NA MWANDISHI WETU,@@@@
MKURUGENZI muanzilishi kutoka bilali Muslim missin of Tanzania Kairo Nbanu Alidha alisema kuwa, kwa mashirikiano ya Tigozanztel wameamua kuanzisha kambi ya matibabu ya macho siku 3 kisiwani Pemba.
Alieleza kuwa tayari wamejipanga katika kuwapatia matibabu wagonjwa 1000 kwa siku, wakiwemo na waupereshi 3000 kwa siku tatu, watakazo kuwepo.
Aliyasema hayo huko katika skuli ya Uweleni wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini Pemba, wakati alipokuwa akitoa huduma kwa wananchi kutoka sehem mbali.
Aidha aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi, kuja kupata huduma hiyo kwa itawasaidia wao na kuhamasisha wenzao ambao, hawakufika kwa siku hiyo.
"Huduma ni bure kuanzia dawa, miwani na hata upasuwaji, kwani tunashirikiana na Wizara ya Afya, kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo.
Naye katibu wa CCM Neclaus Chibwana, ambaye alifika katika kambi hiyo, kwa kupata matibabu, alieleza kuwa ni vyema kwa shirika hilo, kuendelea kuja kisiwani Pemba, kwajili ya kutoa huduma hiyo, kwani walio wengine wanakosa huduma, kutokana na sababu mbali mbali.
Meneja kanda ya TigoZantel kisiwani Pemba Said Massoud Ali, alisema wameamua kushirikiana na shirika hilo kwa lengo la kuhamasisha jami, kwa jili ya kupata huduma hiyo ambayo ni bure.
Nao wananchi waliopatiwa matibabu hayo wakiwemo wanafunzi, walielezea kurahishwa kwao na huduma hiyo kwani, ingewabidi kwenda hospitali ya Wete kuifuata.
Zaiba Ali Hassan mkaazi wa Michenzani, aliwashukuru madaktari hao kwa kua ipo haja ya kutoa huduma hiyo, kisiwani Pemba kwani wanapata usumbufu wakati wanapohitaji huduma kama hiyo, kutokaa na gharama kubwa za matibabu yake.
mwisho
Comments
Post a Comment