NA NAFDA HINDI, ZANZIBAR@@@@
KUKOSEKANA kwa vipimo vya kupimia maambukizi
yanayosababisha ukimwi (HIV Kits) Zanzibar ni jambo linalowarejesha nyuma
vijana kujitokeza katika vituo vya Afya kupima afya zao.
Hayo yamebainika kufuatia ziara iliofanywa
na Chama Cha Waandishi wa habari Tanzania TAMWA,ZNZ wakati wa kutembelea vituo
vya Afya na huduma Rafiki kwa vijana vilivyopo Wilaya ya Kati na Magharibi “B”.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti watoa huduma
za Afya kutoka vituo mbali mbali wamesema licha ya vijana kuwa na mwamko wa
kujitokeza kwa wingi katika vituo vya Afya kupima afya zao kwa sasa imekuwa ni
tofauti kwa kukosekana vipimo vya maambukizi ya virusi vya ukimwi ambapo
huvikimbia vituo hivyo.
“Idadi ya vijana ilikuwa iko juu na
inaongezeka kwa kasi kupima Afya zao katika kituo chetu hasa virusi
vinavyosababisha ukimwi ila kwa sasa kila leo idadi inapunguwa kutokana na
tatizo la kutokuwepo vipimo vya kupimia maambukizi hayo,(HIV KITS), “ Mtoa
huduma kituo cha Afya Mwera.
Tatizo hilo la kukosekana kwa vipimo vya
kupimia virusi vya Ukimwi limedhihirika kwa takribani vituo vinne vya Serikali
kutoka Magharibi “B” na Kati kwa Unguja ikiwemo Mwera, Fuoni, Tunguu na
Magirisi kilichopo Taveta ambapo huduma hiyo hupatikana bila ya malipo.
“Kwa sasa kuna upungufu wa HIV kits kwa
wateja wetu, isipokuwa tunatowa upendeleo kwa mama wajawazito tuu ndo
wanaofaidika na huduma hii kwa sasa,”Daktari Kiongozi Kituo cha Afya Fuoni,
Sultani Shella.
Kijana amabae alifika katika Kituo cha Afya
Magirisi kilichopo Taveta Meli Nnne kufuata huduma Rafiki kwa vijana amesema kukosekana
kwa kipimo hicho athari inakuwa kubwa hasa kwa vijana kwa kutokujuwa Afya zao
na hatimae kuleta majanga kwa jamii.
“Athari ni kubwa kwa vijana, kwa sababu
ukitaka kufunga ndoa lazima upime HIV kama hakuna kipimo tutaumia na kuumiza
familia hata Taifa kwa ujumla kwa kutokujuwa nani ni muathirika wa magonjwa
hayo na utazidi kusambaza kwa wengine,” Kijana kutoka Meli Nne.
Hata hivyo kituo Afya Mwera kilichopo Wilaya ya Kati Unguja kinachohudumia Shehia ya Magharibi “A” na
Koani licha ya kutoa huduma Rafiki kwa vijana, kinatowa huduma mbali mbali
zikiwemo Uzazi wa mpango,Ushauri Nasihi, na huduma za mama wajawazito na kwa mwezi
huzalisha wajawazito wasiopunguwa mia moja na hamsini.
Mmoja kati ya mteja anaepata huduma kutoka
kituo cha Mwera Maryam Abdalla Bakar amesisitiza wanawake kuhudhuria clinic
mapema wakati wa kujigunduwa ni wajawazito kwa lengo la kujuwa maendeleo yao na
kujikinga na matatizo yanayoweza kujitokeza.
Nae Mratibu wa Mradi wa kuendeleza utetezi kwa vyombo vya habari juu ya Afya ya Uzazi kwa wanawake na wasichana kutoka TAMWA,ZNZ Zaina Abdalla Mzee amesema ziara hiyo ya kutembelea vituo vya Afya ina lengo la kugundua changamoto na kuziwasilisha kwa wahusika na kupatiwa ufumbuzi.
“Tunafanya ziara hii kwa lengo la kuvijuwa
vituo vya Afya na vinavyotoa huduma Rafiki kwa Vijana vilivyopo Wilaya ya
Magharibi “B” na Kati kujuwa changamoto zinazovikabili vituo hivyo na kutafutiwa
ufumbuzi kwa wahusika,” Zaina Abdalla Mzee, Mratibu wa kuendeleza utetezi kwa
vyombo vya habari juu ya Afya ya Uzazi kwa wanawake na wasichana kutoka
TAMWA,ZNZ.
Afisa muelimishaji na muhamasishaji kwa vijana kutoka Wizara ya Afya
Zanzibar, Kitengo Shirikishi cha Afya ya Uzazi mama na mtoto Fatma Ussi Yahya anasema wanatoa elimu kupitia
vyombo vya habari kwa mama wajawazito kuhudhuria clinic mapema kwa kujuwa
maendeleo yao na changamoto zinazowakabili ili kuzitatuwa mapema.
“Sisi tunahamasisha vijana kupima Afya zao
na muitikio ni mkubwa, kwa sasa Chanagamoto za uhaba wa vipimo vya kupimia
virusi vinavyosababisha Ukimwi (HIV KITS) la muda mrefu kiasi kwa Wilaya zote
kwa Pemba na Unguja,” Afisa muelishaji na muhamasishaji vijana kutoka Wizara ya
Afya, Fatma Ussi Yahya.
Mradi wa kuendeleza utetezi kwa vyombo vya
habari juu ya Afya ya Uzazi kwa wanawake na wasichana wa mjini na vijijini
unafanywa kwa Wilaya ya Kati na Magharibi “B” kwa Uguja na Chake chake kwa
Pemba unatekelezwa na TAMWA.ZNZ kwa ufadhili wa Wellspring Philanthropic
Fund(WPF) ya Marekani.
MWISHO
Comments
Post a Comment