NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema
ameshayatekeleza kwa vitendo, aliyowaaahidi wananchi, ikiwemo ujenzi wa
madarasa 2,773 katika skuli zote za Unguja na Pemba.
Alisema,
Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 iliitaka serikali kujenga madarasa 1,500 ingawa
wameshavuuka lengo hilo, kwa asilimia 184, na bado kazi inaendelea.
Dk. Mwinyi
aliyasema hayo jana, mara baada ya kuifungua skuli ya skondari ya ghorofa tatu
ya Konde wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, ikiwa ni shamra shamra za
miaka minne ya uongozi wake.
Alisema, serikali
imepanga hadi kufikia mwaka 2025, iwe imeshajenga vyumba 2,000 vya madarasa katika
skuli zote za Unguja na Pemba, ili kuondoa mikondo miwili.
Alisema kama
kuna watu wanapiga porojo na kusema, uongo waangalie takwimu kutoka wizara ya
elimu, zitadhihirisha ahadi zake kwa wananchi.
Akizungumza mafanikio
mingine, alisema ni kuongezeka kwa bajeti ya mikopo ya elimu ya juu, kutoka
shilingi bilioni 11.5 hadi shilingi bilioni 33.4, jambo liliongeza wigo kwa
wanafunzi.
‘’Haya hayahitaji
porojo, maana nambari siku zote zinasema ukweli, na waje waangalie mafanikio
haya, sasa wanaopita pita wakisema hovyo, wapuuzeni,’’alieleza.
‘’Bado tuna
nia ya kweli ya kuongeza idadi ya waalimu katika ujiri, ili kuhakikisha hakuna
skuli yenye upungufu wa waalimu, kwani kwenye samani na majengo tuko vizuri,’’alifafanua.
Hata hivyo
alisema, kila skuli mpya inayojengwa kwa sasa, suala la miundombinu ya samani,
maktaba na maabara ya masomo ya sayansi ni lazima.
Alisema haya
yanafikishwa, kutokana na kuimarika kwa bajeti ya mendeleo ya wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Amali Zanzibar, kwa kufikia shilingi blioni 518 sawa na ongezeko
la asilimia 552.
‘’Ndani ya
miaka minne ya serikali ya awamu ya nane, bajeti ya maendeleo ya wizara ya
elimu imekuwa, maana kabla ilikuwa bajeti yote ni shilingi bilioni 83, ambayo
ilikuwa haikidhi haja kufanikisha haya,’’alifafanua.
Akizungumzia
kuhusu wanaobeza mafanikio hayo, aliwataka wananchi kuwapuuza na kutowaunga
mkono, na badala yake waiunge mkono, serikali ili kufanikisha malengo yake.
Hata hivyo
amewataka wanachi, kuendelea kuitunza amani na na utulivu uliopo, ili isaidie
kutekelezwa malengo yaliokusudiwa hapo kabla.
Akimkarisbisha
Rais, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, alisema wakati
huu, ndio kwa wananchi kujiimarisha, kielimu na kiuchumi.
Alisema, awamu
na nane, ndio eneo pekee kwa wananchi wa Zanzibar, kuwa makini na kujiweka tayari
kuhakikisha wanazitumia fursa zilizopo.
Hata hivyo,
amewataka wananchi wa Jimbo la Konde, kutowaunga mkono wenye nia kuchochea siasa
za fitna, kwani kwa sasa hazina nafasi.
‘’Kwa hakika,
hili linaloendelea kufanywa na Dk. Mwinyi ni jambo la kuungwa mkono, na
wananchi wa Konde, msikubali kuhadaliwa na wapinga maendeleo, ambao wanaendesha
shughuli zao,’’alifafanua.
Mapema Katibu
Mkuu, wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdalla Said, alisema
ujenzi wa skuli hiyo, ni hatua kubwa, ya kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa
utulivu.
Alieleza kuwa
ujenzi huo, unakwenda sambamba na azma ya kweli, ya Rais wa Zanzibar Dk. Hussein
Ali Mwinyi, ya kutaka kuoandoa mikondo miwili, katika skuli zote za Zanzibar.
‘’Sisi
wizara ya Elimu, tunashukuru mno kwa jitihada zako maalum kwetu, ambazo
zinachangia kwa kiwango kikubwa, kuimarisha miundombinu ya elimu nchini,’’alieleza.
Hata hivyo, amempongeza
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdalla, kwa jitihada zake,
zinazosaidia utekelezaji wa miradi hiyo.
Nae Mkuu wa
Mkoa wa kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib, alisema awali wanafunzi walikuwa
wakiingia mikondo mitatu, ingawa kwa ufunguzi wa skuli hiyo, hilo sasa
limeondoka.
‘’Sasa wanafunzi
wa skuli ya sekondari ya Konde, naamini watasoma kwa utulivu, na hakuna tena
mikondo miwili hapa, tunakushukuru,’’alifafanua Mkuu huyo wa mkoa.
Akizungumzia
ujenzi wa skuli hiyo, alisema inadhihirisha ukweli wa Dk. Mwinyi kwa wananchi
wake, ambapo aliahidi kutekeleza kwa vitendo ahadi zake.
Hata hivyo,
ameipongeza wizara ya Elimu, kutokana na juhudi zake za utekelezaji wa miradi mikubwa,
ambayo yanaendana na kasi ya Dk. Hussein Mwinyi.
Kuhusu
ujenzi wa barabara ya Finya- Kicha, alisema tayari mchakato wake umeshaanza,
hivyo wakati wowote itaanza, ili wanachi wapate kuitumia kwa nyakati zote.
Akitoa
salama za wananchi, Mwakilishi wa Jimbo la Konde Zawadi Amour Nassor, alisema
sasa Konde, inag’ara kwa kuwepo skuli za ghorofa tatu, ikiwemo Kifundi, Makangale
na Konde.
‘’Leo Konde
inang’ara kama ilivyo majimbo mingine ya Zanzibar, na hata wapo wazee 2,250
wanaopata pencheni jamii pamoja na vikundi 59 ambao wanapokea mikopo 530 kutoka
serikali,’’alifafanua.
Hata hivyo,
alisema kutokana na kasi ya Dk. Mwinyi, ya utekelezaji wa miradi mbali mbali, asiwe
na wasi wasi wa ushindi kwa uchaguzi mkuu ujao, wa mwaka 2025.
Mwananchi
aliyezungumza kwa niaba ya wenzake wa Mkoa wa kaskazini Pemba, Omar Khamis Hamad
alisema yapo mazuri yaliyofanywa na Dk. Hussein katika mkoa huo.
‘’Sisi
wananchi wa Konde na mkoa kwa ujumla, tunakushukuru sana, kwa jitihada zako
mbali mbali, na tunakuomba kuendelea kutuunga mkono,’’alifafanua.
Skuli hiyo yenye
ghorofa tatu, ina madarasa 42, yenye uwezo wa kusomewa na wanafunzi 1,890
wastani wa wanafunzi 45 kwa kila darasa moja.
Aidha skuli
hiyo ina ofisi nne za waalimu, ofisi ya Mwalimu Mkuu, ukumbi wa mkutano, vyoo
52, maabara mbili za sayansi, chumba cha TEHAMA, chumba cha ushauri nasaha
pamoja na maktaba moja na kugharimu shilingi bilioni 6.2.
Mwisho
Comments
Post a Comment