NA NUSRA
SHAABAN
Wahamasishaji jamii(CBs) pamoja na
wanakamati walio katika mradi wa Kuongeza Ushiriki wa Wanawake kwenye Masuala
ya Uongozi na Demokrasia (SWIL), unaofadhiliwa na Ubalozi wa Norway nchini
Tanzania, wameibua mjadala huo kufuatia kikao kilichoandaliwa na Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar
(ZAFELA) katika ukumbi wa Skuli ya
Turkey Mpendae Zanzibar.
Kikao hicho, kimewapa fursa wanakamati
hao pamoja na Wahamasishaji jamii hao,
kuwasilisha ripoti zao za ufuatiliaji wa changamoto za kijamii na utendaji kazi
wao kuanzia mwezi Januari 2023 mpaka Juni 2023.
Jumla ya ripoti kumi
zimewasilishwa na kuibua mijadala
tofauti inayohusu wanawake na uongozi.
Miongoni mwa maeneo yaliyozua mjadala
mkubwa ni suala la wanawake wanaotaka kugombea nafasi za uongozi kuambiwa vyeti
vyao ni feki.
Akielezea kwa undani juu ya changamoto
hiyo, Bi Sabahi Bakari Hassan, Mhamasishaji jamii kutoka Wilaya ya Kati, alisema kwa
wanawake waliopo Wilaya ya kati changamoto hiyo ya vyeti inaonesha imewaathiri
kwa kiasi kikubwa kwani hupata
usumbufu wa kutofikia malengo wanayokusudia hasa ikizingatiwa cheti cha
kuzaliwa kina umuhimu wake katika harakati za mwanamke na uongozi.

Comments
Post a Comment