NA SALIM HAMAD, PEMBA@@@@
WAZAZI na walezi katika shehia ya
Chumbageni wilaya ya Mkoani Pemba, wamehimizwa kuwasomomesha watoto wao kitabu
kitukufu cha Qu-ran, ili kupatikana kwa kizazi chenye misingi ya maadili mema
leo na baadae.
Shekh Said Abdalla Nasor, ametoa kauli hiyo leo
Septemba 8, 2024, wakati akizungumza na wazazi, walimu na wanafunzi wa Amladrasatul
Imanniya ya Chumbageni Wambaa wilayani humo, katika mahafali ya kuwatunuku vyeti
wanafunzi waliomaliza juzuu 30, na tathmini ya mwaka uliopita kwa madrssa hiyo.
Alisema ili kupatikana kwa viongozi bora wa nchi, maimamu,
masheikhe na hata watumishi wa umma wa baadae, hakuna budi kwa wazazi katika
kuwabidiisha watoto wao, kukisoma kitabu hicho.
Alieleza kuwa, taifa linahitajia madaktari, wakuu wa
wilaya, waalimu wa madrassa na masheikhe wenye misingi ya dhati ya dini ya
kiislamu, ambapo hilo litafanikiwa, ikiwa watakisoma kwa dhati kitabu hicho.
‘’Nichukuwe nafasi hii, kuwataka wazazi na walezi
wetu, kuhakikisha tunawabidiisha watoto wetu na kitabu kitakatifi cha qur-an,
ili kupata raia wenye Imani na misingi ya dini yao,’’alieleza.
Katika hatua nyingine, sheikh Said Abdalla Nassor,
ameutaka uongozi wa madrssa hiyo, kuandaa mpango maalum, kwa ajili ya mashindani
ya qur-an, katika mwezi mtukufu wa ramadhani mwaka huu.
Mapema Mkurugenzi Uratibu wa Shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar
ofisi ya Pemba, Haji Naasor Mohamed, amewataka wazazi na walezi, kuwalipia ada za
watoto wao kwa wakati, ikiwa ni sehemu ya kuungamkono juhudi za maendeleo ya
elimu.
‘’Wapo wazazi na walezi wamekuwa walipaji wazuri wa
ada kwa watoto wao kwa masomo ya skuli, lakini kwenye madrassa shilingi 200 kwa
wiki hailipwi kwa wakati,’’alifafanua.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo Uratibu wa
Shirika la Magazeti ya serikali ofisi ya Pemba, ameahidi kusaidia gharama zote
za ujenzi wa shimo la choo katika madrassa hiyo.
Alisema, kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi katika
madrssa hiyo, amelazimika kuungano juhudi za ujenzi wa huo wa choo, ili kuwakinga
wanafunzi na magonjwa ya mripuko.
‘’Hali inatisha kwa idadi ya matundu ya vyoo ilivyo na idadi ya wanafunzi zaidi 200, nami nimeguswa na hili na naahidi kuchangia gharama za ujenzi wa shimo la choo,’’alieleza.
Hata hivyo, amewakumbusha wazazi na walezi, kuongeza
bidii katika kufuatilia nyenendo za watoto wao, ili kuwasaidia waalimu katika kufanikisha
ndoto za watoto.
Akisoma risala katika mahafali hayo, mwalimu Saleh Abdalla Mohamed, amesema pamoja na mafanikio yanayopatikana katika madrassa hiyo, bado kuna changamoto kadhaa zinazorejesha nyuma, ikiwemo uhaba wa vifaa vya kusomeshea kama vile vitabu.
Alieleza kuwa, jambo jingine ni uhaba wa makaazi,
ulipaji mdogo wa ada kwa wazazi na utoro wa wazazi kwenye vikao vya kutathamini
maendeleo.
Katika mahafali hayo, yaliambana na mambo mbali mbali
ikiwemo mashindano ya kuhifadhi qur-an, sira, fikih na qur-an tafsiri, ambapo wanafunzi17 wakiwa wote wanawake waliomaza juzuu 30 walikabidhiwa vyeti.
Mwisho
Comments
Post a Comment