NA SAIDA ALI, PEMBA@@@@
AFISA Mdhamini Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Ahmed Abuubakar Mohamed,
amesema mazingira mazuri ni kuunga mkono kwa kutumia nishati salama ya gesi, ikiwa
ni njia moja wapo ya kulinda mazingira yao, ili kuweka mabadiliko yanayotokezea
kutokuwa na hali nzuri ya kimazingira.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza wafanyabiasha ya ‘Oryx gas’ juu ya
matumizi salama ya nishati safi ya kupikia, ukumbi wa Tibirinzi Chake chake
Pemba.
Alisema kuwa utumiaji mzuri wa gesi na uhamasishaji, wanaweza kulinda hali
ya mazingira, ukataji wa miti ovyo na uchimbaji wa nchanga na uharibifu wa
viunbe hai ambavyo vinaweza kuwa mazingira mazuri.
" Uwepo wenu kutasaidia wananchi kutumia nishati safi na salama ya kupikia,
pamoja na kuacha kukata miti na mbadala wake, kutumia gesi, ili kuhakikisha
hali ya mazingira inakuwa salama," alifafanua.
Meneja Mkuu wa taasisi ya Oryx gas Zanzibar Shuwekha Khamis Omar, alisema kuwa,
wanadhamira ya kuhakikisha upatikanaji wa gesi, unakuwa wa uhakikika na kuimarisha
huduma zao kwa ufanisi.
Alisema kuwa, ufanisi huo umekuwa hasa katika kipindi hichi cha miaka mitano,
wameweza kuimrisha huduma zao kwa kuweka bohari kubwa la kupokelea gesi na
kuhifadhi eneo la Mangapwani Unguja.
Alieleza kuwa, bohari hiyo imeweza kupokea Meli za Gesi Zanzibar, na uhifadhi
mkubwa wa karibu tani 1,300 na inauwezo wa kutumiwa na wananchi
wa Unguja na Pemba.
"Tumekuwa tukiimarisga huduma na ufanisi mkubwa katika tasisi yetu, na ufanisi
huo umekuwa hasa katika kipindi hichi cha miaka mitano kwa kuweka bohari kubwa
ya kupokelea na kuhifadhi,’’ alieleza.
Mkurugenzi wa Oryx gas Zanzibar Fuad Alinabhany alisema, nishati pekee yenye
kuaminika ni utumiaji wa oryx gas pamoja uuzaji wa mitungi hiyo.
Kwa upande wake mfanyabiashara Juma Mussa Said wa Chanjaani Chake chake, aliahidi
kuyachukua vyema mafunzo hayo na kuwa mabalozi mzuri, kwa wauzaji wao.
Alisema kuwa jambo jema walilolipata hapo kwenda kuwahamasisha watumiaji wa gesi,
kueka sehemu salama pamoja na kuinasihisha jamii, kutumia nishati mbadala.
MWISHO.
Comments
Post a Comment