NA HAJI NASSOR, UNGUJA:::
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Katiba,
Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Haroun Ali Suleman, ameiagiza Idara
ya Katiba na Msaada wa Kisheria kwa kushirikiana na tasisi ya LSF, kukutana
kila baada ya miezi mitatu, ili kuona maazimio 16 yaliobuliwa kwenye jukwaa la
msaada wa kisheria yanafanyiwa kazi.
Alisema,
Zanzibar imekuwa hodari wa kuanzisha mambo na kisha kuyaweka kwenye karatasi
bila ya kufanyiwakazi, lakini kwa hayo maazimioa 16, lazima wajitahidi
kuhakikisha wanayatekeleza.
Waziri
Haroun ameyasema hayo Disemba 14, 2022 wakati akilifunga jukwaa la pili la
Msaada wa Kisheria Zanzibar, lililoandaliwa na Idara ya Katiba na Msaada wa
Kisheria Zanzibar kwa ufadhili wa LSF na kufanyika Chuo cha Utalii Maruhubi
Unguja.
Alieleza kuwa,
kila baada ya miezi mitatu anahitaji kupata ripoti ya utekelezaji wa maazimio
hayo, ili kuona waliolengwa wanufaika nayo.
‘’Mhakikishe
Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria kwa kushirikiana na wadau wenu LSF, na
mimi nitawaita kuanzia mwezi Machi 2023 kujua mliyofanya,’’alieleza.
Aidha waziri
Haroun, alipendekeza kuwa jukwaa la tatu la Msaada wa kisheria ni vyema
likafanyika kisiwani Pemba, ili washiriki kutoka Unguj,a wapate kujifunza mambo
mbali mbali kisiwani humo.
Alieleza
kuwa, anaamini Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria kwa kushirikiana na LSF,
wakikaa pamoja, wanaweza kufanikisha suala la jukwaa hilo, kufanyika kisiwani
humo.
Kwa upnde
wke Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar Hanifa Ramadhan
Said, alieleza kuwa, katika kongamano hilo, kumeibuliwa maazimio 16.
Alieleza
kuwa, moja kati ya hayo LSF kuendelea kusadiana kuwajengea uwezo watendaji wa
Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria, pamoja na kufunguliwa kwa ofisi za
wasaidizi wa sheria katika ofisi ya wilaya.
‘’Kuhakikisha
kuandika ripoti za utendaji kazi, kwa kugusia malengo 17 endelevu ya dunia, ili
kuonesha muitikio wa jamii pamoja na kuimarisha mifumo itayohakikisha taifa
linakuwa na raia wema,’’alifafanua.
Azimio
jengine ni kwa Idara hiyo, kuhakikisha inachukua juhudi za kuratibu na kufanya
marekesbisho ya sheria ya Msaada wa Kisheria, ili kuweka mfuko wa taifa wa
Msaada wa kisheria.
Aidha
Mkurugenzi huyo alisema azimio la 15 ni kuongeza kasi ya mafunzo ya usuluhishi
na utatuzi wa migogoro kwa wasaidizi wa sheria.
‘’Natarajia
tukikutana tena kwenye jukwaa la tatu la msaada wa kisheria hapo mwaka 2023,
yawe tayari haya yameshatekelezwa kwa kadiri itakavyoamuliwa,’’alieleza.
Afisa
Mtendaji mkuu wa taasisi la LSF Deogratus Bwire, alisema wamefarajika kuona
kuwa, bado Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria inaendelea kushirikiana kwa
karibu.
Awali
wakichangia mada kwenye jukwaa hilo, Msaidizi wa sheria wilaya ya kusini Unguja
Ahmed Haji Mkema, alisema wanafunzi wa sheria, baada ya kumaliza chuo, wamekuwa
na uwelewa mdogo.
Hata hivyo alisema
lazima kituo cha msaada wa kisheria ‘legal aid clinic’ kilichopo ndani ya
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kizidi kujitangaaza, ili wanafunzi
wakifahamu.
Mapema
akiwasilisha mada ya elimu ya saikolojia kwa wahanga wa matendo ya udhalilishaji,
wakili Ali Rajab, alisema lazima wasaidizi wa sheria, wajifunze elimu hiyo.
‘’Inawezekana
kuna mtoto ameshadhalilishwa na hakuna hata kesi yake moja iliyopata hatia,
sasa saikoloji yake ni mtu wa kudhalilishwa, na hasikii tena elimu, ushauri
wala msaada wa kisheria,’’alifafanua.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ Harusi Miraji Mpatani, akichangia
mada alisema, vyama vya wanasheria, lazima viongeze nguvu, ili jamii ipate
msaada.
Alieleza
kuwa, msaada wa kisheria umewalenga wale watu maskini zaidi, hivyo lazima
viongozi wa vyama na wale wanasheria, wanawasaidie wananchi.
‘’Hapa
mawakili wa kujitegemea, lazima sasa tujitolee kuzisimamia kesi bila ya kujali
malipo ‘probono cases’ na huo ndio mchango wetu kwa jamii,’’alishauri.
Nae mdau wa
sheria Sabaha Bakar Hassan, amesema bado elimu inahitajika kwa jamii, ili kufahamu
vyema, dhana ya msaada wa kisheria.
Nae sheha wa
shehia ya Chumbuni Hassan Juma Juma, aliwataka mawakili kuanzisha utamaduni
kama wa kukutana na wananchi ngazi ya kijiji, ili kutoa elimu kwao.
Hata hivyo
Afisa sheria wa Vyuo vya mafunzo Zanzibar, Seif Maabad Makungu, amewshauri
mawakili wasiziache kesi njiani, ambazo wameshalipwa na watuhumiwa.
Hili ni
jukwaa la pili la msaada wa kisheria Zanzibar, kuandaliwa na Idara ya Katiba na
Msaada wa Kisheria kwa kushirikiana na LSF, ambapo ujmbe wa mwaka huu ni uimarishaji
wa huduma bora na endelevu za utoaji wa msaada wa kisheria Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment