NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR
Hali ya wanawake, ikiwa pamoja na kushika nafasi za uongozi
zinatafuatiana duniani kutokana na sababu nyingi.
Miongoni mwa hizi sababu ni sera za nchi hizo, sheria, mila,
tamaduni na dhana potofu ya kumchukilia mwanamke kama mtu ambaye haki zake kama
binaadamu hazistahili kuwa sawa na zile za mwanamume.
Matokeo yake ni kuona wanawake wengi wanakosa haki zao
nyingi, ikiwa pamoja na za elimu, urithi , kushika nafasi za uongozi na kuwa na
sauti inayosikika na kuheshimika katka kufanya maamuzi.
Ripoti ya mwaka 2018 inayohusu uwiano wa kijinsia
ulimwenguni imeweka picha halisi ya haki za wanawake katika siasa, uchumi na
elimu ili kuutanabahisha ulimwengu kasoro ziliopo na kuelezea umuhimu wa
kufanyika marekebisho.
Hivi sasa ziaonekana zinafanyika jitihada mbalimbali
kurekebisha dosari hizi ili kuhakikisha mwanamke, anakuwa ni sehemu ya uongozi,
ikiwemo kwenye mambo ya kisiasa kwa vile huko ndiko anapofanyika maamuzi muhimu
ya kimaisha, kisiasa na kiuchumi.
Changamto hizi za kila aina zimekuwa zinawarudiasha nyuma
kutimiza ndoto zao za kuwa na maisha bora na kuwa na maendeleo kwao wao,
familia zao na kwa taifa lao.
Katika kuzizungumzia changamoto hizi, hasa za wanawake wa
Zanzibar kushika za kuwa Wawakilishi wa majimbo, Naibu katibu Mkuu wa Umoja wa
Wanawake Zanzibar Tunu Juma Kondo, alisema jamii haina elimu ya kutosha na ndio maana ni
wanawake wachache wanaojitokeza kutaka nafasi hizo kupitia vyama vya siasa.
Aliwaasa wanawake wenziwe wasibaki kulalamika pembeni, bali
wajishirikishe katika vyama vya siasa na jitihada zao ziwasaidie kufungua
milango ya kuwaptia uongozi wa majimbo.
Mwanasiasa kutoka chama cha Wananchi (CUF), Nadhira Ali
Haji, alisemakwa bahati mbaya jamii inamuangalia mwanamke kwa dharau na hivyo kuona hawezi kuongoza.
Katika uchaguzi mkuu wa miaka miwili iliyopita wapo wanawake
walojitokeza kugombea uongozi kwenye
majimbo, lakini kutokana na changamoto zilizowakuta baadhi yao walikata tama ya
kuendelea kutaka nafasi hizo za uongozi.
Mtumwa Feiz Said, Naibu Mkurugezi wa Chama cha ADC, alisema
amepata changamoto mbalimbali wakati wa kugombea jimbo la Mfenesini katika
chaguzi za mwaka 2015 na 2020 .
Hio ni pamoja na vitisho mbalimbali vilioambatana na kupigwa,
hali ambayo ilimkatisha tamaa ya kuendelea kugombea uongozi.
Mdau wa masuala ya
wanawake na uongozi, Said Suleiman Ali, alisema moja ya njia itayowasaidia
wanawake kupata haki yao ya kuwa viongozi katika majimbo ni kuwa wamojana
kujipangia mkakati utaowavusha daraja hili kwa salama.
Miongoni wa maeneo yanayotakiwa kufanyiwa kazi ni la
kuepukana na ubaguzi unaotakana na tafauti zao za vyama.
Eneo hili hivi sasa linafanyiwa kazi na tasisi mbali mbali
za kitaaluma na kiraia kwa lengo la
kuwainua wanawake kuwa viongozi na moja ya taasisi hizo ni Jumuiya ya
Wanasheria wanawake (ZAFELA).
Mratibu wa mradi wa kuwainua wanawake katika uongozi (SWIL),
Khamis Ali Rashid, alisema changamoto moja kubwa inayopeleka wanawake kutopata
nafasi za uongozi mifumo ya vyama vya siasa.
" SWIL
tulishanya mikutano zaidi ya 100 kwa lengo la kuwasaidia wanawake, kuweza
kuwatatulia changamoto hizo,’’alisema.
Mmoja wa wanasiasa ambae hakuta jina lake litajwe
alipendekeza ofsi ya msajili wa vyama
vya siasa sasa iweke sheria inayolazimisha mfumo wa uongozi wa juu wa chama
uwendane na usawa wa kijinsiaKwa mfano, Mwenyekiti akiwa mwanamume Katibu wa
chama awe mwanamke..
Ofisa kutoka Idara ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar, Suhaila
Abdallah Saleh, alisema wanajikita
katika harakati zitazopeleka wanawake kujpatia nafasi zaidi za uongozi.
"Tunawashajihisha kwa kuwapa elimu, ikiwemo juu ya
kuzingatia ushiriki wa wanawake na kuwajengea uthubutu watoto wa kike ili
wafikie malengo yao," aliongeza.
Mwanasheria wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Zanzibar,
Fatma Haji Mohamed, alisema wnatumia njia tafauti ambazo zitawasaidia wanawake
kuondokana na changamoto zinazowakabili.
" Sheria ya vyama vya siasa Zanzibar ni ya muda mrefu
na sasa hivi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan,
amelekeza pafanyike taratibu za kurekebisha sheria mbalimbali za vyama vya
siasa,’’alisema.
Mwaka jana vikao vya Kikosi kazi vilipokea malalamiko ya
wanawake ya kuwepo nafasi finzu kwa wanawake
kushiriki katika nafasi za uongozi katika vyama na hatimaye ndani ya
serikali.
Mkurugezi wa Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Thabit Idarous Faina,
alisema katika majimbo 50 ya Wawakilishi
wa kuchaguliwa wanawake ni wanane tu.
Anasema wabunge wanawake wanaowakilisha Zanzibar ni wanne
tu, sawana asilimia 8, huku mawaziri wakiwa sita, sawa na asilimia 33 na
makatibu wakuu ni saba, sawa na asilimia 39.
Kwa upande wa wakuu wa mikoa, mwanamke ni moja tu , swa na
asilimia 20, wakuu wa wilaya ni wanane, sawa na asilimia 36 na masheha wanawake
ni 68, sawa na asilimia 17 kwa masheha wote ambao ni 389.
Mwisho
Comments
Post a Comment