NA KHAULAT SULEIMAN,PEMBA
KATIKA harakati za kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi, jitihada za akina mama zinazidi kwa kuandaa mbinu, ambazo zitasaidia katika kukabiliana na janga la mabadiko ya tabia ya nchi.
Mabadiliko ya tabia ya nchi yanazidi kujitokeza siku hadi siku, kiasi ambacho husababishwa na shughuli za kibindamu, ikiwemo ukatwaji wa miti ya juu na ile ya pembezoni mwa bahari.
Ambayo kisayansi yametajwa kuwa, husaidia kuzuiya upandaji wa maji juu ama kufika katika sehemu za makazi ya wanachi.
Mabadiliko ya tabia ya nchi (climate change) ni mwenendo wa hali ya hewa yakiwemo majira, wastani na vizio vya juu na chini kabisa vya joto, utokeaji na mtawanyiko wa mawingu, mvua na theluji.
Zipo athari kadhaa ambazo zinasababishwa na hali hiyo, ambayo huathiri jamii na nchi kwa ujumla.
Moja wapo ni ongezeko la nyuzijoto, na kasi ya matukio mabaya mno ya hali ya hewa kuanzia kwa mawimbi na joto, ukame, mafuriko, dhuruba za msimu wa baridi, vimbunga na mioto ya mwituni.
Mnamo mwaka 2019, shirika la hali ya hewa ulimwnguni (WMO), linasema joto la wastani ulimwenguni lilikua 1.1, juu kuliko kipindi cha kabla ya ujenzi wa viwanda.
Linasema mwaka huo huo ilihitimishwa muongo wa joto la kipekee ulimwenguni, kupungua kwa barafu na uswa wa bahari, kutokana na gesi za ukaa zinazozalishwa na shughuli za binadamu.
WMO likaenda mbali na kufafanua kuwa, watu 30 kila 100 ulimwenguni kote, wanakabiliwa na wimbi baya la joto yanayotokezea zaidi ya siku 202 kwa mwaka.
Mkufunzi wa kilimo msitu chini ya mradi wa mabadiliko tabia nchi Zanzibar ZANZADPT, unaoendeshwa na Jumuima ya uhifadhi wa misitu CFP, Fatma Ali Mgwali wa shehia Kiuyu Minungwini, anasema kilimo hicho ni himilivu.
Kilimo msitu ni kilimo ambacho ni mchanganyiko wa mazao mbali mbali, kama minanasi, michikichi migomba, njugu, mahindi, mbazi na miembe, kinasaidia kuhimili na kulinda upotevu wa hali ya hewa.
Mkufunzi na mkulima wa shehia Mjini kiuyu Ridhiki Ali Juma, anategemea kupata mvuno mfululizo, wakati wa msimu wa mavuno ukianza.
āBaada ya kupewa elimu na CFP, ili niwape na wenzangu, nilianza kuotesha shamba la kilimo msitu na sasa nna minanasi, michikichi, migomba pamoja na mboga mboga kwenye eneo dogo,āāanasema.
Wanasema faida nyingine ya kilimo msitu ni kupata miti kwajili ya kuni, mbao matunda, kurutubisha undogo, malisho ya mifugo dawa za asili na usindikaji wa bidhaa zinazotokana na mazao ya misitu
WANUFAIKA WA MRADI
Fatma Shaban Mohamed ni mkulima wa kilimo msitu mkaazi wa Kiuyu minungwini ambaye alihamasika katika kilimo hicho.
āMradi huu ulitufikia mwezi wa tatu , tulianza mafunzo na kulima minanasi 1625 ,miche ya miparachi ambapo awamu ya kwanza ilikua sita kwa kupiga matuta umwagiliaji wa maji āāanasema.
Hidaya Khatib Hamad mkaazi wa Kambini bandani anaeleza kuwa, kupitia kilimo msitu kinaweza kusaidai wanawake kujikwamua kimaisha.
āMwanzo niliona kilomo hichi kitanikwamisha katika shughuli zangu nyingine na kukatishwa tamaa kua hakina faida yoyote na ipo miradi mbali mbali ambayo inakuja, ingawa hatupati faida, kupitia kilimo msitu tunaona faida na tutaweza kufikia malengo yetu.
WANAUME WANASEMAJE
Khatibu Suleiman Juma Katibu wa kamati ya uhifadhi wa shehia ya Kambini, amesema kamati imezingatia kuweka idadi kubwa ya wanawake kwenye kamati kuliko wanaume ili kuwapa kipaumbele.
āKatika kutoa mchangao kwa wanawake kushiriki na kutoa mamuzi kwa kupaza sauti zao, ili kuweza kusikika,āāanasema .
Khatib Omar , mjasiriamali mkazi wa Mjini kiuyu aliwashauri wanaume ambao bado wapo nyuma katika uwelewa wa kuwashirikisha, kuwapa nafasi uhuru wa kufanya shughuli za kujikwamua kimaisha.
TAMWA
Chama cha wandishi wa habari wanawake TAMWA Zanzibar, nao husimama kidete katika tetea haki za upatikanaji wa usawa wa kijinsia, na kuwashirikisha wanawake.
Kaimu Mratibu wa chama hicho, ofisi ya Pemba, Amina Ahmed amesema ,wameona bado kuna nafasi kwa wandishi wa habari kupaza sauti zao kwenye mabadiliko ya tabia nchi.
āāTulishirikiana na CFP na CFI lakini tutahakikisha sauti za wanawake zinasikika katika zote shehia nne ambazo zimefika mradi kwa kupaza sauti zao, kwenye mabadiliko tabia nchi,āāanaeleza.
CFP
Mkurugenzi wa Jumuiya ya uhifadhi ya misitu Pemba, Mbarouk Mussa amesema, athari mbali mbali za ukataji wa miti ya mikoko kwa shughuli mbali mbali za kijamii, zimekuwa zikijitokeza katika maeneo tofauti huku jumuiya hiyo ikiendelea kutoa elimu.
Nae Saada Juma Afisa kilimo kutoka CPF, amesema mradi umelenga watu wote hauja bagua na lengo ni kuwainua wanawake katika shughuli za kujitafutia kipato.
āāShughuli za ugawaji wa mbegu za kilimo msitu katika shehia( 4 ) hufanyika kika baada ya miezi minne, ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa mbegu hizo kwa walengwa,āāanaeleza.
Afisa Mdhamini Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Pemba, Mhandishi Idris Hassan Abdulla amefafanua kuwa ,wameanda mpango maalum wa kuhakikisha, wanazalisha kupitia kilimo msitu kwa kuchanganyisha miti tofauti.
Uharibifu wa mazingira na rasilimali zilizopo pamoja na kushauriana na wadau kuona ni kwa namna gani tatizo hilo linaondoka
MWISHO.
Comments
Post a Comment