Joyce Joliga,Tunduru
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Tanzania Dkt. Oswald Masebo alitoa ushauri mzito wa kuyataka Mabaraza ya Mila na Desturi kutumia matamasha ya kumbukizi yatumike kukemea vitendo vya unyanyasaji Watoto, wenye umri wa siku 0 hadi miaka 8
Watoto hao wanekuwa wajikutana na vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji ,ulawiti ambavyo vimekithiri kwenye jamii ili kujenga jamii bora ambayo inaenzi mila na Desturi za kitanzania.
Kadhalika ameyataka Mabaraza ya Mila na Desturi kukemea vitendo vya ushoga ambavyo vimekithiri nchini vikiwemo na vitendo viovu vinavyokwenda kinyume na mila na desturi ya mtanzania.
Ikumbukwe kuwa Ushauri huu wa Dkt.Masebo ametoa ushauri huo kwenye kongamano la kumbukizi ya mashujaa wa vita ya Majimaji lililofanyika kwenye ukumbi wa Crasta mjini Tunduru.
Kongamano hilo ni sehemu ya kumbukizi ya miaka 118 ya mashujaa wavita ya Majimaji waliuawa na wajerumani Februari 27,1906 kwa kunyongwa mashujaa 67 na wajeruamni katika eneo la Songea Klabu na kuzikwandani ya makumbusho yaTaifa ya Majimaji Mahenge Songea.
Taifa lipo katika vita ya kupambana na watu wanaoharibu mila nadesturi za mtanzania ambapo kumekuwa na mmomonyoko wa maadili kwa Watoto na vijana.
“Hivi sasa vitendo vya ukatili kwa watoto wadogo hasa wenyeumri chini ya miaka 8 ,ubakaji,ulawiti vinatishia maishaya watoto wetu ni jukumu la Wazee kutumia matamasha haya kuelimisha jamii kuacha vitendo hiyo ,pia vitendo vya kishoga ambavyo ni kinyume na mila na desturi zetu vimekuwa tishio kubwa kwa vijana wetu,hivyo tunapofanya kumbukizi kama
hii ya mashujaa wa vita ya Majimaji inatakiwa sote kukemea kwa nguvu
zote ili kulinusuru Taifa kuingia kwenye janga kubwa la mmomonyoko wa
maadili’’,alisisitiza Dkt.Masebo.
Siyo siri kumekuwa na vitendo vingi vya matukio ya unyanyasaji watoto ambavyo vinakiuka haki za watoti na haki za Binadamu,Kesi zinaendelea .
Akizungumza wakati wa ufungaji kongamano hilo ambalo lilishirikisha wadau mbalimbali kutoka mkoa wa Ruvuma ,Wizara ya Maliasili na Utalii na watoa mada kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam,mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tunduru .Ngollo Malenya ameipongeza Wizara kwa kufanya kongamano hilo kwa mara ya kwanza katika wilaya ya Tunduru.
Licha ya kauli hii vitendo vya ukatili wa watoto wadogo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara ambapo vimeacha kumbu kumbu mbaya kwa jamii hasa yenye watoto waliofanyiwa ukatili.
Katika kongamano hilo mapendekezo mbalimbali yalitolewa ikiwemo mapendezo ya kurejeshwa hapa nchini malikale zote za Mkoa wa Ruvuma zilizopo nje ya nchi na wanafunzi katika shule za sekondari na vyuo kila
mwaka kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kwenye matamasha ya mila na utamaduni ili kurithisha historia ya Tanzania.
Ni zairi kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuenzi mila na Desturi za Mababu zetu kwani zimesaidia kuwa na taifa lenye amani,upendo na mshikamano nalimesaidia kuwana wananchi wenye umoja,ambapo kwenye matamasha hayo kumesaidia pia kujenga urafiki inakuweza kujifunza mambo mbalimbali ya kale, pamoja nakuelekezana vyanzo vya maendeleo kiuchumi
katika kongamano hilo Mada mbalimbali ziliwasilishwa zikiwemo kutoka kwa wahadhari wa chuo kikuu cha Dar es salaam na Wataalam wa Makumbusho ya Taifa zikiwemonafasi ya ndumba katika vita,urithi na utamaduni wa wangoni na utamu wa historia ya Mkoa wa Ruvuma.
Kilele cha miaka 117 ya kumbukizi ya mashujaa 67 wa vita ya Majimajikinatarajiwa kufanyika Februari 27,2023 katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji mjini Songea ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa
Maliasili na Utalii.
Hivyo Basi kuna haja ya Wazazi walezi,pamoja na Jamii kwa ujumla kuenzi kwa vitendo matamasha haya kwa kufata mila na desturi za mababu zetu ili tuwe na jamii salama na kuweza kuwalinda na manyanya,Ukatili wa kingono watoto wetu kwa ajili ya urithi wa taifa la kesho.
mwisho.
Comments
Post a Comment