MRADI wa ‘world vegetable center’ kwa
kushirikiana na wakala wa uwezesha wananchi kiuchumi (ZEEA),
wameweka mpango mkakati wa kuwapa taaluma wajasiramali wadogo, kwa lengo la
kuhakikisha wanapata soko la bidhaa zao ndani nan je ya Pemba.
Aliyasema hayo Mtaalamu wa kilimo cha mbogamboga
Renatha Edgar, kutoka mradi huo, kwenye
kiwanda cha usindikaji cha wajasiriamali kilichoko Pujini Wilaya ya Chake chake,
mara baada ya kukagua na kufanya tathmini, kwa wajasiriamali ambao wamepatiwa
mafunzo ya kuzalisha na kusarifu mchicha lishe.
Alisema, lengo la kutoa taaluma kwa wajasiriamali
hao ni kuweza kujipatia fursa mbali mbali, ambazo zitawaongezea thamani ya
bidhaa zao, na kupata soko ambalo, litawaongezea kipato.
“Kwa sasa tumepiga hatua kwa kufanya mafunzo kwa
wajasiriamali zaidi ya 200, ambao kati yao wameshaanza kufanya hii kazi, ya
kuongeza thamani za bidhaa zao kwa kutengeneza unga wa mchicha lishe,’’alifafanuwa.
Hata hivyo, alitoa wito kwa jamii kuwa na mwamko wa kuutumia
unga huo (wa mchicha lishe) ,ili kuimarisha afya zao, huku akiwaomba
wajasiriamali hao kujitokeza kwa wingi kupata mafunzo hayo ili yawasaidie katika kutengeneza bidhaa
hizo.
Naye Kaimu Mratibu Wakala wa Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (ZEEA) Haji Mohamed Haji, alisema kuwa wajasiriamali hao, wamenufaika
kupitia mafunzo hayo, na wamefikia hatua kubwa katika kuzalisha bidhaa hiyo na
kuongeza pato lao.
Aidha aliwataka wajasiriamali hao kuyatumia mafunzo
hayo, kwa kuzalisha bidhaa zilizobora ambazo zitaongeza thamani na ubora wa
kuuzika.
Kwa upande wake Msimamizi wa wajasiriamali kutoka mradi
wa ‘World Vegetable Center’ Nadra Suleiman Haji, alisema kuwa
matumaini ya mafunzo hayo ni kuendelea kuwafikia wajasiriamali wengi zaidi, ili
kufikisha taaluma ya kujikomboa kimaisha, inasambaa kwa walio wengi.
Naye mjasiriamali ambaye amenufaika na mafunzo kupitia
mradi huo, Amina Adam Makame, alisema ameyapokea mafunzo hayo na ameshawajiisha
watu wengine, ili kuzalisha mbegu za mchicha lishe, na kusarifu unga wenye virutubisho
kadhaa.
Mradi wa ‘World Vegetable Center’
ukishirikiana na (ZEEA) chini ya ufadhili ‘USAID’ kupitia Mradi wa AID- I, kwa
sasa unaendelea kuwapatia mafunzo wajasiamali ya kuendeleza biashara zao, jambo
ambalo litaweza kuinuwa vipato vyao.
MWISHO.
Comments
Post a Comment