NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MAHAKAMA
ya Wilaya Wete, imemhukumu kwenda kutumikia chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miezi
sita, Salim Suleiman Juma (29) mkaazi wa Mtambwe, baada ya kutiwa hatiani kwa wizi wa mazao.
Mshitakiwa
huyo ametiwa hatiani kwa kosa la wizi wa ndizi mkungu mmoja aina ya Mkono wa Tembo,
wenye thamani ya shilingi 30,000, kwa kukisia mali ya Othman Hamad Ali .
Aidha mbali na adhabu hiyo, pia mshtakiwa ametakiwa
kumlipa fidia ya hilingi 30,000 muathirika wa tukio hilo, ambae ndie mkulima na
mmiliki.
Imeelezwa mahakamani hapo na Mwendesha mashtaka wa
serikali Shaame Farhan Khamis, mbele ya Hakimu Maulid Hamad Ali, kuwa, mshitakiwa
huyo alitenda kosa hilo Aprili 5, mwaka huu majira ya saa 3:30 usiku katika kijiji
cha Kiapaka Mtambwe.
Mshitakiwa huyo amekiri kutenda kosa hilo, baada ya
kusomewa shitaka lililokuwa linamkabilia na hivyo kuamriwa aende chuo cha
mafunzo miezi sita.
Aidha mshitakiwa alitakiwa kulipa fidia ya shilingi 30,000 na akishindwa atumikie chuo
cha mafunzo kwa kipidi cha mwezi miezi mitatu zaidi.
Kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 251 (1)
na 268 (1), (2), (3) vya Shria ya Adhabu
nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.
MWISHO.
Comments
Post a Comment