NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WAZAZI na walezi wa kijiji cha Kidutani, shehia ya Chumbageni Wambaa wilaya ya Mkoani Pemba, wameahidi kuiunga mkono kamati ya maadili na taaluma ya kijiji hicho, ili kuwadhibiti vijana kutojiingiza katika vigenge visivyo na tija, kwa maisha yao ya leo na kesho.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo, walisema mkakati ulioanzishwa na kamati ya muda, wa kuhakikisha wanawarejesha wanafunzi madrasaa, skuli na kuingia kwenye ibadaa ni wazo zuri, kwani manufaa yake ni makubwa.
Walieleza kuwa, wazo hilo, ni vyema kila mzazi na mlezi, kukubaliana na mauelekeo wa kamati hiyo, kwani imekuja kusaidiana malezi ya pamoja, na hasa yenye kufangamana na mwenendo, tabia na mafundisho ya dini ya kiislamu.
Mmoja katia ya wazazi hao Shaibu Pandu Makame, alisema katika kufanikisha lengo hilo, huu ni wakati wa kuungan na kusahau tofauti zao walizonazo.
Alieleza kuwa, suala la malezi katika karne hii limekua gumu, hasa baada ya kila mzazi, kutaka kumlea mtoto wake, ingawa hujitokeza ugumu.
āāTulipoteleza kwamba, kila mzazi amlee mtoto wake, ndio matunda yake ni haya, sasa kama kuna wenzetu wameamua kuanzisha ushirikiano huo, ni vyema tukawaunga mkono,āāalifafanua.
Kwa upande wake mzazi wake, Time Makama Ussi, alifafanua kuwa, kama wazazi wakikubali kuwa kitu kimoja, inaweza kuwa rahisi kwa jamii nzima, kufikia malengo yao.
Nae mzazi Zainab Omar Juma, alisisitiza haja kwa wazazi wenzake, kushirikiana katika jambo hilo, kwani linaweza kuzaa matunda makubwa ya malezi ya watoto wenye maadili na nidhamu.
Mapema Mwenyekiti wa muda wa kamati hiyo, Saleh Abdalla Mohamed, alifahamisha kuwa, suala la kutafuta elimu, ni wajibu kwa kila mmoja, na hilo ni miongoni mwa mambo yanayosimamiwa na kamati yake.
āāTunakusudia kwa wale waliokatisha masomo iwe ya madrassa au skuli na hata walioacha kufanya ibada tutakutana nao pamoja na wazazi, ili kuona wanarejea,āāalifafanua.
Katibu wa kamati hiyo Machano Ali Makame na mlezi wa Jumuiya hiyo, Amini Haji Makame aliwawataka vijana waliotoroka madrassa, skuli na kuacha kufanya ibada, kurejea haraka, kwani kanuni dhidi yao zinaandaliwa.
mwisho
Comments
Post a Comment