Chama cha waandishi wahabari wanawake Tanzania Zanzibar
TAMWA,ZNZ kinalipongeza jeshi la Polisi kwa kuchukuwa hatua za haraka
kushughulikia suala la uvunjaji wa maadili lililofanywa hivi karibuni na
kusambaa katika mitandao ya kijamii.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mkurugenzi wa chama cha
waandishi wahabari wanawake Tanzania Zanzibar, TAMWA ZNZ Dk Mzuri Issa amesema kutokana
na tukio lilotokea hivi karibuni na kutoa taswira mbaya ya kimaadili, kinidhamu
na Udhalilishaji nchini, hivyo TAMWA imeliomba Jeshi la Polisi kuwakamata wote
waliohusika na Sheria kuchukuwa mkondo wake.
Amesema TAMWA ZNZ inaomba hatua kali zichukuliwe dhidi ya
wahusika kwa mujibu wa sheria zilizopo ili kuwa funzo kwa wengine wanaotaka
kujaribu na hivyo kulinda mila, silka na maadili ambazo ni moja kati ya tunu muhimu
za Zanzibar.
“Ni dhahiri kwamba vitendo hivyo kamwe havikubaliki na
vinaweza kuleta athari na madhara makubwa ya hivi sasa na baadae katika kuimarisha
yetu na vizazi vya leo na hapo baadae.”
Dk Mzuri.
Aidha TAMWA ZNZ inawaomba wadau wanaosimami masuala ya
utamaduni kufanya kazi kwa mashirikiano ya pamoja na TAMWA katika kuelimisha jamii umuhimu wa
kujiheshimu na kuvaa mavazi ya staha, matumizi sahihi ya lugha ili kujenga
jamii yenye ustaarabu inayolinda na kuheshimu utu wa wanawake, watoto na
makundi yote katika jamii.
Hata hivyo TAMWA ZNZ imetowa wito kwa wanawake na watoto wa
kike kujiheshimu ili waweze kuheshimika katika jamii nzima ya wanawake.
Sambamba na hayo TAMWA ZNZ imeiasa jamii kukomesha vitendo
hivyo na kuwa msatari wa mbele katika kulinda na kufichuwa vitendo vyote
ambavyo vina nia ya kuchafuwa ustaarabu na nidhamu ya maadili na heshima ya
wanawake na jamii kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Sheria ya Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu
na Utamaduni ya 2015 imeeleza majukumu ya Baraza hilo ikiwa ni pamoja na
Kifungu no 7 (b) Kuhifadhi,kulinda na kuimarisha mila, silka
na maadili ya Utamaduni wa Zanzibar
Kifungu no 7 (d) Kulinda sera ya Taifa katika mambo
yanayohusu Sanaa na Utamaduni na kuitangaza sera hiyo.
Ingawa Sheria hiyo ya Baraza la Sanaa na Sensa ya Filamu na
Utamaduni 2015 haijaeleza moja kwa moja kifungu gani ambacho kinamtia hatiani mtuhumiwa
pindi atakapovunja maadili, mila na silka za Utamaduni wa Zanzibar pamoja na
adhabu yake.
MWISHO
Comments
Post a Comment