Joyce Joliga, Tunduru:::
WANAFUNZI wa Shule za Msingi Namasimba na Makoteni Katika kata ya Ligoma wanajisaidia Porini kutoka na shule zao kutokuwa na vyoo jambo ambalo linahatarisha afya zawanafunzi hasa wenye umri wa miaka 5-8 endapo utatokea ugonjwa wa mlipuko wa homa za matumbo katika eneo hilo .
Hayo yalisemwa na Diwani wa kata ya Ligoma Mmala Abdalah Mmala wakati akiongea kwenye kikao cha baraza la Robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kilichofanyika katika ukumbi wa Claster ya walimu wa tarafa ya mlingoti mnjini hapa.Akifafanua taarifa hiyo Mmala alisema kuwa kutokans na hali hiyo kipindi cha kiangazi waanchi walijitolea kuchimba vyoo vya muda katika maeneo ya shule hizo lakini kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha wanafunzi wanaogopa kuendelea kuvitumia vyoo hivyo kwa kuogopa kutumbukia.
Alisema ,kufutia hali hiyo Mmala akatumia nafasi hiyo kutokana na taarifa alizo nazo katika shule hizo kuna vifaa vilibakia wakati wa ujenzi wa madarasa ya mradi wa uviko hivyo anaimba Halmashsuri kuridhia vifaa hivyo vitumike kwa ajili ya uimarishaji wa miundombinu hiyo ili kuondoa adha hiyo.
Kwa mujibu wa Diwani huyo vifaa hivyo ni pamoja na mifuko ya Saruji,matofari ,Rangi , Michanga na Kokoto.
Nae Diwani wa kata ya Lukumbule Omar Ghaib Hilal akatumia nafasi hiyo kueleza kuwa pia katika eneo lake wanafunzi wa Shule ya sekondari Lukumbule wanajisaidia Porini hasa nyakati za usiku kutokana na mabweni yao kutokuwa na huduma hiyo.
Alisema kinacho umiza zaidi watoto hao wamekuwa wakilazimika kwenda kujisaidia katika vyoo vilivyopo upande wa pili wa madarasa hali ambayo imekuwa ikihatarisha afya hasa kipindi hiki cha mvua ambapo endapo yatazuka magonjwa ya mlipuko.
Alisema sambamba na hali hiyo pia kitendo cha wanafunzi kutoka nje na kwenda kujisaidia porini au eneo hilo ambalo lipo mbali na enep la mabweni wanayo lala kuwa ni hatari kwao kutokana na eneo hilo kuwa na wanyama wakali wakiwemo Simba,Tembo, Nyoka na Chui.
Akihitimisha hutuba ya kamati ya fedha uongozi na mipango makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Said Bwanali pamoja na mambo mengine aliwataka wataalamu watembelee maeneo yaliyo bainisha ili kutafuta ufumbuzi
Aidha alitoa maelekezo kwa kuwataka Diwani aitishe kikao na kuandika barua ya kuomba kubadilisha matumizi ya vifaa vilivyo tajwa kubakia kwenye mradi wa ujenzi wa madarasa ya uviko ili utekelezaji ufanyike
Kuhusu vyoo ambavyo vilitanjwa kufuata choo upande wa pili aliigiza viongozi wa idara ya Elimu sekondari kufanya ufutiliaji na kutafuta ufumbuzi wake.
Mwisho
Comments
Post a Comment