RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amewataka Wananchi ambao sio raia halali wa Tanzania kufika katika Ofisi za Uhamiaji kwa lengo la kujiorodhesha ili waweze kutambulika rasmi katika nchibya Tanzania.
Aliyasema
hayo wakati wa kukabidhi vyeti vya Uraia Tanzania kwa Tajnisi hoko ikulu katika
Mkoa wa Mjini Unguja, ambapo alisema baaadhi ya wanachi wanashi Tanzania bila ya utambulisho wowote .
"Nawaomba Wananchi ambao kwa namna moja au nyengine hawajafika
kwenye Ofisi za Uhamiaji kujiorodhesha, ni vyema wakaitumia fursa hiyo ili
waweze kutambuliwa rasmi. Serikali zetu zimedhamiria kulimaliza tatizo hili
kutokana na athari zake." alisema Dk
Mwinyi
Pia alisema Jumla ya wananchi elfu tatu mia tatu na kumi na
tisa 3,319 wamekabidhiwa vyeti vya uraia wa Tanzania tajnisi Ikiwemo
Msumbiji,Comoro,Burudi na Ruwanda.
"Kwa hakika, nchi,
yetu leo inaandika historia mpya ya kulikamilisha jambo hili kubwa la kuwapa
uraia ndugu zetu ambao tumekuwa tukiishi nao kwa zaidi ya miaka 50 sasa wakiwa
na asili ya mataifa jirani ya Burundi wakiwa raia
watano 5 , raia wa Comoro mia moja na
aroubaini na saba 147, raia wa Msumbiji thalathini na
mmoja elfu miamoja na kumi na sita 3116 na raia wa Rwanda 1".
alisema dk Mwinyi
Pia
ametoa shurkan kwa Uongozi wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya nchi na Jeshi la
uhamiaji kwa kuhakikisha linasimama na
timia zoezi hilo
" Natoa shukurani kwa
Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Jeshi la Uhamiaji kwa namna
walivyolishughulikia na kulisimamia jambo hili hadi leo tumefikia hatua ya
kuwakabidhi vyeti vya Uraia ndugu zetu hawa." alisema Dk Mwinyi
" Kwetu sisi
Serikali zote mbili tumefurahia sana kuona kuwa hatimae suala hili limekamilika
kama ambavyo binafsi nilitoa ahadi ya kulishughulikia baada ya kuingia
madarakani mwaka 2020. Leo napata faraja kuona kuwa dhamira njema ya Serikali
na ndoto ya muda mrefu waliyokuwa nayo ndugu zetu hawa, imeweza kutimia ambapo
kumalizika kwa zoezi hili kuna wafanya tuwatambue kuwa Raia wa Tanzania badala
ya Wahamiaji wasiohamishika." aliongezea Dk
Mwinyi
.Aidha alisema ni vizuri kushirikiana kwa
pamoja katika kuleta amani ya nchi bila kuleta vurugu kwa lengo la kutopoteza
hadhira ya serekali.
"Matumaini yangu kuwa mtaipata heshima inaystahili hadhi ya
kuwa raia raia wema,Kwa hakika ndugu zangu mna wajibu wa kuendeleza utiifu wenu wa sheria na
kujiepusha na vitendo viovu ili msipotoshe dhamira njema ya Serikali ya
kukupeni uraia wa Tanzania. Kwa pamoja tushirikiane katika kulinda na kudumisha
amani tuliyo nayo kwa faida yetu tuliopo sasa na wale watakaokuja baadae." alisema Dk Mwinyi
"Hivi sasa mataifa
mbali mbali duniani yanaendelea kuimarisha sheria zao za uhamiaji na uraia kwa
lengo la kudhibiti uingiaji, ukaaji na utokaji wa watu ili kulinda mipaka na
kuhakikisha amani na usalama katika mataifa yao." alieleza Dk Mwinyi
Aidha ametoa wito kwa Idara ya Uhamiaji lenye dhamana ya
masuala ya uhamiaji nchini, kuendelea kuziimarisha sheria zilizopo hususan
Sheria ya uraia wa Tanzania. Sheria hii haijafanyiwa mapitio kwa kipindi
kirefu, hivyo huu ni wakati mwafaka wa kuiangalia upya kwa madhumuni ya
kuiwezesha kukabiliana na changamoto mbali mbali zinazowahusu wananchi na
wageni wanaofika hapa nchini.
Naye
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Yussuf Masauni alisema kutokana na busara
za viongozi ,Raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein
Ali Mwinyi Pamoja na Raisi waJamuhuribya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluh
Hassan wameamua kuwasamehe zaidi ya bilioni 6 waliotakiwa kulipa na kupewa
uraia bure.
"
Serekali ya Mapinduzibya Zanzibar pamoja na Serekali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania imetoa msamaha kwa raia hao kwasababu walitakiwa kulipa zaidi ya
bilioni sita 6 kwa kukaa hapa bila ya kutambulika na imeamua kuwapa uraia bure
bila ya harama yoyote. " alisema Haji yussuf
Naye Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania Dkt. Anne Peter Makakala alisema jumla ya wahamiaji wasiohamishika elfu tatu na mia tatu na kumi na tisa 3319 wakiwemo wanaume 676, wanawake 968 na watoto 1675 walikizi vigezo vya kupatiwa uraia wa Tanzania wa TAJINISI.
Vilevile
amesema serikali zote mbili zimeridhia maombi hayo kwa sharti la kukamilisha
taratibu za uraia kwa mujibu wa kanuni ya Tanzania ya 2017.
Pia
alisema wameanzisha mfumo wa kielektronik
uliotengenezwa kwa wataalam wa ndani kwa ajili ya kutengeneza vyeti hivyo ili
kuepusha udanganyifu na kutunza kumbukumbu za Wahamiaji ao.
Comments
Post a Comment