HAJI
NASSOR NA ZUHURA JUMA, PEMBA:::-
JESHI la
Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, linamshikilia mtoto wa miaka 16, aliyetoa
taarifa ya kubakwa na daktari Is-haka Rashid Hadid, na kisha maelezo hayo, kuyakana
ndani ya mahakama wa mkoa Wete.
Hayo yamekuja, wakati kesi yake ikiendelea, alipotakiwa kutoa
ushahidi mahakamni hapo, ingawa alipinga vikali kubakwa kwake na mtuhumiwa
huyo.
Mtoto huyo alitoa ushahidi mahakamani, ambao ni tofauti na na
maelezo yake ya awali, aliyoyatoa kituo cha Polisi, ndipo Mwendesha Mashitaka
Juma Mussa, alipotoa maelekezo ya kushikiliwa kwa mtoto huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Juma Sadi Khamis,
amekiri kupokea mtoto huyo (awali aliyedai kubakwa na daktari Is-haka),
kwa tuhuma za kuidanganya mahakama.
‘’Ni kweli juzi tulimpokea mtoto wa miaka 16, ambae anadaiwa
kutoa ushahidi wa uongo mahakamani, na kisha kuyakana maelezo aliyoyatoa awali
kituo cha Polisi,’’alisema.
Ilibainika mahakamani hapo kuwa, awali hakimu aliombwa
kumpeleka rumande mtoto huyo, lakini alikataa na ndipo wakili anayeshughulikia
kesi hiyo, akaomba kwa jeshi la Polisi limshikili kwa hatua nyingine.
Kamanda huyo alisema, anamkumbuka vyema mtoto huyo, kwamba
miezi miwili iliyopita, alihojiwa kituoni hapo na kumtaja daktari Is-haka
Rashid Hadid, kwamba ndiye aliyemtorosha na kumbaka mara tatu.
‘’Juzi nashangaa kwamba, alitakiwa kutoa ushahidi juu ya tuhma
hizo, lakini alipofika mahakamani aliyakana maelezo yake, na kudai daktari huyo
sie aliyembaka,’’alieleza.
Hivyo kamanda huyo wa Polisi mkoani humo, amewataka watoto
waache tabia ya kutaja kila mtu, wanapokumbwa na vitendo hivyo, na badala yake
wawatej wahusika.
‘’Polisi alimtaja daktari, lakini mahakamani amegeuka ‘shahidi
kigeu geu’ hivyo ameletwa na taratibu zikikamilika atafikshwa kwenye
mahakama ya watoto, kujibu tuhma hizo,’’alifafanua.
Mwendesha Mashtka Juma Mussa, wakati akimuongoza shahidi huyo (mtoto),
alionekana dhahiri kuyakana maelezo yake, akiwa mahakamani hapo.
‘’Kama pana askari wa kike aje mahakamani amchukue mtoto huyu ‘shahidi
kigeu geu’ ampeleke kituo cha Polisi na afunguliwe mashataka kwa
kuidangaya serikali,’’alisema.
Alisema kuwa, mwanzo alianza vizuri kutoa ushahidi wake,
ingawa alipokuwa akiendelea alibadilisha na kusema yale ambayo hakuyasema kituo
cha Polisi, ndipo akaamua kumfungulia mashitaka.
Wakili huyo aliwataka wazazi na walezi, wawe tayari kutoa
ushirikiano wa dhati kwa Serikali katika kutoa ushahidi wa kesi za
udhalilishaji, ili kuzikomesha katika jamii.
Licha ya mtoto huyo kuyakana maelezo hayo, lakini kesi ya
msingo bado inaendelea kwenye mahakama ya mkoa Wete na tayari wazazi wake
wawili wameshatoa ushahidi.
MWISHO.
Comments
Post a Comment