NA HAJI NASSOR, PEMBA:
email:
hajipembatoday@gmail.com
JAMII imetakiwa kufahamu kuwa, ubongo
wa mtoto mchanga unakuwa na ufahamu wa asilimia 25, katika kipindi cha miezi
mitatu baada ya kuzaliwa, hivyo ni wakati mzuri kwa familia kumuandaa mtoto huyo
watakavyo.
Tafiti
zinaeleza kuwa, kama wazazi wanataka kuwa na mtoto mwenye ufahamu wa kujua
mambo kadhaa, waanze nae ndani ya miezi mitatu ya mwanzo, kwa kuzungumza nae,
kumshirikisha na kumtajia majina ya vitu kama vilivyo.
Mtaalamu wa
malezi ya kisayansi ya awali ya watoto ‘SECD’ Rashid Said Nassor, alisema sio
sahihi katika kipindi hicho, wazazi kuzungumza na mtoto wao, kwa kuigizia sauti
ya kichanga.
‘’Sio vyema kwa
wazazi na walezi kuyatumia maneno kama mma, nyamu, chamaki, mbobo, dizi, ledio,
chimu, pecha bali kwa wakati huo, wanapowasiliana na watoto wao, wayatamke majina
kama yalivyo,’’alieleza.
Aidha
mtaalamu huyo alisema, sayansi ikaubali kuwa, mtoto anauwezo mkubwa wa kusikia
na kuhifadhi kila kitu kinachozungumza kwenye jamii yake, kupitia ubongo wake.
Alieleza
kuwa, ubongo wa mtoto mchanga mara anapozaliwa huwa, mtupu na unatabia ya
kuchukua na kugandisha kila kitu, hivyo kama wazazi watatenga muda kumfundisha
mtoto, anakuwa rahisi kuyamudu mazingira yake mapema.
Kwa upande
wake mtaalamu wa malezi ya kisayansi na makuzi ya awali ya mtoto ‘SECD’
Zanzibar Mohamed Dau, alisema mtoto, akifikia umri wa mwaka mmoja, huwa na
uwezo kama wa mtu mzaima kwa asililimia 60.
Alieleza
kuwa, anapofikia umri wa miaka kati ya minne na hadi sita, uwezo wa ubongo wa
mtoto huyo kufahamu kinachoendelea huwa ni kwa asilimia 90.
‘’Wazazi
kama wanataka kuwa na watoto wenye uwelewa na kuyamudu mazingira yao, waanze akiwa
na siku moja baada ya kuzaliwa hadi anapofikia miaka minane,’’alieleza.
Nae mkufunzi
wa malezi hayo kutoka Tanzania bara Davis Gisuka, alisema umri sahihi kwa
wazazi wa kumtayarisha mtoto wao, ni ule kabla ya kuanza elimu ya awali.
‘’Inaonekana
kama vile ili umuandae mtoto vyema, ni kumsubiria hadi afikie miaka minene, kwa
kumpeleka skuli nzuri na kumlipia fedha nyingi, wakati maandalizi mazuri ni
tokea akiwa tumboni,’’alisisitiza.
Kaimu Mkuu
wa Idara ya Ustawi wa Jamii Pemba ambae pia ni mtaalamu wa ‘ECD’ Omar Mohamed
Ali, alisema bado wazazi, wanadhani ni kupoteza muda, wanapoelezwa faida ya
kuwasiliana na watoto wao wachanga.
‘’Wazazi na
walezi, wanaona kama vile uchawi fulani, wanapoambiwa kuwa ubongo wa mtoto
mchanga, unapokea na kuhifadhi kila kitu, lakini ni sahihi na tafiti
zimeshafanywa,’’alisisitiza.
Wazazi na walezi kisiwani Pemba walisema, bado
elimu ya ‘ECD’ haijasambaa ndani ya jamii, na ndio maana bado imekuwa ni vigumu
kwao, kuitekeleza kama ilivyo.
Mkurugenzi
Mkaazi wa tasisi ya Children in Crossfire Cragi Ferla alisema nguvu ya pamoja
inahitajika, kati ya vyombo vya habari, maafisa ustawi na maendeleo kuifikisha
elimu hiyo kwa jamii.
‘’ECD ni njia
ya malezi thabiti, ambayo kama wazazi na walezi watayafuata kama ilivyo,
wanaweza kuona maajabu ya kiungo cha ubongo kwa mtoto, kadiri anavyokuwa
wanakua,’’alieleza.
Mzazi
Hassina Haji Iddi ‘mama dula’ wa Gombani Chake chake alisema, ijapokuwa katika
siku za hivi karibuni, baadhi ya kliniki wanazokwenda wamekuwa wakielimisha
njia hizo.
‘’Zile
kliniki ambazo manesi au madaktari wao wamerudi vyuoni katika miaka ya hivi
karibuni, wamekuwa wakituelekeza mama wajawazito, lakini sio zahanati
zote,’’alieleza.
Hidaya
Kassim Khalfan wa Msingini Chake chake, alisema elimu hiyo inahitajika kupatiwa
na akinababa pia, ili mtoto apate malezi, makuzi ya pande zote.
‘’Kidogo
akina mama wamekuwa wakifanya kwa vitendo malezi ya kisayansi kwa watoto wao
wachanga, kwa kule kuchangamana nao, lakini wanaume bado sana,’’alieleza.
Mzazi Issa
Hassan Issa miaka 55 wa Mtambile alikiri kuwa, bado elimu hiyo ni mpya, ingawa
wamekuwa wakiifanya lakini sio kama maagizo ya wataalamu.
Kwa upande
wake sheikh Mohamed Hussein Imamu, alisema maandiko yanakubali mno, suala la
malezi ya mtoto tokea akiwa tumboni na muda mfupi baada ya kuzaliwa kwake.
Mwisho
Comments
Post a Comment