NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
JUMUIYA ya kuhifadhisha kur-an ya kanda ya Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, inakushudia kuendesha mashindako ya kanda, mwishoni mwa mwezi huu, na kuwaomba waumini wenye uwezo, kuiunga mkono jumuiya hiyo, kwa ajili ya zawadi za washindi.
Hayo yameelezwa jana na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ustadhi Hassan Othman Khamis, kwenye mfululizo wa vikao vya maadalizi, vilichofanyika Chumbageni chini ya msaidizi mlezi wao, Abrhaman Mohamed Khamis.
Alisema, tayari Jumuiya hiyo imeshafanya mashindano ya mchujo uliofanyika Machi 1, mwaka huu, hivyo sasa inatoa nafasi kwa kuandaa mashindano makubwa, mwishoni mwa mwezi huu.
Alieleza kuwa, ni nafasi kwa wenye uwezo kushirikiana na Jumuia hiyo, kwa ajili ya kukitangaaza kitabu cha Allah (S.W) kupitia mfumo wa mashindanI kwa wanafunzi.
Mwenyekiti huyo, aliwakumbusha wale wenye nia ya kuungana nao, kuwa mwenye kuchangia jambo jema hasa katika mwezi huu mtukufu wa ramadhan, Muumba ameshahidi malipo makubwa kwa mja wake.
‘’Niwaombe wale wote wenye uwezo wa kifedha au zawadi nyingine kuungana na kamati yangu, ili kuona tunafanikisha mashindani yetu ya tano kwa mwaka huu,’’alieleza.
Akizungumzia juu ya wakaazi wa shehia za Wambaa na Chumbageni, aliwakumbusha kuendelea kuwaunga mkono kama ilivyokuwa kwa mwaka jana, kwani mpango huo sasa wa mashindani utakuwa kila mwaka.
Katibu wa Jumuiya hiyo ustadhi Abdalla Haji Ali, alisema fedha wanazohitaji ili kufanikisha mashindani hayo pamoja na zawadi kwa washindi na washiriki wingine ni shilingi milioni 1.6.
Alifahamisha kuwa, hadi sasa waumini wenyewe wa shehia za Wambaa na Chumbageni wameshachangia shilingi 640,000 jambo ambalo bado nguvu zinahitajika.
Hata hivyo alisema, kamati ndogo iliyoundwa kuratibu mashindani hayo, inaendelea kupita kwa waumini wa makundi mbali mbali, ili kuomba sadaka zao.
‘’Bado kamati yangu ya kuratibu jambo hili, inaendelea kuwatembelea waumini kama wafanyabiashara, wamiliki wa hoteli, masheha na waalimu wa skuli, ili nao kutoa sadaka zao,’’alieleza.
Msaidizi mlezi wa Jumuiya hiyo sheikh Abrhaman Mohamed Khamis, alisema ili kufanikisha mashindano hayo makubwa kwa kanda ya Wambaa na Chumbageni, ni waumini wenyewe kutoa sadaka zao.
‘’Ikiwa waumini wa dini ya kiislamu wataamau kwa moyo wa dhati, tunaweza kufanikisha mashindani haya ya tano, kama tulivyojipangia, na hasa katika eneo la zawadi,’’alisisitiza.
Mjumbe wa Jumuiya hiyo Raya Juma Khamis, alipendekeza kuwa, ni vyema kwa wazazi na walezi kuwaunga mkono watoto wao, hasa katika kuwatunza.
Katika mashindani hayo ya tano kwa mwaka huu, yatashirikisha madrassa saba kutoka Wambaa na Chumbageni, kwa juzuu ya kwanza, pili, tatu, tano, saba, 10, 15 na 20.
Mwisho
Comments
Post a Comment