ASHA ABDALLA, PEMBA@@@@
MKUU wa Mkoa wa kusini Pemba Mattar Zahor Massoud,
amewataka watendaji wa bandari ya Mkoani kisiwani humo, kufuata na miongozo iliyowekwa,
ili kutoa huduma bora kwa wananchi wanaotumia bandari hiyo.
Aliyasema hayo wakati alipokua na ziara ya kutembelea taasisi
mbalimbali pamoja na Mamlaka ya Bandari na kuelezea changamoto ambazo
zinajitokeza, katika bandari ya Mkoani kisiwani Pemba.
Alisema kua madhumuni makubwa ya ziara hiyo nikuangalia
utendaji wa bandari ya Mkoani, jinsi inavyo fanya kazi na kuangalia changamoto
za wananchi na kuona namna gani wataweza kuzitatua.
"Tumepata nafasi ya kuzungumza na taasisi mbali mbali
zinazofanya kazi bandarini hapa na tumekubaliana mambo ya msingi, namna ya
kurekebisha changamoto hizi na nmna yakuahudumia vizuri wananchi,"aliesema.
Hata hivyo, aliwaomba wanachi kutumia bandari hiyo kwa
kufuata taratibu na sheria, ambazo wanaelekezwa na uongozi, ili kuhakikisha
wanapata usafiri wa uhakika bila ya usumbufu wowote.
Kwa upande Mneja Mkuu wa Boti ya Zan Fast Ferries
Haroun Aslam Esmail, alieleza kuwa ndani ya bandari ya Mkoani, wanakabiliwa na
changamoto mbali mbali, zikiwemo ufinyu wa sehemu wanayokaa abiria, kusubiri
muda wa kusafiri.
Aidha aliishukuru serikali na Mamlaka ya bandari, kwa
kuweza kuwapa ushirikiano mkubwa, katika kufanikisha malengo yao kupitia
boti hiyo.
Nae Mkurugenzi wa tawi Shirika la Bandari Pemba Abdullah
Salum Abdullah, aliwahakikishia abiria usalama wao wakati wote wanapokuwa bandarini
hapo.
Aidha Mkurugenzi huyo aliwataka watendaji wa bandari kwa
ujumla, kuendelea kutumia bandari kwa kutii sheria ambazo zimewekwa na kuwajali
wananchi kwa kuwapa huduma bora.
Ziara hiyo ya Mkuu wa mkoa wa kusini Pemba, Mattar Zahor
Massoud, ilijuimuisha viongozi mbali mbali wakiwemo kamati ya ulinzia na usalama,
viongozi wa boti ya zan Fast ferries pamoja na Mkurugenzi wa tawi shirika
la bandari Pemba.
mwisho |
Comments
Post a Comment