NA ASHA ABDALLA, PEMBA@@@@
Hayo yameelezwa na Meneja wa Mradi wa
‘Eco-Schools’ Talib Kassim Abdi kwenye mafunzo ya utunzaji wa mazingira, kwa
walimu hao, waliomo katika mradi huo, yaliyofanyika ukumbi wa TASAF Chake chake
Pemba.
Alisema, ipo haja
kwa waalimu hao kuyatumia mafunzo hayo, yatokanayo na mradi huo, kwani yatawajengea
uwelewa, wakati wa kuwafundisha wanafunzi, mada zinazo za utunzaji na athari za
kimazingira zitokanazo na mabadiliko tabia nchi.
Mapema akifungua mafunzo
hayo ya siku mbili, Afisa Elimu na Mafunzo ya Amali Mkoa wa kusini Pemba, Mohamed
Shamte Omar, alisema utekelezaji wa mpango huo, ni fursa kwa wanafunzi kuzipatia
ufumbuzi changamoto za kimazingira zilizopo, katika maeneo wanayojifunzia.
Aidha aliwataka waalimu
hao, kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kwa vitendo, ili kuleta mafanikio, ikiwa
ni sehemu ya mkakati wa skuli, katika kuunga mkono Sera ya Elimu kwa maendeleo
endelevu.
Kwa upande wake
Afisa Elimu msingi Pemba, Hassan Hakim Mohamed, alisema elimu hiyo inastahiki
kusambazwa, ili ufahamu wa athari zitokanazo na uharibifu na uchafuzi wa mazingira
ufahamike.
Hata hivyo
aliwashukuru wadau wa mradi huo, kwa kuwaunga mkono, na kuendelea kuwapatia
taaluma ambayo itasaidizi kurejesha hadhi ya mazingira bora, ambayo ndio msingi
wa maisha mwanadamu.
Nae Mwalimu Fadhila
Rashid Khamis kutoka skuli ya sekondari Connecting continents ya Mgogoni Chake
chake, alisema wanajukumu kubwa kwa kuyapeleka mafunzo hayo kwa walimu wenzao
na wanafunzi, ili nawao waweze kuwa
wajumbe kwa jamii.
Waalimu 35 kutoka
Unguja na Pemba ambao wamepatiwa elimu hiyo endelevu ya utunzaji wa mazingira,
kupitia mradi wa Eco-Schools, kwa kupitia ufadhili wa Ubalozi wa Ailend nchini
Tanzania.
Ambapo mradi huo
umeshirikiana na taasisi inayo shughulikiaVijana, Elimu, Mazingira na shughuli
za kijamii "ZAYEDESA "na wizara ya Elimu pamoja na Idara ya
mazingira katika utekelezaji wake, na walengwa wa mradi huo ni wanafunzi.
MWISHO
Comments
Post a Comment