuanza kuchangishana fedha kwa ajili ya
kuanzisha ujenzi wa madrassa ya kisasa.
”
Sisi Baraza hatuna mfuko maalumu wa kumsaidia mtu mmoja moja kama huyo, kwani
anayoyafanya ni mambo ya kijamii ispokuwa tunawaomba wanajamii kuchangia, ili
aweze kujenga madrassa”, alishauri.
UONGOZI WA SHEHIA
Sheha
wa shehiya ya Shumba vyamboni Time Said Omar, ameleza kuwa mwalimu
huyo anapata shida kwani
anasomeshea wanafunzi wake katika baraza
ya nyumba yao
na wakati mwengine
hukaa kwenye Muembe.
Amesema ameshachukua
jitihada mbali mbali
kuhakikisha anapatiwa msaada wa kujengewa madrassa japo chumba kimoja,
lakini bado hajafanikiwa.
‘’Nimeshawapeleka
viongozi wengi ili waweze kumsaidia lakini bado hatujafanikiwa na hivi saivi nimejipanga niende kwenye jumuia ya Milele Foundation ili
waweze kumsaidia’’, alieleza sheha .
Licha
ya ulemavu wake lakini mungu amemjalia kipaji cha elimu ameshafika
Dar-es-salamu kushiriki
mashindano ya qur ana, hivyo anahitaji
kuungwa mkono kwa hali na
mali ili aweze kuendeleza kipaji chake hicho.
UONGOZI WA WILAYA
Mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya,
anasema anelewa changamoto ya mwalimu, huyo ingawa wanaangalia namna ya
kumsaidia.
‘’Hakuna
fungu maalum kwa ajili ya kumsaidia mtu mmoja mmoja
kwa ajili ya kujengea
nyumba ama Madrassa, lakini kama wakitokezea wahisani
tutampekelekea,’’anasema.
OFISI YA MUFTI
Msaidizi
Katibu ofisi ya Mufti Sheikh Said Ahmad Mohamed, kwa vile ofisi hiyo ndi msimamizi
mkuu wa madrasa zote za Qur-an, ameahidi kuonana naye.
‘’Nimevutiwa
mno kuona kuna mwanamke tena mwenye ulemavu wa viungo ameanzisha mpango wa
kuihuisha dini ya kiislamu, na sisi tutaangalia namna ya kumasaidia,’’anasema.
KATIBA YA ZANZIBAR YA MWAKA 1984
Kifungu
cha 10 (g) kinafafanua ‘kwamba serikali itawekea mazingira rafiki kwa makundi
ya wagonjwa, waliojiajiri, wazee, watoto na watu wenye ulemavu’.
Lakini
hata kifungu cha 12 (1) kimefafanua kuwa, ‘watu wote ni sawa mbele ya sheria,
na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya
sheria’.’
SHERIA YA WATU WENYE ULEMAVU NO 9/2006
Kifungu
cha 9, kinaelezea haki ya kupata elimu kwa watu wote wenye ulemavu na mafunzo
mengine kama ilivyo kwa raia wengine.
MWISHO.
Comments
Post a Comment