NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
UONGOZI wa shehia ya Wawi, wasaidizi wa sheria
na askari wa shehia hiyo, wametiribua mpango unaosukwa na familia, ya kijiji
cha Vikutani shehiani humo, wa kutaka kumuozesha mtoto wao, anaesoma darasa la
saba, ambae anadaiwa kuwa na ujuzito.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shehiani humo, iliyopatikana Juni 11, 2024 familia hiyo
baada ya kupewa taarifa na wasamaria wema, juu ya mabadiliko ya mtoto wao,
waliamua kumfikisha hospitali kumfanyia vipimo.
Ilielezwa kuwa, baada familia kugundua kuwa mtoto wao
anaujauzito unaokisiwa wa miezi sita, waliamua kumfuatilia kijana anaesadikiwa
kuwa amempa ujauzito huo, ili kumfungisha ndoa.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, sheha wa shehia ya
Wawi Sharifa Waziri Abdalla, alisema baada ya kugundua mpango huo, sasa
wameshaifuata familia hiyo, na kuitahadharisha juu ya uamuzi wao huo.
Alieleza kuwa, kwa sasa wamekuwa karibu mno kumfuatilia
mtoto huyo, ili kuhakikisha kwanza anarejshwa skuli, kuendelea na masomo na kuona
hafungishwi ndoa kabla ya wakati.
Alifahamisha kuwa, juzi Juni 6, 2024 aliiandikia familia
hiyo barua, ili kukutana nayo na kuiekeleza namna ya kufungua lalamiko Polisi,
ingawa ilishinwa kutii agizo hilo.
''Taarifa tulizinazo kwa sasa, wapo watu wakiwemo wa upande
wa kijana wa kiume, wanasuka mipango ili kuhakikisha mtoto huyo anaolewa,
ingawa tunapokea taarifa kila kinachoendelea,’’alieleza.
Sheha huyo alieleza kuwa, wamekuwa wakishirikiana kwa
karibu kati yake na wasaidizi wa sheria na Askari wao shehia, ili kuona
wanaifuatilia haki ya mtoto huyo.
Katika hatua nyingine, Msaidizi wa sheria wa shehia ya Wawi
Fatma Hilali Salim, alisema hakuna namna ya kesi hiyo kuimaliza kienyeji, bali
ni kwa wazazi kufungua lalamiko la ubakaji.
‘’Tumekuwa tukiwaelimisha wananchi kila siku, kwamba kesi
za udhalilishaji hazitakiwi kumalizwa kienyeji, na ndio maana tunashirikiana na
uongozi wa shehia, ili kulifikisha Polisi,’’alieleza.
Katib wa sheha wa shehia hiyo Sham Haroub Said, alisema
awali aliwapelekea wito wazazi hao, ingawa walishindwa kutii agizo na badala yake
walikimbilia kijiji jirani.
‘’Juzi tulipokwenda usiku, mama na mtoto wake ameshakimbilia
kijiji jirani, ingawa tukilimkuta kaka na baba mzazi, na tuliwaarifu juu ya
kufika Polisi na kutoa maelezo ya utuhma za ubakaji kwa mtoto wao,’’alieleza.
Baba mazazi wa mtoto huyo (jina limehifadhiwa), alisema
hana taarifa zozote za mtoto wake kuwa ni mjamzito na anahudhuria masomo ya
skuli na madarassa, kama kawaida.
Kaka wa mtoto huyo, anayesoma darasa la 12, alikiri kuwa mdogo
wake ana miezi mitano sasa, hajahudhuria masomoni, ingawa hajaelezwa lolote juu
ya tuhma hizo.
‘’Ni kweli mdogo wangu anayesoma darasa la saba kwenye moja
skuli za Jimbo la Wawi, hahudhurii masomoni, sasa ni miezi mitano na nusu, lakini
sijui kwamba amebakwa ama amejiuzia mwenyewe,’’alifafanua.
Baadahi ya wananchi wa kijiji cha Vikutani shehia ya Wawi, walisema,
mtoto huyo amekatisha masomo kwa miezi mitano sasa, na familia inazotaarifa za
uhakika, juu ya ujauzito wake.
Mwananchi huyo aliyekataa kutaja jina lake, alisema waliogundua
mabadiliko ya afya yake, ni waalimu wake, na ndipo taarifa hiyo ikafikishwa kwa
wazazi na kuamua kumfanyia vipimo.
Daktari aliyekataa kutaja jina lake wa hospitali binafsi ya
Dira Machomanne Chake chake, aliyemfanyia uchunguuzi mtoto huyo, alisema
amemgudua ana ujauzito wa miezi sita.
‘’Huyu kwa mwaka huu ni mwanafunzi tisa, kuja kuchunguuzwa
na kubainika akiwa na ujauzito, ingawa wa mwisho alionekana na ujauzito wa miezi
nane, bila ya familia kugundua,’’alieleza.
Mratibu wa Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania
TAMWA-Zanzibar ofisi ya Pemba, Fat-hya Mussa Said, alisema bado jamii, imekuwa
ikizifanyia sulhu kesi hizo, na kuviza mapambano ya kutokomeza udhalilishaji.
Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wasaidizi wa sheria wilaya ya
Chake chake Nassor Bilali Ali, aliitaka familia hiyo haraka kukimbilia Polisi
na kufungua shauri la ubakaji, na kuacha mpango wao wa ndoa.
Matukio ya ubakaji
na ulawiti yanayowakumba wanawake na watoto kwa miezi ya February na Machi mwaka
2023/2024 yaonekana kupungua na kufikia 300, pungufu ya matukio 24 kwa mwaka
jana.
Kulingana na takwimu
zilizoripotiwa kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali, inaonesha miezi hiyo Febuari
na Machi mwaka uliopita, zinaonesha kuwa ndani ya siku 59 ya miezi hiyo miwili
kumeripotiwa matukio sita, kwa kila siku moja.
Taarifa zinaeleza matukio
ni 624, yaliyoripotiwa kwa miezi minne kwa Zanzibar, na kuonesha wastani wa
matukio 56 kuripotiwa kila wilaya, kati ya 11 za hapa Zanzibar.
Mtoto huyo mwaka
2022, aliwahi kutuhumiwa kubakwa na kijana wa miaka 20 ambae ni jirani yake, na
baada lalamiko hilo kufikishwa Polisi, akimbia hadi sasa hajarudi kwao.
Mwisho
Comments
Post a Comment