Na Mwandishi wetu, @@@@
Dhana ya kupanga uzazi kama haki ya binadamu ni muhimu. Inapinga maoni yoyote potofu kwamba ni aina ya udhibiti wa idadi ya watu na itahakikisha kwamba vizazi vijavyo kamwe havichukui haki hii ya kibinadamu iliyopatikana kwa bidii kuwa ya kawaida.
Katika kuhakikisha huduma za afya ya uzazi zinafikiwa kwa urahisi, mafunzo ya siku tatu kuhusu SRHR yalifanyika kwa waandishi wa habari, uhamasishaji ulifanywa kwa siku mbili, na vyombo vya habari vilijengewa uelewa kuhusu SRHR ikiwa ni pamoja na uzazi wa mpango.
Hata hivyo, pamoja na mafanikio yaliyopatikana, bado kuna changamoto katika upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi.
Kwa mfano, ingawa upatikanaji wa uzazi wa mpango ni haki ambayo inapaswa kufurahiwa na wote, lakini sio wote wanaofaidika na haki hiyo.
Na ingawa ni wazi kuwa uzazi wa mpango unachangia katika kupunguza vifo vya uzazi na kuhakikisha kuwa akina mama na watoto wachanga wanakuwa na afya njema, wanandoa wengi bado wananyimwa haki ya kupanga uzazi na wapenzi wao.
Wanaume wamekuwa kikwazo cha kufikia malengo ya kitaifa kwa sababu wanasitasita kuwaruhusu wake zao kutumia njia za kupanga uzazi na hata kutishia talaka.
Hata hivyo, kama elimu ya uzazi wa mpango itawafikia wanaume wengi zaidi basi lengo la kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga ungekuwa na mafanikio makubwa zaidi.
Tunapaswa kujua kwamba kwa kila shilingi inayotumika kupanga uzazi serikali inaweza kuokoa maisha ya mama na mtoto na kufanya uzazi wa mpango kuwa mojawapo ya uwekezaji wa gharama nafuu nchini.
Uzazi wa mpango unatoa fursa kwa wanawake na vijana kuchagua lini na mara ngapi kupata watoto lakini pia wasichana wengi zaidi wanaweza kubaki shuleni na wanawake wengi wanaweza kuamua kuingia au kubaki katika uchumi.
Mashirikia ya kimataifa kama UNFPA yameendelea kuongeza uwekezaji wa kitaifa katika huduma za uzazi wa mpango na huduma za afya ya uzazi, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa huduma za kupanga uzazi, huku ikiunga mkono juhudi za kupanua wigo wa vituo vinavyotoa huduma za kisasa za uzazi wa mpango na kuimarisha ubora wa huduma hizo.
Lengo la UNFPA, miongoni mwa mengine, ni kupanua upatikanaji wa taarifa na huduma kwa vijana na makundi mengine yaliyo hatarini.
Kufikia malengo ya maendeleo endelevu ifikapo 2030, kunategemea ni kwa kiasi gani haki za afya ya uzazi zinazingatiwa.
Utimilifu wa mahitaji ya wanawake na wasichana ya kupanga uzazi ni mojawapo ya uwekezaji wenye faida zaidi kwa Zanzibar.
Dk Ali Omar Ali kutoka wizara ya afya, anasema uzazi wa mpango ni haki ya binadamu wote na ni muhimu huduma bora uzazi wa mpango zipatikane na kufikiwa kwa urahisi.
Sheikh Abdullah Talib, Katibu Mtendaji wa Wakfu na Maliamana, anasema kuwa uzazi wa mpango unakubalika katika uislamu na unaruhusu familia kujitengenezea mazingira bora ya kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kiafya pamoja na kuweka mazingira bora zaidi ya elimu kwa watoto wao.
Anatoa wito kwa jamii kushikamana na ukweli/mafundisho ya kidini na kutosikiliza imani potofu.
ReplyForward |
Comments
Post a Comment