NA HAJI NASSOR, PEMBA
TIMU za soka za mahakama kuu Pemba,
na ile ya wazee ya mji wa Chake chake, zimeshindwa kutambiana kwenye mchezo
maalum, wa kuisindikiza siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria
Zanzibar, mchezo uliopigwa uwanja wa Polisi Madungu jioni.
Katika
mchezo huo, uliohudhuriwa na watazamaji wengi kiasi, ulianza kwa kasi, ili kila
tumu iondoke na ushindi uwanjani hapo.
Dakika ya 22,
nusura timu ya Mahakama kuu Pemba, ijipatie goli la kuongoza, baada ya
mshambuliaji wake Adam Abdalla, kuachia fataki zito langoni mwa timu ya wazee,
ingawa liliokolewa na mlinda mlango wao, Said Mohamed.
Dakika 45 za
awali, zilimalizika kwa kosa kosa za hapa na pale, na kipindi cha pili,
kilianza kwa kasi na mashambulizi ya kushtukizia kila upande.
Dakika 79,
baada ya timu ya wazee kugongeana vyema, na kisha mpira kumfikia Saleh Said, aliburura na kuwapiga chenga
walinzi wa mahakama, ingawa shuti lake, lilikuwa chakula mbele ya mlinda mlango wao Abubakar Ali.
Timu ya
mahakama, itapaswa kujilaumu yenyewe, baada ya kupata penalti, na mpigaji kuitoa
nje senti mita chache, na mchezo kumalizika kwa kutofungana goli lolote.
Akizugumza
baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Jaji mkaazi wa mahakama kuu Pemba Ibrahim
Mzee Ibrahim, aliitaka timu ya mahakama, kuiendeleza timu yao.
Alisema, sio lazima kucheza michezo ya kujipima nguvu kwa kusherehekea siku ya sheria pekee, bali hata kwenye shughuli nyingine.
“Timu haina
mazoezi ya kutosha, lakini imecheza vizuri, sasa ni vyema ikaendelezwa, ili
vipaji tulivyonavyo vije vitumike kwa mashindano mbali mbali,’’alieleza.
Kwa upande
wake, Naibu Mrajisi msatafu wa mahakama kuu Pemba, Abdull-razaki Abdaull-kadir
Ali alisema, pamoja na mambo mengine, lakini mchezo ni sehemu ya kuagwa kwake.
“Kama
twengefungwa, basi kuniaga kwenu ingekuwa mumeniaibisha, lakini kama kutoka nguvu
sawa, mmeniaga kwa salama na amani,’’alifafanua.
Nahoza wa
timu ya mahakama kuu Pemba Adam Abdalla, alisema kukosa mazoezi ya kina na uzoefu
ndio sababu ya timu ya wazee kuondoka salama.
Nae mlinzi
wa timu ya wazee wa Chake chake Ghalib Bedui, alisema umakini hafifu wa
wafungaji wake, ndio sababu ya kukosa ushindi.
Mwisho
Comments
Post a Comment