NA HAJI NASSOR, PEMBA::: KIJANA Gizahibu Ali Amour miaka 38 aliyekatwa miguu yote miwili, miaka mitatu iliyopita kwa tuhma za wizi, shehia ya Pujini wilaya ya Chake chake, amepona na kupata ulemavu wa kudumu. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia simu, Januari 8, 2023 alisema licha ya kuwa bado yuko hai, lakini amepata ulemavu wa kudumu na kulazimika kutembelea miguu ya bandia. Alisema, mguu mmoja wa bandia aliununua kwa shilingi 400,000 ambapo kwa hatua za awali alichangia na ndugu na jamaa, marafiki na madaktari katika hospitali aliyokuwa amelazwa. Alieleza kuwa, sasa ni mwaka mmoja, tokea atoke hospitali na kutumia miguu ya bandia, na imeanza kumbana na kuanza kuisaidia kwa mgongo mawili. Kijana huyo alieleza kuwa, kama hakupata usaidizi tena, anachokiona mbele yake, ama ni kubakia nyumbani muda wote au kutembelea magongo, kwenye safari zake ndogo ndogo. ‘’Kwani nipo nyumbani na ilikuwa natembelea vyema miguu yangu ya bandia, lakini sasa imeshaanza kucha...