NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
ILIKUA kama ndoto, kwa siku ya kwanza kati ya zile 360 zinazounda mwaka.
Ndoto hizi zilikuwa kwa waalimu, wanafunzi, wazazi, walezi wa shehia ya Mwambe Mkoani Pemba, kunawa uso
mbele ya Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali
Mwinyi.
Sio
tu kunawa uso, kwa maji kama ilivyozeeleka, wao walinawa kwa kumalizika skuli
ya msingi ya ghorofa mbili eneo hilo la Mwambe.
Hapa
wazazi, walezi, wanafunzi na waalimu, maji kwenye upindo wa kucha ya mtoto
mchanga, yalitosha kuwakogesha mwili mzima.
Furaha
yao, sio tu kuamka wakiwa wazima siku hiyo ya Januari 1, mwaka 2023, lakini ni
pale waliposhuhudia jengo la kwanza la ghorofa katika eneo la Mwambe, na bahati
nzuri sio la mtu binafsi, bali likiwa la serikali.
WANANCHI MWAMBE
Haji
Omar Kheir (65), anasema aliposikia ahadi ya rais wa sasa wa Zanzibar Dk. Hussein
Ali Mwinyi, juu ya ujenzi wa skuli ya ghorofa, hakuamini.
‘’Si
unajua baadhi ya wanasiasa wakitaka jambo lao, watakuahidi jambo hata ambalo
yeye hajawahi kuliona, wala kuliskia,’’anasema.
Kisha
kwa Januari mwaka huu, akasema sasa anakubali kuwa Dk. Mwinyi, anachokiahidi
anakitekeleza, akatolea mfano skuli hiyo ya ghorofa mbili, Mwambe.
Asha Muhsini Mohamed (45), anasema sasa baada ya kusimama kwa jengo hilo, ni wajibu wao kuwahimiza watoto kusoma kwa bidii.
Is-mail Hamdu Mjaka (25), anasema jengo hilo, alitarajia lijengwa mjini Chake chake au mjini Unguja, lakini kwa uungwana wa Rais wa sasa Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewapelekea wao.
‘’Kwa
hakika ile Mwambe wa miaka 55 iliyopita sasa imeshatoweka, na hii ya sasa ni
kama ilivyo mjini Chake chake au Unguja, kwa kuwepo kwa jengo la
kisasa,’’anasema.
Alikumbusha kuwa, yeye kuanzia darasa la kwanza hadi la nane kwa wakati huo, alisoma chini mti wa Mwembe, na kishga darasa la tisa kuingia darasani.
''Haya ni matunda makubwa kwangu, kuanzia elimu ya maandalizi mwanafunzi yumo ndani ya darasa lenye sakafu, haya ni mafanikio,''anasema.
Mshibe Ali Said (19), mwenye ulemavu wa uoni, anasema anaamini kuwa yajayo ni neema tupu na imeanzia kwao tena kwenye sekta ya elimu.
WANAFUNZI
Kazija
Omar Haji na mwenzake Asha Haji Ussi wanasema, sasa ni kazi ya kamati,
washirikiane na wazazi, ili kutimiza ndoto zao za kupata elimu.
Makame
Mcha Kheir na Abubakar Mohamed Machano, wao wanasema watasoma kwa ushindani na
skuli nyingine, hasa baada ya kupatiwa jengo la kisasa.
Wanafunzi
wanakumbuka, wakati ule walipokuwa wakiingia mikondo mitatu, wakisema hawakuwa
na mtiririko mzuri wa kujifunza.
''Kwanza darasa moja (chumba), kilikuwa na wanafunzi 104 hadi 110, hivyo lililokuwa likitawala ni fujo, na joto, lakini sasa tuna hadi mafeni,''anasema mwanafunzi Haji Mohamed Omar.
RAIS WA ZANZIBAR
Januari
hiyo 1, mwaka huu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Hussein Ali Mwinyi, alikwenda mwenyewe, kuifungua skuli hiyo mpya ya ghorofa
mbili.
Kwenye
hutuba yake fupi na iliyojaa kila kitu, alianza na kuipa agizo wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Amali, ishirikiane kwa karibu na Idara ya Utumishi, ili kuajiri
waalimu nchini.
Akasema, changamoto ya uhaba wa waalimu anaijua kuwa ipo, lakini ni vyema kwa wizara husika, kuongeza kasi ya kuajiri waalimu, na kipaumbele, iwe ni wale ambao walishajitolea siku za nyingi.
Wakati
serikali ikijenga skuli mpya zikiwemo za ghorofa, na kuzifanyia ukarabati zile
za zamani, lazima na suala la kuajiri waalimu, nalo liangaliwe kwa haraka,
alisisitiza Dk. Mwinyi.
‘’Kama
walionesha moyo wa kujitolea kwa taifa lao, kwa kuwatumikia wananchi wenzao,
sasa wakati ukifika nao kuajiriwa, wapewe kipaumbele kwa wenye sifa,’’akasisitiza.
Lakini,
kubwa na la kufurahisha kwa eneo hilo la Mwambe, ni pale Dk. Mwinyi, alipoahidi
kujenga skuli nyingine ya ghorofa, ili kukabiliana na uwingi wa wanafunzi
uliopo.
Akaeleza
kuwa, ameshtushwa na idadi ya wanafunzi wanaoendelea kuandikishwa wa darasa la
kwanza kwa mwaka huu, ambapo walifikia 970 kwa wakati huo.
‘’Kwa
hili, lazima niwaahidi wananchi wa Mwambe na vijiji jirani kuwa, serikali
itajengwa tena skuli nyingine ya ghorofa, ili kuondoa hata mikondo miwili,’’anaeleza.
Tena
hapa akagongomelea msumari kuwa, bado serikali ya awamu ya nane, itaendelea
kuona kuwa, elimu ndio kipaumbele cha kwanza, na azma ya kujenga skuli za
kisasa na vifaa vya kufundishia ipo.
‘’Ndio
maana zipo skuli 24 za zamani kwa Unguja na Pemba, zinaendelea kufanyiwa
matengenezo makubwa, ambapo kwa wilaya ya Mkoani, ni skuli za Mauwani Kiwani,
Chambani na Maendeleao Ngwachani.
Kumbe
ndani kipindi cha mwaka mmoja, serikali imeshajenga madarasa 143, kati ya hao
95 yalianzishwa kwa nguvu za wananchi na 48 ndio mapya, samba mba na ujenzi wa
vyoo 318 kwa skuli za maandalizi, msingi na sekondari mkoani humo.
WIZARA YA ELIMU
Mwenye
dhamana kuu ya elimu ya Zanzibar Leila Mohamed Mussa ambae ni Waziri wa wizara
hiyo, anasema, kwanza amevutiwa mno na kasi ya Dk. Mwinyi ndani ya wizara hiyo,
akisema imesaidiai kutatua changamoto tofauti, zikiwemo za maakazi kwa
wanafunzi.
Kumbe,
sio Mwambe pekee, lakini kila wilaya ya Unguja na Pemba, ameshaacha alama, kwa
kuhakikisha kunajengwa skuli za kisasa na za ghorofa, kuingiza na samani zake
kamili.
Waziri
huyo wa Elimu akaenda mbali zaidi, pale alimpongeza Dk. Hussein kwa kuwapatia
fedha shilingi bilioni 68, kwa ujenzi wa skuli na kutia samani.
Hata
ununuzi wa vitabu, sambamba na kukamilisha ujenzi skuli 25 za maandalizi Unguja
na Pemba, ikiwa ndio msingi wa elimu ya sekondari.
Kwake
anaona, kukamilika kwa skuli hiyo ya ghorofa mbili Mwambe, kama vile amemalizka
changamoto kubwa hasa eneo hilo.
Katibu
Mkuu wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdalla Said, akiutaja
ujenzi wa skuli ya ghorofa ya Mwambe, akasema baada ya kumalizika, sasa
umejumuisha madarasa 46, yakiwemo 25 ya zamani.
Lakini pia, akazigeukia fedha za sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar za miaka 59, shilingi milioni 450, zitawasaidia kwa ununuzi wa samani na vitabu katika skuli mbali mbali za Unguja na Pemba.
‘’Skuli
hii yenye ghorofa mbili na moja ya chini (ground) ni ya kwanza kwa
Zanzibar, ambayo itapunguza changamoto ya makaazi kwa wanafunzi wa
Mwambe,’’alieleza.
Wizara,
tayari imeshaingiza viti, meza mpya na za kisasa ndani ya skuli hiyo, na sasa
iko tayari kwa ajili ya kuhamiwa.
Afisa
Mdhamini wizara ya elimu na mafunzo ya Amali Pemba Mohamed Nassor Salim,
anasema matayarisho ya kuongoeza idadi ya waalimu skulini hapo, yameshakaa
vyema.
VIONGOZI WENGINE
Mattar
Zahor Massoud ndie mwenye mkoa wa kusini Pemba, baada ya kulishuhudia ghorofa
likiwa limesimama wima, akawakumbusha wananchi wa Mwambe, kuilinda miundo mbinu
ya skuli hiyo.
‘’Hii
ni hazina ya urithi wa elim na shilingi bilioni zaidi 3.5 zimeshatumika hadi
kukamilika, sasa lazima na sisi wananchi tuthamini jambo hili,’’anasema.
Kumbe
ndani ya mkoa huo, vipo vyumba vya madarasa 1,116 ikijumuisha hivyo 42 vya
skuli ya ghorofa ya Mwambe.
Mwakilishi
wa Jimbo la Kiwani ilipo skuli hiyo ya Mwambe, Mussa Foum Mussa, akaigeukia
serikali kuhakikisha kuwa, inaongeza idadi ya waalimu, ili kwenda sambamba na
idadi ya wanafunzi.
‘’Hapa
pana waalimu 49 tu, kwa wanafunzi 4,234 sasa lazima tuone hiyo changamoto,
baada ya kupata makaazi sasa ni ajira kwa waalimu,’’alikumbusha.
Hata
Mwalimu mkuu wa skuli hiyo, Ali Mohamed Omar, anasema ujenzi wa skuli hiyo,
umetoa mwanga mpya wa kupata elimu.
Anaona
kuwa, sasa kilichobakia ni jukumu la wazazi na walezi, kuwahimiza wanafunzi wao
ili, uwepo wa jengo hilo la ghorofa mbili, thamani yake iaendane na kasi ya
kupata elimu.
ILIKOTOKA SKULI YA MWAMBE NA SASA
Skuli
ya msingi Mwambe, iliasisi mwaka 1973 ambapo kwa wakati huo, ikiwa na wanafunzi
wasiozidi 100, na ilianza ikiwa na madarasa ya kusomea 25.
Kisha
skuli hiyo katika miaka ya 2000, baada ya idadi ya wanafunzi kuongezeka, mtindo
wa kuingia mikondo mitatu skulini hapo, ulianza.
Hadi
mwaka 2022, ndipo ilipoanza ujenzi wa skuli ya kisasa ya ghorofa moja ya chini
(ground) na ghorofa mbili za juu.
Sasa
zikijumuisha vyumba 21, na ukijumlisha vyumba vya zamani, skuli hiyo itakuwa na
vyumba 46, vikibeba wastani wa wanafunzi 45 kwa chumba kimoka kutoka 86 kwa
zamani.
Skuli
hiyo kwa sasa, ina jumla ya vyoo 30, na kila ghorofa kuwepo kwa ofisi tatu za
waalimu, achia mbali ile ya mwalimu mkuu.
Lakini
wapo wanafunzi 4,234 ikijumuisha na ile skuli kwa madarasa ya zamani, huku ile
mpya pekee, ikiwa na uwezo wa kubeba wanafunzi 1,890 kwa mikondo miwili.
Ambapo
hapo wanafunzi 945, wataingia asubuhi na wengine mchana, wakitumia vyumba 21
kwa wastani wa wanafunzi 45 kila darasala moja.
Kwa
kipindi cha miaka mitano mfululizo, skuli ya msingi Mwambe, wapo wanafunzi 820
walifanya mitihani ya taifa, lakini ni wanafunzi sita tu wa michepuo na wawili
wa kipawa maalum.
Na
ile ya sekondari, nao kwa kipindi hicho hadi mwaka 2021, hawajapata mwanafunzi
aliyepata ufaulu wa daraja la kwanza ‘division one’.
Skuli
hiyo ya ghorofa mbili ya msingi ya Mwambe wilaya ya Mkoani Pemba, ujenzi wake
umechukua mwaka mmoja, umejengwa na kampuni na Mwamba kwa shilingi bilioni
3.571 fedha za UVIKO 19, kupitia Shirika la Fedha Duniani ‘IFM’.
Mwisho
Comments
Post a Comment