NA
TATU NAHODA, ZU@@@@
……………fuata
nyuki ule asali…………….
Ndivyo walivyosema wahenga, wakimaanisha kuwa, unapaswa
kufuata vitu, watu au sehemu zenye ujuzi, ili kufanikiwa katika malengo yako.
Msemo huu
unatumika katika nyanja nyingi ikiwemo ya wanafunzi wanaofuta elimu, hasa kwa
mfumo wa kupitia maktaba ziwe na skulini au maeneo mingine.
Maktaba ni hazina pekee inayomtajirisha mwenye
kuhitaji utajiri wa kitaaluma na kimaarifa, kwani mtumiaji hapitwi na wakati,
na hupata taarifa muhimu juu ya mambo mbali mbali.
Kwa wanafunzi na walimu wao, maktaba imekuwa ni
hazina yao ya thamani, kama alivyosema mtaalamu Marcus Tallus Cicore "if
you have a garden and library you have everything you need " ukiwa
na tafsiri isiyorasmi kuwa, kama una
bustani na maktaba basi tayari una kila kitu.
KWANINI
MAKTABA NI MUHIMU SKULINI?
Ahmed Khamis Ahmed mwanafunzi wa kidato cha pili skuli
ya Madrasatul-Ahbaab Kisauni Unguja anasema, maktaba kwake ni suluhisho la ufumbuzi
wa kielimu na maarifa.
Kwani, anaona ni chanzo cha upatikanaji wa vifaa
vya kujifunzia, kama vile vitabu, majarida na vifaa vyengine vinavyohusiana na
tasnia ya elimu na masomo yao kwa ujumla.
"Maktaba ni hazina isiyochakaa, ambayo
utajiri wake unajitokeza kwa kila mmoja wetu, na kwa kadri ya kila mmoja wetu
anavyoitafuta elimu na kujifunza,”anasimulia.
Wanakuwa wanajifunza vitu vipya, ambavyo
hawakupata kufundishwa kwa upana madarasani na walimu wao, na hivyo huamua
kwenda zao maktaba na kujisomea, ili kuongeza maarifa zaidi.
Salum Issa Salum na mwenzake Aziza Hassan Mzee wanaosoma
kidato cha nne skuli ya Mtambile Mkoani, wanasema wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Amali, imefanya jambo jema, kujenga kituo cha maktaba skulini kwao.
"Kwa sasa ni tofauti na zamani, ambapo
tulilazimika kuzifata huduma za maktaba mji wa Chake Chake, jambo lililotuwiya
vigumu kutokana na masafa yalivyo,’anasema Salum.
Asia Kassim Daru mwanafunzi wa kidato cha sita
skuli ya Dk. Salmin Amour ya Chumbuni Unguja, anasema maktaba huhimiza
utamaduni wa kujifunzia stadi za maisha na kuwatia moyo, ili waendelee kutafuta
maarifa zaidi ya masomo yao.
"Kupitia Maktaba hasa wanafunzi tunaotarajia
kufanya mitihani yetu ya taifa, maarifa huongezeka, mithili ya chem chem
jangwani, kwani tunapata weledi wa kujibia mitihani hiyo," anaeleza.
Kwake Maktaba ni msaada mkubwa, kwani ni sehemu
inayoleta amani, utulivu na umakini, ambao unafaa katika mazingira ya kujisomea,
na hata kumpa uwezo mzuri wa kufikiria, juu ya masomo yake.
Mwanafunzi
Makame Nahoda Juma, wa kidato cha tano skuli ya Mwanakwerekwe ‘C’ iliyopo wilaya
ya Magharibi ‘B’ Unguja, anaeleza kuwa, Maktaba ni fursa pekee ya kupata
taarifa za kielimu na kijamii bila ya kujali hali ya kijamii na kiuchumi.
"Wanafunzi walio wengi hali zao za kiuchumi
ni ndogo, hivyo hawamudu baadhi ya mahitaji ya skulini, kama vile ununuzi wa vitabu
ambavyo wanapaswa kuwa navyo, katika masomo yao,"anafanua.
WAALIMU
Kama maneno ya wahenga walivyosema,"mwalimu
ni mwanga wa maarifa katika giza la ujinga, hii ikiwa na maana walimu hutoa
muongozo na elimu kwa wanafunzi wao.
Mwalimu mkuu wa skuli ya Mtambile Mkoani Pemba,
Abrahman Hassan Bakar, anasema kuwepo kwa vituo vya maktaba katika skuli
huchochea ongezeko la ufaulu.
Mwalimu huyo anafafanua kwa kutoa mfano kuwa,
kati ya wanafunzi 200, hivyo wastani wa wanafunzi 150, huingia maktaba kufanya
kutafuta maarifa zaidi ya kielimu.
Anaeleza kuwa, ujio wa maktaba hasa skulini
kwake, kama vile umekuja kuwaamsha na kuchochea wanafunzi, kwanza kujisomea
zaidi, kupata maarifa na mbinu za kujibia mitihani ya taifa.
Akaeleza kwa mfano kuwa, kwa mwaka 2022 skuli hiyo
ilifaulisha wanafunzi 26, kuingia kidato cha tano, na kuvunja rikodi ya historia
ya skulini hapo.
"Kwa mara ya kwanza, skuli imeongeza ufaulu
wa wanafunzi, ikiwa miongoni mwa kichocheo kikubwani ni uwepo wa Maktaba skulini hapa,"anasimulia.
Hivyo, akawagawageukia wanafunzi wa skuli mbali
mbali, kutumia maktaba zilizomo skuli mwao, ili ziwasaidie kupata ufahamu na
ujuzi wa mada mbali mbali, zilizomo kwenye mtaala.
Mwalimu Hafidh Said Ali na mwenzake Zakia Ali
Abdallah, wanasema maktaba za skuli hazisaidii wanafunzi pekee, bali na wao
kwani, huingia maktaba kupata maarifa zaidi kabla kuingia madarasani.
"Maktaba skulini zimezaa matunda ya elimu,
sio tu kwa wanafunzi wetu lakini hata kwa sisi walimu wao, maana tunazitumia
kabla na hata baada ya kusomesha masomo yetu,"wanaeleza.
Hapa Msimamizi wa Maktaba skuli ya Mtambile Amina
Said Salum, anaeleza kuwa, kuwepo kwa maktaba, kumesaidia kuinua kiwango cha ufaulu
kwa wanafunzi, katika masomo yao mbali mbali.
Mkutubu Sabra Abdallah Nassor, katika maktaba ya
skuli ya Almadrastul-ahbaab ya ya Kisauni Unguja, anaeleza kuwa, muamko wa
wanafunzi katika skuli hiyo, kuhudhuria maktaba ni mkubwa.
Anasemea kwani wanafunzi wanaohudhuria ni zaidi
ya 30, kwa kila wanafunzi 40, kutoka madarasa tofauti tofauti yakiwemo yale
wanaojitayarisha na mitihani ya taifa.
Katibu wa Jumuiya za kukuza Maktaba za skuli
Zanzibar Abbas Mohamed Omar, anaeleza kuwa, kuwepo kwa maktaba skulini ni suala
zuri, kwani husaidia wanafunzi, kuondoa changamoto zao za kielimu na maarifa.
Anaeleza kuwa, skuli nyingi za sekondari za
Zanzibar, zimekuwa na maktaba, ingawa suali la kujiuliza je, maktaba hizi
zinakidhi haja za watumiaji wake?.
Anaona kuwa, Maktaba nyingi za skuli za sekondari,
hazikidhi haja za watumiaji wake, kutokana na kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa
ni pamoja na baadhi zao, kukosa wakutubi wenye sifa.
‘’Kwa kweli wizara ya Elimu, imejitahidi
kuhakikisha kuwa, kila skuli ya sekondari inakuwa na Maktaba, lakini bado vifaa
vya kutosha ni changamoto mpya,’’anaeleza.
HALI YA
MAKTABA ZA SKULINI
Kwa mujibu wa Shirika la Huduma za Maktaba
Zanzibar, linaeleza kuwa, ni skuli 40 pekee kati ya kila skuli 100, ndizo
ambazo zina maktaba na 60 hazina.
Ingawa kwa upande wa skuli za sekondari za
Zanzibar, imebainika kuwa, kila skuli 100, basi 70 zinahuduma ya maktaba na 30
pekee, bado hazijafaidika na huduma hiyo.
Takwimu hizi zinaonesha kuwa, suala la maktaba
bado halijapewa umuhimu wake, unaostahili katika skuli za msingi, skuli ambazo
kama jina lake lilivyo, zinatarajiwa kumjengea msingi madhubuti wa mwanafunzi.
MWISHO.
Comments
Post a Comment