NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WAANDISHI wa habari nchini,
wamesisitizwa kujikita katika kuandika habari za uchunguuzi, ambazo kwa kwaida
huisaidia jamii, katika kupata haki na kukuza uhuru wao wa kujieleza.
Akifungua
mafunzo ya siku moja leo Machi 14, 2023 kwa njia ya kielektroniki ya zoom, wakati akifungua
mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari, Msimamizi wa vyombo vya habari
kutoka Internews Alakok Mayombo kupitia mpango maalum chini mradi wa Boresha
habari, unaotekelezwa na Intrernews Tanzania.
Alisema,
njia ya waandishi wa habari kujikita katika kuandika habari za uchunguuzi, ndio
ambazo huibua changamoto kwa jamii na kuimarisha uhuru wa kujieleza.
Alieleza kuwa,
katika eneo la utawala bora, haki za binaadamu, jinsi na afya hasa eneo la
Covid 19, ambalo linahitaji kuangaliwa kwa kina, ili jamii itambua haki zao.
Alifahamisha
kuwa, bado jamii inavitegemea vyombo vya habari, kuandika habari kwa kina na
zenye tija, ili kujua wajibu wao, haki zao pamoja na changamoto zilizopo.
‘’Waandishi
wahabari nyinyi ambao meingia katika mafunzo haya maalum, Internews imewaamini
na bila shaka, na nyinyi mtaifanya kazi hii kwa kina,’’alieleza.
Katika eneo
jingine, Msimamizi huyo wa vyombo vya habari kutoka Internews Alalok Mayombo,
alisema vyombo vya habari, bado vitaendelea kuwa tegemeo kwa jamii husika.
Mkufunzi wa
mafunzo hayo, mwandishi mkongwe Erick Kabendera, alisema habari za kina ‘uchunguuzi’
zinahitajika kufanywa kwa utulivu na tahadhari kubwa.
‘’Mara zote
unapoandika habari za ukweli, huweza kukuletea madhara ikiwe kifo, kuwekwa
chini ya ulinzi, kwani wanaoandikiwa huwa hawapendi, aibu zao zinatoka nje,’’elieleza.
Hata hivyo
amewataka waandishi hao wa habari, kuwashirikisha wengine ili kupata jicho la
pili, kwani habari inajengwa makundi mbali mbali.
Katika hatua
nyingine alisema, kinga pekee kwenye habari za uchunguuzi ni kuandika habari za
ukweli na zenye ushahidi, ambapo kufanya hivyo wengine watawajibishwa.
Aidha amewahimiza
waandishi kujisomea kwa kina, kwani jukumu lao ni kuandika na kusoma zaidi ili
kuandika habari zenye tija.
Wakitoa maoni
yao, waandishi hao wa habari, wameahidi kuyafanyia kazi mafunzo, na kwa
kuandika habari za kina, ili kuimarisha utawala bora na uhuru wa maoni.
Mwandishi Denis Nyali, alisema sasa ameelewa kuwa, sio kila tukio linaweza kuwa habari ya uchunguuzi, kama halikutimia vigezo husika.
Nae Chelu Matuzya, alisema kweli kuna umuhimu mkubwa wa mwandishi wa habari kusoma zaidi, ili kuwa mweledi wa kuandika habari za uchunguuzi.
Faraja Masinde, alisisitiza kuwa, bado kuna umuhimu wa kwa waandishi w ahabari kuendelea kufuatilia kwa karibu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hsabu za serikali, ili kupata vyanzo vyengine vya kuandika.
Mwisho
Comments
Post a Comment