NA ABUU BAKAR, ZU@@@@
MWANI ‘sea weeds’ ni aina ya zao, lenye mnasaba na kiumbe hai, kinachopatikana baharini pekee.
Kwa
uasili wake viumbe hawa, huota na kukua kwenye fukwe zenye asili ya mawe au
mchanga mzito, nyasi za baharini na kwenye matumbawe.
Kwa karne mbili na nusu zilizopita, zao la mwani,
halikubeba thamani yake, na lilionekana kama vile ni bustani ya habarini yenye
lengo la kuwapendezesha viumbe kama samaki.
Kwa
kule kucheza cheza kwao, kufanya mazalio, nyumba, sehemu za mapunziko na
chakula kwa baadhi ya viumbe.
Ilionekana,
kama vile mwani ni viumbe vinayoota na kufa kila baada ya muda, na hakuna
aliyefikiria kuwa, iko siku zao hilo linaweza kuwa sehemu ya kukuza pato la mtu
au taifa.
Baada
ya kuonekana kuwa na thamani, sasa wataalamu wanatueleza kuwa, ziko aina mbali mbali
za mwani, ambazo hutofautiana kutoka ukanda mmoja wa bahari na mwingine.
Kwa
mfano Tanzania, kuna aina mbili kuu za mwani, ule unaoitwa “Eucheuma
denticulatum” au kwa jina jingine hujulikana kama “Eucheuma spinosum” na
aina ya pili inaitwa “Kappaphycus alvarezii”.
Kwa kwaida mwani huwa na rangi ya kijani,
kahawia na nyekundu, ambapo rangi hizo zinasababishwa na kuongezeka au kupungua
kwa kina cha maji ya bahari.
Wizara
ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, imeanisha kuwa, uzalishaji wa zao la
mwani umeongezeka kutoka, tani 10,531 kwa mwaka 2021 hadi tani 12,594 kwa mwaka
2022 sawa na ongezeko la asilimia 20.
Taarifa
ikafafanua kuwa, usafirishaji wa mwani nje ya nchi umeongezeka kutoka tani
12,124 kwa mwaka 2021 hadi tani 13,972 mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia
15.
CHANGAMOTO ZIPI WANAZOZIPATIA WA
KULIMA WA MWANI?
Mkulima
wa zao hilo kutoka shehia ya Sizini Salma Khamis Juma, anasema hulazimika
kufanya jitihada binafsi, ili kuupata mwani, ikiwemo kutembea kwa miguu kwa
kuvuuka sehemu zenye hatari.
Changamoto
nyingine anasema, sehemu wanazopita kutafuta mwani zina kuwa na tope na visiki vinavyochoma
mithili ya misumiri, ambapo huwakumba wao, wasio na viatu vya kinga.
‘’Mwani
hata ukifika nao juu kwa ajili ya kuuwanika, umeshapitia kadhia kadhaa, na wakati
mwengine unaweza kushindwa kurudia siku nyingine kwa miguu kupata
majeraha,’’anaeleza.
Haisau
siku aliyongia kwenye dimbwi lenye tope, na kuzama mpaka magoti, wakati anarudi
kuvuna mwani shambani kwake, na kuokolewa na mwenzake.
Mkulima
Raya Ali Bakar wa Shehia hiyo ya Sizini wilaya ya Micheweni, anaeleza kuwa, kama
sio shujaa wa kweli, ni vigumu kwa mwanamke kujiingiza kwenye kilimo cha mwani.
Anaona
kuwa machungu, shida, kadhia ya kuuza roho inayowakabili wakulima wa mwani, ni
vyema ikaenda samba mba na bei husika.
‘’Sisi
wanawake ambao tumejiingiza kwenye kilimo cha mwani, ni sawa na kuuza maisha
yetu kila siku, na huku ukiangalia bei nayo inaumiza kama matayarisho ya kilimo
chenyewe,’’anaeleza.
Ali
Salim Bakar, anaeleza kuwa kilimo cha mwani hawezi kukifafanisha na kilimo
chochote chenye tija na taifa, kutokana na ugumu uliopo wakati wa matarisho
yake.
Kule
kulimwa ndani maji, kushughulikiwa ndani ya maji na hata kuvunjwa ndani ya maji
ni ishara kuwa, kilimo hicho kinaishi pamoja na changamoto zake.
‘’Kila
mmoja anasema kama akipata kazi nyingine anaweza kukihama kilimo cha mwani,
maana machungu ni makubwa ingawa bei haiendani na kazi zake,’’anaeleza.
Zainab
Ali Bakar, anasema ukosefu wa vifaa kinga, vidau vya kusafirishia mwani, bei na
wizi unawakosesha furaha katika kazi yao ya kilimo cha mwani.
UONGOZI WA SHEHIA YA SIZINI
Sheha
wa shehia ya Sizini Suleiman Shaame Hamad, anasema wakulima wengi wanaoendesha
kilimo hicho ni wanawake, hivyo ni vyema wakaangaliwa kwa jicho la huruma.
‘’Naelewa
kuwa, kwa sasa serikali inayomikakati kabambe ya kuhakikisha, wakulima wa mwani
wanasahau machungu wanayopata kwenye kilimo hicho,’’anaeleza.
Sheha
anawakumbusha wakulima wa zao hilo, kuwa nao watakuwa juu kama walivyowakulima
wa zao la karafuu, hasa baada ya uwepo wa kiwanda cha kusarifia mwani Chamanangwe.
Afisa
Uvuvi Wilaya ya Micheweni Abdalla Issa Nassor, anasema kuwa wakulima
wanakabiliwa na changamoto nyingine inayowakabili wakulima hao ni ya maradhi
kwa mwani wao.
Jambo
hilo hufanya mwani kuharibika, na kuwafanya wakulima wa zao hilo, kutokufikia
malengo yao waliyojiwekea.
Kutokana
na changamoto hizo miradi mbali mbali imeanzishwa kuwasaidia vikundi tofauti, ikiwemo
mradi wa IUCN ambao makao makuu yake yapo Dar es Salam, ambapo mradi huo
husaidia sehemu mbili kwa Pemba, Mkoani na Micheweni.
Kwa
upande wa Micheweni Umesaidia kikundi cha Mikoko, kinachoitwa Shirikani
Coparetive Society, kikundi cha Ufugaji wa samaki kinachoitwa Mapambano
Coparetive Society na kikundi cha mwani Tuelewane kilichopo kinowe.
SERIKALI KUU INASEMAJE
Waziri
wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleiman Massoud Makame anasema kwa mwaka huu wa
fedha, mkazo zaidi umewekwa kwenye maendeleo ya viwanda vya kusarifu samaki,
mwani na mazao mengine ya bahari.
Aidha anasema machungu wanayoyapata wakulima
wa mwani wa Unguja na Pemba, yataondoka karibuni kuwatafutia mikakati ya
vitendo iliyowekwa na serikali ya awamu ya nane, ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha
kusarifia mwani.
Akisoma taarifa ya kitaalamu wakati mwenge wa
uhuru ulipotembelea Juni mwaka 2023, Mkurugenzi mkuu Kampuni ya mwani Zanzibar
Massoud Mohamed Rashid, anasema ujenzi wa kiwanda hicho umefikia hatua nzuri.
Alieleza
kuwa, ujenzi huo ambao unajengwa na Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar
‘KMKM’ uko katika awamu ya kwanza, kati ya zile tatu hadi kukamilika kwake.
Alieleza
kuwa, awamu ya kwanza inajumuisha ujenzi wa jengo kuu la kiwanda, ujenzi wa
ghala pamoja na uzio maalum kwa ajili ya kulihifadhi eneo hilo.
‘’Awamu ya
pili utajumuisha ujenzi wa maeneo ya bustani, ufungaji wa mitambo husika na
awamu ya tatu ni kuanza uzalishaji bidhaa zitokanazo na mwani,’’aliwaeleza
wakimbiza mwenge kitaifa.
Kwa wakati
huo, tayari ujenzi huo wa awamu ya kwanza umeshafikia asilimia 86, na
ukitarajiwa kutumika shilingi bilioni 8.2 ingawa wameshatumia shilingi bilioni
4.024 na utakapomalizika wote, utagharimu shilingi bilioni 13.
‘’Mradi huu
wa kiwanda, utakapomalizika utakuwa na uwezo wa kusarifu mwani tani 30,000 kwa
mwaka, ambapo umiliki wake kwa asilimia 55 utakuwa serikalini na asilimi 45
utakuwa wa kampuni ya Nutri-san.
Taarifa
kutoka wizara ya Uchumu wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, zinaeleza kuwa, usafirishaji wa mazao ya baharini ikiwemo matango bahari, mwani,
dagaa, kaa na pweza umeongezeka kutoka tani 19,063 mwaka 2021 hadi tani 23,158
mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 21.
Uzalishaji wa zao
la mwani nao umeongezeka kutoka tani 10,531 mwaka 2021 hadi tani 12,594 kwa
mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 20.
Huku pia
ikianishwa kuwa, usafirishaji wa mwani nje ya nchi umeongezeka kutoka tani
12,124 mwaka 2021 hadi tani 13,972 mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 15.
Mwisho
Comments
Post a Comment