Skip to main content

''TUNATAKA KUONA WANAWAKE WANAJITEGEMEA' WAZIRI PEMBE

 



Salha ZJMMC@@@@

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe Juma amesema Serikali imeamua kuwawezesha wanawake jasiri ili kuwawezesha kiuchumi na kuweza kujitegemea weneyewe ili kuondokana na hali ya utegemezi katika jamii.

Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya wanawake shupavu wa amali ya Zanzibar yaliyofanyika Bweni katika Chuo cha Ufundi Karume Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Amesema kutoa mafunzo kwa wanawake wenye ujasiri kunaongeza uwezo zaidi wa kuweza kuzalisha bidhaa zao zenye ubora.

Pia ametoa wito kwa wataalamu jasiri wanaopatiwa mafunzo ya kuwa walimu kwa wanawake wengine ambao hawajapata fursa ili kuwawezesha wanawake wengi kuweza kujiajiri na kuondokana na utegemezi katika familia zao.

Hata hivyo ametoa wito kwa wanawake kuwapenda, kuwaongoza, na kuwalinda watoto wote ili kuwasaidia kuepukana na vitengo vya  ukatili wa kijinsia na udhalilishaji.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Kazi na Uwekezaji Maryam Juma Abdalla amesema tayari jumla ya Shilingi Bilioni 26 zimetoka kwa wanawake kwa ajili ya mikopo na kujiajiri.

 



Aida kwa upande wa wadhamini wa mafunzo hayo walisema lengo ni kuwajengea uwezo vijana wa kike ili waweze kuzalisha bidhaa bora na kuendeleza soko na kusafirisha nje ya nchi ya Tanzania.

Mafunzo ya wajasirimali ya siku mbili  yamefadhiliwa na NGO za Tanzania Wormen Chember of Commerce Zanzibar, Mwanamke Initiatives Foundation na Zanzibar Economic Empowerment Agency.

Mwisho

Comments