Mwakilishi wa Jimbo la Chwaka Issa Haji Ussi, amesema ataendelea kutoa misaada mbali mbali ya vifaa vya kielimu katika Jimbo hilo.
Kauli hiyo ameitowa huko Ndijani wakati akikabidhi vifaa mbali mbali vya kielimu.
Alisema vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka ambapo vitatumika zaidi msimu huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani unao tarajiwa hivi karibuni.
Alieleza viongozi wa Jimbo Hilo wako pamoja na wanchi katika kuwafikishia kile wanacho kitaka katika sehemu zao.
Aidha mwakilishi huyo alisema wako tayari kusaidia katika Kila sekta ambayo imekuwa na changa moto ya miundo mbinu husika.
Vifaa hivyo vilivyo tolewa vimegharimu zaidi ya shilingi miloni Hamsini huku ahadi ikitolewa kwa imamu atakae swalisha tarawehe atalipwa elfu Hamsini
Mmoja wanafunzi Haisam Juma kwa niaba ya wanafunzi wenzake alieleza msaada huo wameupokea kwa mikono miwili na watautumia kama wali vyo jipangia.
MWISHO
Comments
Post a Comment