NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
WIZARA ya
Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imewatahadharisha wazazi, walezi na vijana
wanaosubiri ajira za uwalimu, kuwa makini kwani, kwani matapeli wanaweza
kuingilia kati zoezi hilo.
Wizara hiyo
imesema, matapeli wanaweza kuwahadaa wazazi, walezi au wataka ajaira hizo, na
kuanza kuwapa maelekezo mingine yasiokuwa au yanayofafana na ya wizara, ili
kuwatoleshea fedha.
Akizungumza na
waandishi wa habari Pemba, Katibu Mkuu wa wizara hiyo Khamis Abdalla Said,
alisema ni kweli, katika mwaka huu wa fedha, wizra inaompango wa kuajiri waalimu,
lakini nao matapeli wanaweza kutumia fursa hiyo.
Alieleza kuwa,
ndio maana wizara imeona iwatahadharishe wazazi na vijana wenyewe mapema, ili zoezi
litakapoanza lisije kuwaathiri wananchi.
Katibu mkuu
huyo alieleza kuwa, maana wakati huo wa zoezi likiwa katika mchakato, wapo
wanaoonekana kulalamikiwa, baada ya kupigiwa simu wakiahidiwa kusaidiwa kupata
ajira hizo.
‘’Wizara ya Elim
una Mafunzo ya Amali, inachukua nafasi hii, kuwatahadharisha wazazi na vijana,
wanaotaka ajira ya uawalimu, kujiweka mbali na vishoka,’’alisisitiza.
Katika hatua
nyingine, Katibu mkuu huyo Khamis Abdalla Said, alisema watakaoomba ajira za
waalimu, hakuna sharti lolote la wizara la kudai fedha, na ikitokezea hivyo
wananchi waripoti.
‘’Rais wa
Zanzibar anapotupa kibali cha uajiri cha waalimu, huwa hakuna sharti la mtaka
ajira, atowe fedha hata shilingi moja, na ikitokezea hivyo tuarifuni,’’alifafanua.
Hivyo amewakumbusha
wazazi, kuwa mchakato wa ajira za waalimu unakwenda kwa mujibu wa taratibu na nivyema
wakaitumia wizara yao, kwa changamoto yoyote.
‘’Njooni wizara
muwatumie maafisa wetu sehemu ya uajiri, iwe kwa kuuliza au kutaka ufafanuzi wa
jambo lolote, lakini msikubali kughilibiwa na wingine,’’alisema.
Baadhi ya
wazazi na walezi walikiri kuwa, suala la uchakachuaji kwa baadhi ya watu, wanaojifanya
maafisa usalama, limekuwa mara tu baada ya kutangaazwa kwa ajira.
Mmoja kati
yao, Iddi Khamis Iddi wa Machomane, alisema hata yeye mwaka jana, alitakiwa
alipe shilingi 40,000 kwa ajili ya ujazaji wa fomu, zinazokwenda Ikulu, ili
mtoto wake aajiriwe.
Nae Mayasa
Haji Mohamed wa Wawi, alisema suala la kupigiwa simu hasa kipindi cha kusubiri
matokeo ya usaili, hujitokeza mara kwa mara.
Kwa upande
wake kijana Khamis Mcha Haji, alisema suala la kuliwa pesa kwa njia ya utapeli
huwepo, na wapo wanaojua taarifa za mtaka ajira kwa undani.
Hivi
karibuni, akiwa kwenye ufunguzi wa skuli ya ghorofa ya sekondari Konde Pemba, Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi,
alisema moja ya mafanikio ya miaka minne ya uongozi wake, ni kuajiri waalimu 3,384.
Aidha alieleza kuwa, ndani ya mwaka huu wa fedha, serikali ya awamu ya nane, inayompango wa haraka wa kuajiri tena waalimu 1,239 kwa Unguja na Pemba.
Mwisho
Comments
Post a Comment