NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
JUMUIYA ya tahafidhi qur-an kanda ya Wambaa na Chumbageni wilaya ya Mkoani, imewashukuru waumini wote na taasisi nyingine, kwa michango yao, iliyofanikisha mashindani yao ya tano ya tahafidh qur-an, yaliyofanyika hivi karibuni.
Akizungumza kwenye kikao cha tathmini, kilichofanyika almdarsaatul- imaniya Chumbageni, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ustadhi, Hassan Othman Khamis, alisema pamoja na kujipanga kwao, lakini michango ya wadau, ilisaidia kufanikisha shughuli hiyo.
Alisema kuwa, umoja na mshikamano waliopewa na jamii ya Chumbageni na Wambaa, ni vyema ukawa endelevu kwani, wanamalengo ya kuendesha mashindani mingine makubwa, hapo mwakani.
Alieleza kuwa, bila ya wanajamii kufanikisha michango yao, isingekuwa rahisi wao, kufikia malengo na kuendesha mashindani hayo ya tano kwa mwaka huu.
āāKwa hakika michango ya fedha, vifaa na zawadi nyingine zilizotolewa na wanajamii, ilisaidia mno kunogesha mashindani yetu, na tunawapa shukran watu wote,āāalifafanua.
Hata hivyo, amwapongeza viongozi wenzake wa Jumuiya, kwa moyo wao wa kujitoa wakati wote wa maandalizi, kuanzia siku ya kwanza hadi kwenye kilele husika.
āāHasa wazazi wa kiume, tunawashukuru mno kwa kuhudhuria kwao, maana kwa mwaka jana, walikuwa wachache mno, jambo ambalo lilitukatisha tamaa kama wanajumuia,āāalifafanua.
Hata hivyo, amezikaribisha madrassa nyingine kutoka nje ya shehia za Wambaa na Chumbageni, kujitokeza kushirikiana na jumuiya yao, ili kuongeza idadi ya madrassa hapo mwakani.
āāNi kweli kwa awamu tano mfululizo, hatujawahi kupata madrasaa nje ya shehia zetu mbili, lakini kwa mwakani tunazikaribisha madrassa nyingine, ili kuongeza idadi kutoka saba, walau kufikia 10 mwakani,āāalifafanua.
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wa shehia za Wambaa na Chumbageni, walisema mashindani ya mwaka huu, yalikuwa mazuri mno, ikilinganishwa na mwaka jana.
Wakati huo huo Nnaibu Mwenyekiti wa kamati hiyo, ustadhi Awesi Abdalla Ali, amesema wanakusudia kuendesha uchaguzi wa viongozi wapya wa jumuia hiyo, mapema mwezi ujao.
Alieleza kuwa, walikuwa wanasubiria kumalizika kwa mashindani hayo, na kuitisha uchaguzi mwingine, ambao ni takwa la kikatiba.
āāMwanzoni mwa mwezi ujao, tutakutana kwa ajili ya kupanga mikakati na kuendesha uchaguzi, ili jumuiya ya tahafidhi qur-an ya kanda ya Wambaa na Chumbageni, ipate viongozi wapya,āāalieleza.
Nao wajumbe wa kamati hiyo, wamewakumbusha viongozi wa jumuia hiyo, kwa mwakani, kuanza maandalizi mapema, ili mashindani hayo yazidi kuwavutia wengi.
Raya Juma Khamis, alisema kama sikuchelewa kuanza maandalizi kwa mwaka huu, wengepata asilimia 100 ya mafanikio, kwa mashindani hayo.
Mashindani ya tano ya tahafidh qur-an kanda ya Wambaa na Chumbageni, yalifanyika mwezi 22 ramadhan, katika msikiti wa ijumaa Chumbageni na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Mkoani Dk. Hamad Omar Bakar.
mwisho
Comments
Post a Comment